Mr Pompeo: Wenye kudhulumu haki ya kuishi wapo Minneapolis

Mr Pompeo: Wenye kudhulumu haki ya kuishi wapo Minneapolis

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2015
Posts
18,487
Reaction score
13,611
Niliusoma ule ujumbe wa waziri wa mambo ya nje wa Marekani kumhusu mkuu wa mkoa wa Dar juu ya watu kudhulumiwa haki ya kuishi, kichwani mwangu zikaja kila aina ya fikra. Zilikuwa ni tuhuma nzito zilihitimishwa kwa RC wa Dar kunyimwa haki ya kuingia Marekani.

Lakini kesho hakuna binadamu aijuaye namna inavyofanana. mapolisi wa Minneapolis wamemnyanyasa na kumnyima haki ya kuendelea kuishi George Floyd akiwa ni kijana wa miaka 46. Dunia nzima imeona tukio lote lililovyokuwa kwanza likirekodiwa na kamera za CCTV za jengo moja na pili kwa video fupi jongevu iliyochukuliwa na mpita njia.

Maandamano yanaendelea ulimwengu mzima, hasira zimewawaka watu wa kila rangi, watu weusi wakiwa ndio viongozi wa maandamano. Kule Uingereza wananchi wanaiangusha minara yenye kusimama kama kielelezo cha biashara za kitumwa.

Wamarekani wanabeba mabango yenye maandishi yasemayo DEFUND POLICE yaani bajeti zinazotengwa kwa ajiii ya polisi na zipitiwa upya, wengine wanashauri mifumo ya utendaji kazi ya polisi na yenyewe ipitiwe upya.

Siku zote kauli huwa zinaumba, Donald Trump na msaidizi wake Pompeo hawajifunzi lolote kuhusiana na hekima hii ya miaka na miaka, kwao kuongea mambo bila kuangalia madhara yake sio kitu muhimu.

Wenye kudhulumu haki ya kuishi ni polisi wa Marekani, kwani dhuluma yao inasababisha ulimwengu mzima kuandamana. Dhuluma ya Marekani ni mbaya sana kwani ni ya miaka na miaka, kule kwenye majimbo ya kusini yenye weusi wengi kumekuwa na sehemu ambazo mtu mweusi haruhusiwi kuvuka. Akithubutu basi haki yake ya kuishi inakuwa imechukuliwa bila ya ridhaa yake.

Yale maandishi ya Pompeo yenye kumuongelea RC wa Dar namna anavyodhulumu haki ya kuishi yamemgeuka yeye na bosi wake. Wao ndio wenye kudhuluma haki za watu za kuishi tena ni utamaduni wao kwa miaka zaidi ya mia nne.
 
Lumumba hamna akili kwa kweli. Huyo Pompeo unayemsema tayari Marekani wameshachukua hatua ya kuwafukuza kazi hao Askari Waane waliomuua George Floyd na wameshakifikishwa mahakamani. Nyie Makonda aliyewekewa travel ban mmemfanya nini????

Kweli Elimu ni Tatizo sana Bongo
 
Hii takataka ingekuwa vyema umtumie kwenye email yake , humu huwa hapiti huyo. Polisi aliyeuwa hatua za kinidhamu na kisheria zinachukuliwa dhidi yake.

Je, wale waliomuua Akwilina mliwafanya nini!? Kwani Bashite lazima aende Marekani!? Mnawaita mabeberu huku bado mnajipendekeza kwenda kwao. Kwa nini msiende wa wazalendo uchwara wenzenu!? Sheeenzy sana.
 
Tatizo la Marekani na Tanzania ni Marekani Polisi Wanaua bila kutumwa na wanasiasa ila Tanzania Police wanaua kwa kutumwa na wanasiasa.

Yaani kiufupi mauaji ya polisi Tanzania ni political idelogy matter ila US ni polisi anaua kwa msukumo wake mwenyewe sio kwa kutumwa na mtu tofauti na bongo ambapo mtu anaweza wahonga mapolisi na kuwapa vitu kibao ili waende kutekeleza matakwa yake. bashite ni gaidi.
 
Tatizo la Marekani na Tanzania ni moja Marekani Poli Wanaua bila kutumwa na wanasiasa ila Tanzania Police wanaua kwa kutumwa na wanasiasa.
Polisi wa Marekani hawaui. Ni incidents tu, leo hii Polisi wa Tanzania wakiambiwa wawe na body cameras na dash camera si mtaanguka mfe.
 
