Mradi gani wa kiuchumi unaweza kuanzisha kwa kutumia fedha za mafao kiasi cha Tshs 90,000,000/-?

Mradi gani wa kiuchumi unaweza kuanzisha kwa kutumia fedha za mafao kiasi cha Tshs 90,000,000/-?

FDs are currently at around 4-6% annually, hiyo 50m ukiiweka kwa rate ya 6% at the highest unapata 3m less 300,000 (10% WHT). Net ni 2,700,000 ambayo ni 225,000/- kwa mwezi.

Unaweza kufanya hiyo biashara?
Weka hiyo milioni hamsini kwenye fixed deposit kama alivyoshauri mtu mmoja hapo juu,faida yake tu inamtosha kwa matumizi,ukichukulia bado tena anavuta kwa mwezi,hiyo arobaini inayobaki fanya investment
Hiyo faida unayosema kuwa itakuwa inamtosha kwa ajili ya matumizi ni kweli itamtosha lakini kumbuka hiyo 50m mwisho wa siku itakuwa ndiyo hiyo hiyo huku thamani yake ikiwa imeshuka maana thamani ya 50m ya leo siyo sawa na thamani ya 50m ya miaka mitatu ijayo.

Kwa maoni yangu kama angepata sehemu nzuri na akanunua kaeneo na kujenga fremu za kukodisha kama nne tu za kawaida kwa ajili ya biashara kwa mwezi atakuwa hakosi laki nne na wakati huo eneo lake likipanda thamani kila mwaka. Uzeeni hakuhitajiki kazi zenye changamoto sana.
 
Mkuu hapo kwenye kununua nyumba mjin, mama angu kastaafu aisee kakomaa sana kununua nyumba mjin cjui apangishe, nimajaribu kuzuia imeshindikan

Sent using Jamii Forums mobile app
Ha haaa haaaaa bora mumuache Maana mkimshauri ishu nyingine bahati mbaya ikaenda ndivyo sivyo atawasikitikia mpaka anaondoka duniani [emoji23]

Sema mumsaidie asipigwe na wajanja mjini Maana utakuta kijumba cha hovyo tu analizwa mamilion ya kutosha
 
Ni kila baada ya miezi mitatu kiuhalisia ila kuna utaratibu mpya wa kupata kila mwezi ila ni kidogo sana kuliko ile ya miezi mitatu
Ndo ninavyojua mkuu! sasa nimeshangaa mama wa ndugu yetu nje ya kustaafu anaendelea kulamba laki 5!
 
Afanye biashara ya urembo au vitu vya kike, hasahasa Handbags za jumla unazifata nje ya nchi, achukue frem kariakoo au mwenge....atumie kama 30milion au 40 milion..handbags znalipa

Au afungue pub au bar ya kueleweka pande za dodoma.

Pia atafute eneo afanye ufugaji wa kuku mdogo kama kurelax anakuwa anatembelea eneo lake weekend.

Anunue viwanja vilivyopimwa vya bei ya chini visivyopungua vi4 ..vya bei kama milion 4 au 5... Atatumia kama 20 m...baaa ya miaka mi2 au mi3 ardh inapanda thaman hivyo itambackup endapo kama mirad yake itayumba anauza viwanja vyake maisha yanakwenda..

Pesa nyingne anajenga nyumba na kutafuta usafiri wa kawaida ili asipigwe na jua..kagar ka bei poa tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuchukua fremu Kariakoo tena wakati watu kule wanafunga biashara kila kukicha? Hii ni awamu nyingine.
 
Soma ulichokiandika juu 👆 na hapa chini 👇 haueleweki
Mkuu utakuwa tu hajanielewa vizuri,mtumishi wa serikali anapostafu unapewa pension ya kila mwezi hadi siku ikifariki ambapp kwa mama yangu anapewa tshs.laki 5.
Tshs 90M ninayoizungumzia hiyo hupewa lumpsum kama kiunua mgongo-ambayo kimsingi ni hela ambayo hukatwa katika mshahara kipindi ulikuwa mtumishi
 
Asiwekeze hela nyingi hivyo ikiwa hela yenyewe ndio hiyohiyo.

Yaani anastaafu bado anawaza kuwekeza hela zote hizo??
Agawe nyingine ale Bata kishafika miaka 60 bado anajibana.

Awekeze angalau 50.

Lkn pia agawie na watoto japo hata 2M each.

Ushauri akaweke fixed akaunti awe anakula Kila mwezi

Sent using Jamii Forums mobile app
Hilo nalo neno japo watoto nao wafaidi matunda ya mama kidogo
 
Kwa kupitia michango ya wadau na wewe nimeona mahali kwamba ana grocery na atakuwa anapata 500,000 kwa mwezi, hiyo inatosha maisha.

Kitu cha kufanya (ninavyoona mimi), atafute kiwanja kwenye makao makuu ya mkoa (mil 10,000/- unapata eneo kubwa ambalo halijapimwa), ukubwa wa kutosha kama sq 1500+.

Hapo anaweza kujenga nyumba 3 simple, za vyumba vitatu kila moja kwa estimate ya 25m kama akisimamia yeye mwenyewe.

Zikiisha hakosi wapangaji hata kwa 200k per month.

