Mradi gani wa kiuchumi unaweza kuanzisha kwa kutumia fedha za mafao kiasi cha Tshs 90,000,000/-?

Mkuuu miradi inayohusu Ujenzi wa Majengo haijawahi kumliza mtu kama umenunua kiwanja sahihi.
JENGA GUEST HOUSE DODOMA.
Kamnunulie Kiwanja eneo la Mjini pale Dodoma Mil 25. Anza ujenzi wa Gesti ya vyumba 10 ambayo utatumia takribani Milioni 60. Baada ya happo ni kukusanya noti kwa kwenda mbele kwa Wabunge na Serikali kwa ujumla baada ya wimbi la kuhamia Dodoma kushika kasi. Nakuhakikishia Guest Dodoma hailali tupu hata iwejeeee! Ukitaka uzoefu zaidi usissite kuniPm ni bure kabisaaaa mkuu. Hongereni
 
Kama hajawahi kufanya boashara yeyote ile, risk ya kuanza na 90m ni kubwa mno. Ni vizuri aanza na mradi utakaotumia mpaka mil 45.
Hakika kama hajawahi kufanya biashara, ni vyema kajenga jengo la bishara, weka fremu kadhaa, anahakika kila mwezi atapata chochote kitu

Au ajenge nyumba simple ya kupangisha maeneo ya mji kidogo, Hakika hatokosa fedha ya kula
 
Hakuna mstaaf aliyewahi kutajirika kwa pension.
Mwambie ale kidogo kidogo. Nyingine awagawie.
 
Mwambie aweke hio hela NMB awe anapokea laki 7.5 kila mwezi. Its a risk free business kuliko ku risk kama hajawahi fanya kabisa biashara yeyote!
 
Kama mtu afahamu maana ya kuwekeza pesa na kupata pesa kwa muda msimpe ushauri huyu ndugu, maana fursa hazina formula zinataka kupambana.... Sasa nasikia mtu anamwambia eti ajenge guest house mjini kwa milioni 60
 
Kama mtu afahamu maana ya kuwekeza pesa na kupata pesa kwa muda msimpe ushauri huyu ndugu, maana fursa hazina formula zinataka kupambana.... Sasa nasikia mtu anamwambia eti ajenge guest house mjini kwa milioni 60
Tena ya vyumba kumi mjini.
 
Mkuu mbona mahesabu yanagoma kichwani mwangu,Dodoma mjini unaweza ukajenga gesti ya vyumba kumi yenye hadhi ya kulala waheshimiwa uchwara wetu kwa milioni sitini.
 
Respect

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hilo nalo neno japo watoto nao wafaidi matunda ya mama kidogo

Namshukuru mama yetu

Alitugawia 5M each tupo 3

Na 1M each ya kwenda kula Bata Ngorongoro.


Yeye hajataka kupata tabu na Biashara kajiwekea fixed akaunti crdb wakati huo ilikuwa Ni asilimia 13 kwa mwezi

So anajipatia laki tano 30 kwa mwezi bila kukimbizana na mtu. Mkataba wake Ni wa miaka 3.

Ila anasema wameshusha riba Ni 9 Sasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama anasimamia mwenyewe basi asifanye miradi inayohitaji sana uangalizi, kwa mtu aliyestaafu na hakuzoea changamoto za biashara au kilimo si vema kuanza kipindi kama hiki...
Kwa maoni yangu naona atafute eneo zuri kwa ajili ya kujenga real estate ndogo ndogo, mfano vyumba viwili viwili unaweza kupata kuanzia 150k-200k per month si haba na haina longolongo,
Pia angepata stationary, kwa hapa apate dada mmoja tuu na yeye mwenyewe, hivyo atakua anaamka kila siku asubuhi kama kipindi yupo kazini, kwa mtu ambaye alizoea kuamka kila asbh kuwahi kazini si vema kukaa tuu,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mshauri afuge nguruwe wa biashara

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu niwie radhi kwa kuendeleza 'debate' kibishani.

Nilichokueleza nina uhakika nacho.

Ninachokuomba 'update' kumbukumbu yako kwa mstaafu mwaminifu juu ya kupata ukweli namna ambavyo wastaafu wanalipwa sasa hivi.

Tena muulize hivi...'eti pensheni za wastaafu zinaingia tarehe ngapi kila mwezi?'...

Hapa naongelea wastaafu wanaolipwa na hazina.

Ni kila tarehe 28 ya kila mwezi na haijawahi kupitiliza katika kipindi cha awamu ya utawala huu na kwenye sikukuu kubwa za kitaifa wanawahishiwa sana.

Na huyo mama anayeelezwa kwenye mada hii, kama alilipwa mkupuo 90m, uhakika wa kulipwa lk5 kila mwezi ni sahihi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani hapati penshion ya kila mwezi??,mfano mama yeye kila mwezi anapewa tshs 500,000
Laki Tano kwa mwezi,Mbona ni nyingi sana,iyo hela aiweke fixed deposit imzalishie aiache kama mwaka mwaka mmoja bila kuigusa ili akili iweze kutulia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…