Mradi Ng'ombe wa Asili

BARA BARA YA 5

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2009
Posts
1,174
Reaction score
835
Wakuu nimeamua kuchukua uamuzi wa kufuga ng'ombe wa asili na kuachana na hawa wa kisasa.
Nitaenda minada ta bara ninunue mitamba kama 50 yenye mimba/au iko tayari kupandwa kwa Sh 250,000 kila mmoja.

Baada ya mwaka nataraji kila mmoja azae na nianze kupata maziwa angalau kwa ng'ombe 30 x lita 2 = 60 litres.

Kwa hapa nilipo lita shs 1,200 hivyo tapata 72,000 kila siku.
Kama nitatengeneza mtindi na yoghurt nitapata hadi laki 1.5 kwa siku.

Kwa mwezi nitapata net ya kama 1.8m hivyo mradi utarejesha fesha ndani ya miaka 2.
Pia tauza mbolea na nyama mwaka wa 3 wa mradi na gharama za uendeshaji kama pumba nk zitapungua.
Utafiiti wangu umehitosheleza na sasa naingia kazini.
 
Ng'ombe kutoa Lita 2 Ni ufala na biashara kichaa.

Kaka kwanza hngra unaplan nzur Sana tatzo hapa utakatishwa tamaa na waswahil wa mijin! Cha kukuongezea hapo weka pia madume nunua waliokonda Ila wamechangamka ukiwafkisha unawachoma sindano y magonjwa meng nununua wa 230, 250, mwez wa 12 huwa Bei iko chin Kisha wakipendeza ita mnunuz pga zako super profit kisha Leta mrejesho!
 
Mim nlinunua 20 last year natarj kuuza mwez wa saba baada y hapo nahamisha mrad songea vijjin nishike por la Bei nafuu niingize mifugo weng sana
 
Kwanza kwa hiyo bei 250,000.00 kwa Mtamba sina hakika nayo HEBU FANYA RESEARCH ZAIDI isijekuwa bei ya mbuzi [pia fanya utafiti kuna ng'ombe wa kisukuma wa pembe fupi halafu kuna ankole yupi bora?]
Kununua Ankole mitamba sio mchezo,nabado inategemea yuko wapi sababu Ankole huwezi waleta hii mikoa kamekame
 
Mawazo yako nimazuri yafanyie kazi
 
Hongera sana - wewe ni mjasiriamali mzuri. Labda nikushauri kidogo kwamba hujasema kuhusu Mtaji ulionao (Overhead costs) na naona kama umekuwa mno too ambitious na kuamini kwamba kila kitu ni ceteris paribus .kwa mfano Mnadani sio rahisi kupata mtamba mwenye mimba; Bei ya ng'ombe 250,000/= huyo ni ndama aliyechoka na sio mtamba Kwa mfano bei ya mtamba Kiteto minadani kwa tarehe 15/04/2022 ilikuwa laki tatu hadi laki tatu na nusu (i.e. Tzs 300.000/= - 350,000/=) halafu ng'ombe wa kienyeji hutoa 1.2 -1.5 Lts za maziwa kwa siku (ni wachache sana hufikia 2.0 - 2.5 ltrs kwa siku). Hujaweka Risks and Uncertainties e.g. Magonjwa, Kukosekana malisho au Uhaba wa malisho, vifo vya ndama n.k. n.k.
Nakushauri wasiliana na Mtaalam wa mifugo wa Ugani (Livestock extension officer) aliye karibu na ww ili kuweka vizuri Mradi wako. Ni hayo tu. 🙏
 
Sahihi kabisa though kufuga ng'ombe wa kienyeji kwa project ya maziwa uwezi kutoka kirahisi awali ya yote kumbuka ng'ombe atazalisha lita mbili ambazo pia ndama anategemea kunyonya hapo hapo na ng'ombe wa kienyeji wanachukua mda mrefu kua matured hivo project itachukua mda mrefu kumpa faida issue za changamoto ya malisho pia utapapambanazo vipi kimsingi hapo mfugaji atafaidikiza kwenye issue ya disease resistant lakini kiuhalisia sio mradi wenye tija.
Ushauri wangu achukue ng'ombe wa maziwa tu ni heri kua na ng'ombe mmoja anaekupa lita 20 au 15 maziwa kuliko kua na ng'ombe 10 wanakupa same amount maana hao kumi watahitaji nguvu kazi kubwa chakula cha kutosha space n.k
 
Kwanza kwa hiyo bei 250,000.00 kwa Mtamba sina hakika nayo HEBU FANYA RESEARCH ZAIDI isijekuwa bei ya mbuzi [pia fanya utafiti kuna ng'ombe wa kisukuma wa pembe fupi halafu kuna ankole yupi bora?]
Niamnini mkuu....mimi pia ni mdau wa minadani na uzoefu ninao
 
Asante Mkuu.. hii pia itauwa fursa nzuri na ninaifikiria
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…