Pia anaweza kuzijenga kwa kujitegemea kila moja kivyake ili akiamua kuuza iwe rahisi.
Ushauri mzuri sana huu bro
 
Mkuu cha kwanza asigawe pesa kwa mtu yyte katika familia maana watoto mzee akistaafu ndio hujikomba na kumpa miradi hewa mzee kwa tamaa mwisho atakufa kwa presha cha pili kwa kuwa mama alikua na grocery maana ake ana uzoefu kdgo na biashara ya vinywaji so aongeze mtaji pale kwa kuboresha na isizid mill 30 au kama anaweza pata sehem nyngne nzuri kwa biashara hio afungue pub nzuri tu isizid mill 30 then nyingne atafute viwwnja hasa dodoma vile vya kupimwa na serikali anunue hata vinne kwa mill tano tano baada ya miaka miwil atauza bei nzur sana na inakua back up yake incase mambo mengne hayaenda vzr na mill 10 atafute kausafir aisee na hizo 30 znazobak aweke kwenye fixed acc za kusoma upepo maana biashara saiv kwa tz lazma uwe na timing.
 
Mkuu nakushauri utembelee washauri wa UTT
ukiongea nao unaweza kuwekeza mfano milioni 50
ambapo utakuwa na uwezo wa kupata faida ya shilingi
milioni 1 kila baada ya miezi 3.Uzuri ni kwamba mtaji wako utakuwa salama.
Hiyo 40M itakayobaki ndo uhangaike nayo
kwenye biashara kama walivyoshauri wadau wengine.
Binafsi naona kuwekeza fedha kwenye
taasisi zenye mfumo wa fixed account ni nzuri
maana unapata faida na mtaji wako unakuwa salama,
kuliko biashara au kilimo ambapo unaweza kukosa faida
na mtaji ukapotea,na huo ndo mwanzo wa stress.
 
FDs are currently at around 4-6% annually, hiyo 50m ukiiweka kwa rate ya 6% at the highest unapata 3m less 300,000 (10% WHT). Net ni 2,700,000 ambayo ni 225,000/- kwa mwezi.

Unaweza kufanya hiyo biashara?
Mkuu kumbuka hela zinazowekwa fixed a/c huwa kuna riba ukiwa unatoa,so hiyo amount hapoo juu itapungua.
 
Mkuu utakuwa tu hajanielewa vizuri,mtumishi wa serikali anapostafu unapewa pension ya kila mwezi hadi siku ikifariki ambapp kwa mama yangu anapewa tshs.laki 5.
Tshs 90M ninayoizungumzia hiyo hupewa lumpsum kama kiunua mgongo-ambayo kimsingi ni hela ambayo hukatwa katika mshahara kipindi ulikuwa mtumishi
Nafahamu hilo mkuu, lakini katatizo kangu ni kadogo tu kuhusu kupewa laki tano kila mwezi umetumia wakati uliopo (Yani amekwisha staafu)
.
Na kuhusu pensheni umetumia wakati ujao hata ukisoma quotation yako hapo juu utaliona nalo lisema, alafu hakuna mfanyakazi wa umma ambae ametumikia kada ya ualimu, uaskari n.k (SI KADA ZOTE) anaepokea pesa nyingi kiasi hiko.
.
Waziri mkuu akistaafu anapokea nadhani asilimia 75-80 ya mshahara Raisi ni 90 kama sjakosea sisi wengine tukistaafu asilimia 50 ya mshahara yenyewe haifiki
 
Ushauri wa bure,
Cha kwanza mayai huwa hatushauri yabebwe kwenye kapu moja ni hatari,
Hapa namaanisha si vema mama akachukua pesa yote akawekeza kwenye mradi ni hatari kwani ikitokea tatizo pesa yote itakiwa hatarini labda tu kama itafanyika stadi yakutosha kuhakikisha usalama wa maradi wenyewe.
Cha Pili kwa umri wa mama yako kwakuwa ameshafika utu uzima tambua kila kunapokucha uwezo wake kwenye kila idara unashuka hapa namaanisha utendaji kazi kwa ujumla ufanisi unaathiriwa na uzee.
Nashauri mama asilimia kubwa ya pesa yake ajenge nyumba za wapangaji apangishe kwani hizi hazihitaji usimamizi wa karibu hata kwa utu uzima wake haitakuwa shida.
Abakize pesa kidogo ndio atumie kwenye miradi inayoshauriwa na wengi kama ufugaji nk.
Uwekezezaji wa hisa kwenye taasisi ambazo zipo imara zenye record yakukuwa kila mwaka nayo ni option nyingine kwani baada yakununua hisa mama yeye atasubiri gawiwo.
Wengi wanashauri sana ufugaji wakifikiri ni rahisi lakini kwa umri wa mama tena mama ambaye hapo mwanzo hakuwahi kufuga haitakiwa rahisi kwake.
Al da best!
 
FDs are currently at around 4-6% annually, hiyo 50m ukiiweka kwa rate ya 6% at the highest unapata 3m less 300,000 (10% WHT). Net ni 2,700,000 ambayo ni 225,000/- kwa mwezi.

Unaweza kufanya hiyo biashara?
Mkuu pia kumbuka kuweka pesa fixed account kwenye utawala wa JPM napo ni risk kubwa-unaweza kutokewa na kama kilichowatokea wateja wa M-bank
 
kama hajawahi kufanya biashara yoyote basi mshauri asijifunze sasa.aweke 80m kwenye fixed deposite wakati anatafakari.halafu achukue 9m aende akakopeshe wanaolima mpunga huko ubaruku Mbeya.watamdhulumu 3m halafu hiyo m6 watamlipa mpunga atakao uza kwa 13m.mwaka unaofuata atakuwa ameshakuwa mwenyeji.na akili itakuwa imeshakaa sawa.ndiyo anaweza sasa kuchukua benk M15 zingine aanze kilimo mwenyewe.kwa sasa asijaribu kuwekeza hela yote atakufa kwa presure. kwa sababu hata wewe mwenyewe utachangia kuzitapanya
 
Back
Top Bottom