Kwa hiyo tunguli limepigwa mwana kulitafuta mwana kulipata nao yawakute-toa kwanza boriti(gogo kubwa linalofunga macho usione-USA)endani ya jicho lako ndipo uone kibanzi(kijiti kidogo-TZ)
 
Tatizo la Marekani na Tanzania ni Marekani Polisi Wanaua bila kutumwa na wanasiasa ila Tanzania Police wanaua kwa kutumwa na wanasiasa.

Yaani kiufupi mauaji ya polisi Tanzania ni political idelogy matter ila US ni polisi anaua kwa msukumo wake mwenyewe sio kwa kutumwa na mtu tofauti na bongo ambapo mtu anaweza wahonga mapolisi na kuwapa vitu kibao ili waende kutekeleza matakwa yake. bashite ni gaidi.
Dunia nzima inaandamana kwa sababu haki ya kuishi ya George Floyd imedhulumiwa, hakuna anayeandama eti kwa kigezo cha RC wa Dar kudhulumu haki ya mtu ya kuishi, huo ushahidi upo wapi?. Unaweza kuwekwa hadharani kama ule wa mauaji ya Floyd ambao upo katika simu za watu?.
 
Polisi wa Marekani hawaui. Ni incidents tu, leo hii Polisi wa Tanzania wakiambiwa wawe na body cameras na dash camera si mtaanguka mfe.
Jenga tabia ya kuangalia documentaries mbalimbali za Marekani zenye kuhusiana na unyama wa polisi magerezani na katika ukamataji wa watu, zitakusaidia kuondokana na hayo maoni uliyonayo sasa.
 
Lumumba hamna akili kwa kweli. Huyo Pompeo unayemsema tayari Marekani wameshachukua hatua ya kuwafukuza kazi hao Askari Waane waliomuua George Floyd na wameshakifikishwa mahakamani. Nyie Makonda aliyewekewa travel ban mmemfanya nini????

Kweli Elimu ni Tatizo sana Bongo

Wameacha akili nyumbani.
 
Jenga tabia ya kuangalia documentaries mbalimbali za Marekani zenye kuhusiana na unyama wa polisi magerezani na katika ukamataji wa watu, zitakusaidia kuondokana na hayo maoni uliyonayo sasa.
Ninaweza kuwa mtu pekee nayeangalia Tv duniani kuliko mwanadamu yeyote.
.
Hapa kwenyewe naangalia hakuna channel siijui hadi za Thai sijui Peru am so good in that sector.
Sasa wewe kutazama kwako hizo footages za NAT GEO zinazoonyesha magereza ya Los Angeles unaona basi ndivyo hali ilivyo ahahaha!
Hizo unakuta zimerekodiwa miaka 10 iliyopita huko.
.
Violence America zipo ila sivyo mnavyotaka kuaminisha watu huku we're safe
 
Dunia nzima inaandamana kwa sababu haki ya kuishi ya George Floyd imedhulumiwa, hakuna anayeandama eti kwa kigezo cha RC wa Dar kudhulumu haki ya mtu ya kuishi, huo ushahidi upo wapi?. Unaweza kuwekwa hadharani kama ule wa mauaji ya Floyd ambao upo katika simu za watu?.
Wakishafanya uharamia wao wanang'oa kamera zooote eneo Hilo ushahidi utaupatia wapi mkuu
 
Violence zinaweza kuwa za miaka kumi iliyopita lakini mpaka leo hao hao weusi wanalalamikia systematic racism. Wanalalamikia uonevu wa mtu mweusi anapokuwa mikononi mwa polisi.

Pompeo aliongea kama monita au kiranja wa dunia kuhusu haki za binadamu, unyama aliofanyiwa Floyd umemuumbua.
 
Wakishafanya uharamia wao wanang'oa kamera zooote eneo Hilo ushahidi utaupatia wapi mkuu
Bado ni dhana za kufikirika za baadhi ya watu huwezi kuzilinganisha na udhalilishaji wa wazi aliofanyiwa marehemu George Floyd.
 
Dunia nzima inaandamana kwa sababu haki ya kuishi ya George Floyd imedhulumiwa, hakuna anayeandama eti kwa kigezo cha RC wa Dar kudhulumu haki ya mtu ya kuishi, huo ushahidi upo wapi?. Unaweza kuwekwa hadharani kama ule wa mauaji ya Floyd ambao upo katika simu za watu?.
Unapohalalisha ukatili wa Makonda kwa refence ya kitoto kama hii wewe ni Zuzu.
 
Back
Top Bottom