Mr. Nice Aokoka! Hallelujah!

Mr. Nice Aokoka! Hallelujah!

sasa si kanisani wanaendaga asubuhi, usiku anakuwa hapao masai, na mimi nilimuona last week hapo Masai. Mbona wa kuokoka kihivyo wapo wengi tu, huwa ninakutana maskani moja na dokta remmy ongala, napiga zake urabu na bangi kisha anafanya na yale mamabo yetu kisha asubuhi anaenda kanisani kuchapa misa.

samahani nje ya mada kidogo!burn vipi tunaweza kuwasiliana?mimi ni msela tu wala usijali.ai mini mimi si yudabliyutiii.unaweza ni pm namba zako?mimi huwa najivuta pale mara moja moja
 
Mbona nimesoma jana tu kwenye magazeti kuwa ameanzisha bendi kama jibu kwa watu wanasambaza taarifa kuwa amefulia!!!!????

MN,
Habari uliyoinukuu hapa kuwa jamaa ana bendi imeandikwa na gazeti la Nipashe la tarehe 24/10/2009 na ninayo nakala yake. Jamaa kaanzisha bendi na yuko mbioni kutoa albamu mbili mpya akiwa na bendi yake hii. Sasa hizi habari za kwamba kaokoka tangu mwezi wa nane zinashangaza kidogo!
Ufafanuzi tafadhali!
 
Aliyekua muimbaji wa Dansi nchini Lucas Mkenda au Mr. NICE kama anavyojulikana na wengi amempa Yesu maisha yake tangu mwezi wa nane mwaka huu. Anahudhuria ibada, maombezi na tayari amebatizwa. Chanzo cha habari kinasema anaabudu Kawe kwa GeoDavie jijini Dar-es-salaam, tayari ana nyimbo nne za kusifu na kumuabudu Mungu. Amekua akitoa ushuhuda wake kwamba Mungu amemponya na kuyaokoa maisha yake.

mr-nice.jpg

Source:http://strictlygospel.wordpress.com/2009/10/12/mr-nice-ameokoka/

Mpendwa Lucas Mkenda, Umechagua fungu lililo Jema.
Ubarikiwe sana.
 
samahani nje ya mada kidogo!burn vipi tunaweza kuwasiliana?mimi ni msela tu wala usijali.ai mini mimi si yudabliyutiii.unaweza ni pm namba zako?mimi huwa najivuta pale mara moja moja

Usijali mkuu nitaitumbukiza kwenye inbox yako punde, hata hao UWT najua hawanitafuti si unajua mimi sio mwanakijiji wala sinaga ma issue yao uhujumu uchumi.
 
MN,
Habari uliyoinukuu hapa kuwa jamaa ana bendi imeandikwa na gazeti la Nipashe la tarehe 24/10/2009 na ninayo nakala yake. Jamaa kaanzisha bendi na yuko mbioni kutoa albamu mbili mpya akiwa na bendi yake hii. Sasa hizi habari za kwamba kaokoka tangu mwezi wa nane zinashangaza kidogo!
Ufafanuzi tafadhali!

Mkuu Nenda kwenye sosi ya habari hii!
 
Sishangai kama Mr Nice kaokoka. Maana hata alipookoka Chidumule na Lemmy wataabishaji walikuwa wengi na hawa wandugu bado wameokoka.

Inawezekana kwamba ni kweli ameshuka kichati katika muziki, mimi sikatai. Lakini kama kasikia sauti ya Yesu kuwa anahitaji kuingia katika maisha yake na kutawala na yeye amekubali, siangalii masuala ya pesa lakini naangalia uamuzi wake. Amelamba DUME.

Mr Nice songa mbele. Usijali maneno ya watu maana hata sisi walitusema hivyo hivyo na bado tumeokoka na Yesu ni mwokozi wetu. Tunapeta mbele.

Yesu alikuja kwa ajili ya wakosaji si wenye haki. Wale wanaodhani hawamuhitaji kwa sababu bado wana vijisenti vyao wasome Yohana 3:16-18
 
KILA JUMANNE:huwa anatumbuiza MASAI CLUB pale karibu na mango-garden.halafu jamaa anaongoza kwa kuomba bia mazee!yani akishaingia tu inabidi wadau tujifiche,maanake ni kama luba.

kwa mfanu jumanne iliyopita alikunywa sana konyagi.............

anaebisha tukutane nae kesho club masai

Nakubali maneno yako, Jumanne ya kuamkia Nyerere day alituburudisha hapo Maasai Club
 
Mimi naomba kuuliza swali...Kila siku nasoma post za watu humu ndani kuna hili neno "FULIA"...Linatumika sana lakini hata sijui maana yake ni nini?...kama kwenye hii topic limetumika 10 Times....na kila nikijaribu kusoma sentensi nashindwa kuelelewa maana ya Fulia naomba msaada please anayejua maana yake.....
 
Mr. Nice kufulia anapenda mwenyewe, atafute sponsor ampeleke Msumbiji miji ya Pemba, Nampula, Beira, Mocimboa akaimbe nyimbo zile zile za Kilakshari, kule wanamhusudu kinoma! Ajifue, akafanye maconcerts. Mr. Nice enzi zake alikuwa ni MC pekee Tz mwenye uwezo wa kuperform kwa zaidi ya masaa matano mfulilizo jukwaani bila kuchoka.

Mbona nyimbo za zamani kama Jojina hadi leo zinapendwa? Kwa wengi Mr. Nice bado ni star; mbinu tu za kurudi kwenye gemu zimemwishia. Akaanzie nje.
 
