Mkuuu miradi inayohusu Ujenzi wa Majengo haijawahi kumliza mtu kama umenunua kiwanja sahihi.Wana JF habari zenu,
Mama yangu baada ya kunusurika na kikotoo ameniomba nimshauri kumpendekezea mradi ambao anaweza akaanzisha na kuusimamia yeye mwenyewe, pesa anazotegemea kupata ni Tshs. 94,000,000.
Fedha anayotegemea kuanzishia mradi ni tshs 90,000,000.
Nimeona ni vyema kuwashirikisha kupata mawazo mbadala, pkwa kuwa ninaamini baadhi yetu wazazi wetu walistaafu na kuanzisha miradi ambayo imekuwa imara na endelevu mpaka sasa.
JENGA GUEST HOUSE DODOMA.
Kamnunulie Kiwanja eneo la Mjini pale Dodoma Mil 25. Anza ujenzi wa Gesti ya vyumba 10 ambayo utatumia takribani Milioni 60. Baada ya happo ni kukusanya noti kwa kwenda mbele kwa Wabunge na Serikali kwa ujumla baada ya wimbi la kuhamia Dodoma kushika kasi. Nakuhakikishia Guest Dodoma hailali tupu hata iwejeeee! Ukitaka uzoefu zaidi usissite kuniPm ni bure kabisaaaa mkuu. Hongereni