Mradi Ng'ombe wa Asili

Utafiti wangu unaendelea ndigu zangu,takwimu nilizopata so far ni kama ifuatavyo:
1.Msimu huu kuanzia /Desemba/Januari ndio ninunue ng'ombe,wananchi watakuwa hoi kwani hadi sasa debe la mahindi huko ni elfu 20.
2.Pia nimeshauriwa badala ya kununua majike,ni chukue hata madume yaliyokonda,nikileta hapa Pwani ndani ya miezi 3 yatabafilika na nikiuza nanunua majike yenye mimba.

3.Naendelea kumobilize fund.

Asante
 
Huo utafiti uliufanyia mkoa gani?

#MaendeleoHayanaChama
 
Ni bora nimekutana na huu uzi maana nilikuwa kwenye mpango wa kuanza unenepeshaji wa ng'ombe wa asili.
 
Kununua Ankole mitamba sio mchezo,nabado inategemea yuko wapi sababu Ankole huwezi waleta hii mikoa kamekame
Ankole siyo ng'ombe wazuri kwa maziwa na gharama za kuwatunza ni kubwa sana kwa biashara ya kukuza na kuuza wako vizuri sokoni.

Wanachangamoto nyingi sana ambazo usipowavumilia unaweza kuacha kufuga.
1. Hawahimili magonjwa hata kupe Kumi tu wanaweza wakammaliza damu na akafa.

2. Wanahitaji walisho ya kutosha sana kwa mwaka mzima kwa maana hiyo ukilegea wanakonda na kufa.

3. Jike hawana maziwa mengi ukilinganisha na wengine.

4. Wanachukua interval kubwa sana kuzaa anaweza kuonyesha hata miaka miwili.

5. Wanapendelea malisho ya kwenye maji maji lakini wakati huo huo wanapata magonjwa ya kwato mara kwa mara.

6. Wakati wakiwa wachanga inabidi utumie dawa nyingi sana kuwahudumia ili wasidumae na kukua kwa haraka.

7. Kama una bucha yako hata nyama yake ni kamba tupu na mafuta hakuna utakimbiwa na wateja.

NB ila kwa sokoni ukiwakuza vizuri madume yanauzwa hadi million mbili plus.
 
Ni wazo zuri sana ila jipange tu maana ufugaji sasa hivi malisho mtihani.
 
Kwanza kwa hiyo bei 250,000.00 kwa Mtamba sina hakika nayo HEBU FANYA RESEARCH ZAIDI isijekuwa bei ya mbuzi [pia fanya utafiti kuna ng'ombe wa kisukuma wa pembe fupi halafu kuna ankole yupi bora?]
Atleast aweke 350000 itawezekana kupata mitamba mizuri.
 
Sio kwamb Hana akili, sema tumshaur afuge nkole idea yake ni nzur
Ankole na kienyeji hawana tofauti sana kwenye maziwa

Na wingi wa maziwa unategemea factors nyingi kwa ng'ombe siyo breed tu.

Yawezekana ameangalia costs za ngombe wa kisasa akaona heri wa kienyeji.
 
Mwenzenu nafikiria kufunga kondoo Tu lakini kunenepesha ng'ombe NI kama kunanivutia. Wazoefu twambie kondoo Vs kunenepesha ng'ombe?
Inategemea na sehemu ulipo kama umeona soko la kondoo ni kubwa ni mradi poa tu kwanza kondoo wana gharama ndogo na hawashambuliwi magonjwa hovyo hovyo.

Kama uko sehemu kame zenye vichaka vidogo na nyasi fupi mbuzi na kondoo ni miradi bora zaidi kuliko ngombe soko la mbuzi ni zuri kuliko kawaida.

Kunenepesha ngombe ni mradi mzuri pia lakini uwe na chimbo la kuwapata hao wenye bei nafuu, uzingatie pia eneo unalowanenepeshea wanakula chakula cha kununuliwa tu au na nyasi asilia ?
 
Vipi kwa maeneo ya Tunduru ?
 
Kati ya chakula cha kununuliwa na nyasi asilia kipi ni kizuri?
 
Hii huwaje Mzee naona hii Mimi itanifaa sitaki mambo mengi
Unanunua ng'ombe waliokondakonda, unawapiga vitamins, dawa za minyoo na chanjo mbalimbali.
Unawalisha msosi maalum wa kunenepesha (nyasi na chakula mchanganyiko). Baada ya miezi michache wananenepa unawauza. Unaweza kununua ng'ombe aliyekonda kwa laki 4 ukaja kumuuza laki 7.
Ila ni muhimu kuwa na Shamba lako lenye nyasi nzuri zinazopendekezwa.
Uwe na josho, na huduma nyingine.
 
Mh, kw.mfano tayari niemununua ng'ombe wa asili tayari na chakula chao ninategemea niwe nawapeleka uwandani wanajilisha na jioni wanarudishwa bandani, je napaswa kufanya nini ili niweze kuwanenepesha? Naomba msaada wa kimawazo na kitaalamu pia na uzoefu kama unao naomba kujuzwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…