Mimi naomba kuuliza swali...Kila siku nasoma post za watu humu ndani kuna hili neno "FULIA"...Linatumika sana lakini hata sijui maana yake ni nini?...kama kwenye hii topic limetumika 10 Times....na kila nikijaribu kusoma sentensi nashindwa kuelelewa maana ya Fulia naomba msaada please anayejua maana yake.....

Neno "Fulia" lina maana kuwa umeloweka nguo kwenye maji (suruali, shati e.t.c) na kuanza kufua (weka sabuni na pikicha), na ghafla unagundua kuwa katika ile nguo (baada ya kusuuza na kuanika) kulikuwa na kitu chako cha maana (pesa, saa, e.t.c) na tayari kimelowana na kuaharibika.

Kwa sentensi unaweza sema "Nimefulia hela yangu kwenye shati". . .

Lakini sasa katika harakati ya kutafuta uwezo wa kwenda "ch**ni" waigizaji wa vicheckesho wa television wametumia neno "fulia" wakimaanisha "kuishiwa pesa" kwa mtu ambaye hapo awali alikuwa nazo.
 
Neno "Fulia" lina maana kuwa umeloweka nguo kwenye maji (suruali, shati e.t.c) na kuanza kufua (weka sabuni na pikicha), na ghafla unagundua kuwa katika ile nguo (baada ya kusuuza na kuanika) kulikuwa na kitu chako cha maana (pesa, saa, e.t.c) na tayari kimelowana na kuaharibika.

Kwa sentensi unaweza sema "Nimefulia hela yangu kwenye shati". . .

Lakini sasa katika harakati ya kutafuta uwezo wa kwenda "******" waigizaji wa vicheckesho wa television wametumia neno "fulia" wakimaanisha "kuishiwa pesa" kwa mtu ambaye hapo awali alikuwa nazo.

Thank you Baba_Enock.....so kufulia ni kuishiwa i will keep that in mind.....
 
ina maana MR nice mziki wake ulikuwa unaenda na ushirikina

looh maybe ndo maana kaamua kurudi kundini
Mkuu, nini Mr.Nice...wanafanya kufuru kina J-zee,P.Diddy na wenzao...kuna kundi la akina dada linaitwa Pussy cate dolls, hawa uchawi wao hauna kificho hata kidogo, wapo Black eyed pies,wanatisha hata sura zao...mkienda katika kumbi za starehe..muwe waangalifu kuna mambo ya ajabu ajabu...yanakirihisha hata kuyasema hapa utatishika tu...kuna bendi Tz inatumia mtindo wa 'sayansi' ya kinu na mchi...hawa wana mizimu yao Ifakara huko...hata aondoke nani hawashuki.
 
eeeeh duniani kuna mengi sawa sawa na bahari kuna papa na nyangumi tena wale wa hatari
 
Muongo mkubwa huyu BAZAZI baada ya kujiona KAFULIA ndio ameamua kuokoka.
 
Aliyekua muimbaji wa Dansi nchini Lucas Mkenda au Mr. NICE kama anavyojulikana na wengi amempa Yesu maisha yake tangu mwezi wa nane mwaka huu. Anahudhuria ibada, maombezi na tayari amebatizwa. Chanzo cha habari kinasema anaabudu Kawe kwa GeoDavie jijini Dar-es-salaam, tayari ana nyimbo nne za kusifu na kumuabudu Mungu. Amekua akitoa ushuhuda wake kwamba Mungu amemponya na kuyaokoa maisha yake.

mr-nice.jpg

Source:http://strictlygospel.wordpress.com/2009/10/12/mr-nice-ameokoka/
Pesa iko kanisani kwa waimbaji! Waimbaji mnaokazania kuimba kwenye maholi ya muziki hamjui wapi iko sukari.

Chidumule alishaonyesha njia na anamapesa balaa kwa kutumia sauti yake tu. Nashangaa kwa nini waimbaji hamuoni hayo!

Mr Nice kaliona hilo, na subiri baada ya mwaka mmoja tu halafu angalieni maisha yake.

Utapeli wa uhakika uko kanisani. Lakini lazima uchague moja ya kanisa la Pentacoste, usifanye makosa ukaenda makanisa uchwala yasiyokomaa katika utapeli.

Hapendwi Mungu hapa, hupendwa pesa tu.
 
This is good marketing strategy for Mr. Nice, kaona kurudi juu tena haitawezekana,njia pekee iliyobaki ni kupitia "gospel", ila sijuwi kama ile miiko ya kiganga ndo imekwisha na jamaa yupo "free" sasa au vp, maana sifikirii kama gospel inaendana na uchawi.

Mkuu,
Ukimtafuta undani wa huyo mhubiri utagundua kwamba assumption yako hapo juu (bold ) ni wrong. Jamaa kaaga kwa wazee, na anatumia nguvu za ajabu na ni vigumu kuwa ni za kiMungu. Siwezi kwenda ndani sana, maana jamaa ni CIA mazima!
 
Natamani awe ameokoka kweli-kweli lakin wasiwasi wangu anaweza kuwashambulia kondoo wa Bwana kwa staili ya ajabu mmh1
Duh mzee umewaza mbaaalli. lakini inaweza tokea bwana mana shetani ana njia nyingi.
 
Kelly01 na Baba_Enock ahsante kwa swali na jibu la 'kufulia' nilikuwa naona neno likitumiwa lakini nilikuwa sijui linamaanisha nini. Ahsanteni.
 
Back
Top Bottom