Mradi gani wa kiuchumi unaweza kuanzisha kwa kutumia fedha za mafao kiasi cha Tshs 90,000,000/-?

Mzee ni kweli kabisa
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii nayo ni nzuri
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu pia kumbuka kuweka pesa fixed account kwenye utawala wa JPM napo ni risk kubwa-unaweza kutokewa na kama kilichowatokea wateja wa M-bank

Yes, ukiangalia mahesabu hayo utaona siyo akili kuweka fixed deposit, unapata 3m kwa mwaka kwa kuweka 50m. Wakati huo huo capital inazidi kushuka thamani (kumbuka issues za time value of money).

Ukichukua hiyo 50 ukajenga vijumba viwili hukosi 200,000 kwa kila kimoja kwa mwezi, na at the same time thamani inazidi kupanda au inabaki pale pale.
 
Mkuu mama alikuwa mwalimu ameanza kazi 1981 akiwa na miaka 18 alipomaliza tu std 7,amsitafu mwaka jana mwezi wa 7.hadi anastafu mshahara wake ulikuwa mkubwa tu ndio maana pension yake ilikuwa nzuri kiasi na ni mimi ndio nilikuwa nafatilia hizi insu zake alipostafu.
 
Mwambie Mama mtembelee crdb bank wana account maalum unaweka fedha pale wao kila mwezi wanakuingizia kiasi Fulani kulingana na makubaliano,mwishoni mwa mkataba kwa mfano miaka miwili unaweza kuchua pesa yako au unaendelea nao.
Kwa makadirio ukiweka 90,000,000 utakua unawekewa kwenye account yako 1,000,000.
Tembelea Crdb kwa maelezo zaidi
 
Wastaafu wengi huwa wanafeli kibiashara naongea kwa mifano zaidi ya 10 ambayo nimeona,ila mstaafu akiwekeza kwenye nyumba za kupangisha hufanikiwa sana
Mkuu kuwa mchumi sio kujua kila kitu,haya mambo ya uwekezaji yanahutaji ideas pia.
Pia hajapanga ku invest 90M mahali pamoja ndio maana nimeandika huu uzi kuomba ushauri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umuige mtu aliyekuwa rais ambaye hata ufugaji wake ni kwa ajili ya kupigia picha????
 
Kwako uliyestaafu. Acha kabisa kuweka pesa zako kwenye mradi kwa vile wewe siyo mfanyabiashara mzoefu. Nakushauri kama ifuatavyo:- Hizo hela zako 90,000,000 ziweke kwenye fixed account kwenye Benki ya NMB. Kwa sasa wanatoa riba ya asilimia 9.5 na unaweza kukubaliana nao kukupa riba yako kwa mwezi. Nikupe hesabu ya riba yako kwa mwezi. 90,000,000 x 9.5/100 = 8,550.000 (faida kwa mwaka) toa kodi ya Serikali asilimia 10 = 7,695,000 (faida kwa mwaka) gawanya kwa 12 ili upate riba yako kwa mwezi = Tshs.641,250(riba ya kila mwezi) unayopata kila mwezi na huku fedha zako zikiwa salama. Hapo bado unapata pensheni yako ya kila mwezi. Achana na biashara fedha zako zitapotea. Biashara hakuna usalama wa fedha zako.
 
Kivipi mkuu yaani milioni moja kila mwezi,mwaka au miaka?
 
Mwenye uelewa mzuri wa manunuzi ya treasury bills (hati fungani za serikali) atoe ushauri hapa kwa kuzingatia hali halisi ya sasa ya uchumi hapa nchini ili kama huyu mstaafu anaweza kuwekeza katika hizo treasury bills afanye hivyo.
 
Hizo hela anapata kila mwezi na anaweza kuvunja mkataba na Benki wakati wowote akipata shida inayohitaji matumizi ya kiasi cha fedha hizo. Kama yuko karibu na Benki anaweza kuwatembelea Tawi lolote la NMB kwa maelezo zaidi.
 
Kila mwezi,inaitwa Thamani A/C,hayo ni makadirio tu ,lakini wanalipa vizuri sana kuliko fixed A/C kama ukiweka kiasi kizuri kama hicho
Lakini hii Thamani Account ukiweka fedha maturity yake si ni miaka mitatu japo utakuwa unapewa faida kwa kila mwezi na ukiamua ku uplift kabla ya huo muda utaambulia hasara?
 
Lakini hii Thamani Account ukiweka fedha maturity yake si ni miaka mitatu japo utakuwa unapewa faida kwa kila mwezi na ukiamua ku uplift kabla ya huo muda utaambulia hasara?
Ni kweli ukitaka kuzitoa kabla ya maturity wanakulamba kwa sababu umevunja mkataba
 
Kuweka 90 m yote kwenye mradi Ni hatari.
Kumbuka biashara Ina faida na hasara,, anything may happen

Ni vizuri angetenga AMT flani aweke fixed account,nyngne atafute mradi awekeze uko,,nyngne kwa ajili ya matumiz ya Kila siku

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Soma ulichokiandika juu 👆 na hapa chini 👇 haueleweki
Nadhani yuko sahihi,Kuna ile pensheni ya kila nwezi ambayo nadhani ndio hiyo 500,000 na kiinua mgongo, ambayo ni ya mkupuo hulipwa once, kwa jinsi taratibu zilivyo mtu kustaafu mara moja au ndani ya muda mchache anaanza kupata pensheni ya kila mwezi, hiyo ya mkupuo huchelewa kwa muda fulani!
 
Nilipata kuambiwa kuwa wao NMB wana Bonus Account ambapo riba yao kama faida kwa mwenye akaunti ni 13% kwa mwaka nadhani ndiyo hii unayozungumzia. Je hiyo riba kwa sasa imeshuka? Tatizo nililoliona kuhusu hii akaunti ni kwamba wao faida ulipa kila baada ya miezi mitatu mitatu na siyo kila mwezi japo napo itategemea na uhitaji wa pesa kwa mwenye akaunti maana kwa mwingine angependa apate fedha hiyo baada ya kupita miezi kadhaa mbele. Je, una hakika kwamba kwa sasa wanalipa hiyo faida kila mwezi na siyo kila baada ya miezi mitatu?

Mhusika akiamua kufungua fixed deposit account itakuwa vizuri akalinganisha zote mbili yaani Thamani Account ya CRDB na hii Bonus Account ya NMB.
 
Mkuu nadhani umehitimisha mjadala huu ndio ushauri wa kuchukua!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…