Mradi gani wa kiuchumi unaweza kuanzisha kwa kutumia fedha za mafao kiasi cha Tshs 90,000,000/-?

Nina mzee wangu ambae kalitumikia jeshj la magereza kwa miaka 34 kastaafu 2015 akiwa na cheo kikubwa tu, huu utaratibu mpya uliokuja wakuwalipa kila mwezi sio wakweli na tarehe uliyoitaja si ya kweli anapokeaga huo mshahara Bank ya posta nasema hivi nikiwa na ushahidi.
.
Na kuna baadhi ya waliokuwa wafanyakazi wenzangu waliostaafu hawalipwi hivo
 
Kwani wakishusha na yeye faida yake ya 13% kwa mwaka itashuka wakati kulingana na mkataba wake yeye alioingia na benki ni kuweka fedha kwa miaka mitatu na faida ikiwa ni 13% kwa mwaka? Hapo sasa si itakuwa kwenda kinyume na mkataba?
 
Wanalipwa kila mwezi ni shahidi wa hilo kwa bibi yangu
 
Maziwa yanalipa hapa nilipo ninakwenda kununua maziwa kwa mfugaji anauza 2400 uko vyema
 
There something wrong with lump sum money(wengi huita pensheni) haiwezekani kila mstaafu lazima afeli
 
Ulipotaja "bank ya posta" tu ndiyo hapo umenifungua!
Mwanzo nilijiuliza sana, mara unataja "check za wastaafu"
Sasa hivi mkuu utaratibu wa check haupo na hao posta ni mumiani wakubwa.

Wanawatongoza wastaafu na kuwapatia mikopo yenye masharti ya kinyonyaji.

Na masharti ya kupatiwa hiyo mikopo, mstaafu ni lazima mwenyewe akiri kwa maandishi kuwa pensheni yake kupitia huko.

Wastaafu wengi si wakweli hasa wakiona "wamepigwa", mfuatilie huyo mzee wako utaupata ukweli wa ninayokueleza.

Kawaida askari magereza mishahara yao huchukulia Nmb ama Crdb.

Anapostaafu hakuna tena mambo ya check, utaratibu huo sikatai ulikuwepo zamani na uliwasumbua sana wastaafu na umekwisha kufutwa.

Sasa hivi pensheni kuanzia hicho kiinua mgongo cha mkupuo na vikokotoo vya kila mwezi, hulipwa 'direct' kupitia kwenye account zao za mishahara na ni kila mwezi.

Ukizidi kubisha mkuu itafikia hatua tuwekeane 'dau' la kutafuta mshindi ili mwisho wa siku ubishi huu tuumalize kwa pesa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni vyema tukawekeana dau mkuu, ili tuumalize mjadala mimi napatikana kwa makonda
 
Kwa umri wake atafute kiwanja ajenge nyumba za kupanga kwa mfano chumba na sebure na choo ndani anaweza jenga hata kumi biashara hiyo haina stress kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mama yangu alistaafu, kiinua mgongo akatumia kujenga nyumba za kupangisha 3. Nyumba ni 2 bedrooms kitchen na sebule. Bahati kiwanja alkuwa nacho tayari na eneo ni zuri karibu na barabara. Hela iliyobaki akanunua gari ya kutembelea, nyingine akaanzisha mradi was kuku wa mayai (alikuwa na uzoefu) nyumba anapangishsha 300,000 kwa mwezi, na zinagombaniwa hakosi wapangaji.
 
Kuna kitu cha kujifunza hapa,wekeza na fanya biashara ukiwa na nguvu zako;fedha za kiinua mgongo ni kwa ajili ya kuukarabati mwili kutokana na magonjwa ya uzeeni.
 
Mkuu natumaini mama yetu alishapata mafao husika pia alishawekeza sehemu ya pesa ya mafao katika miradi ya kuingiza pesa, ingependeza ukarudisha mrejesho namna mradi alioufungua ulivyo hivi sasa ili wengine tupate funzo kupitia uzoefu wenu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…