BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 525
- 1,257
Mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Kabingo-Kibondo-Kasulu-Manyovu wenye urefu wa Kilometa 260.6 unaoanzia Mpakani mwa Tanzania na Burundi upo katika hatua mbalimbali za ujenzi.
Akielezea maendeleo ya mradi huo akianzia na eneo la Mpakani, Mhandisi Ngoko Mirumbe ambaye ni Kaimu Meneja wa TANROADS Kigoma anasema:
“Mpakani kunatarajiwa kuwa na ‘one border stop project’ ambapo itajengwa kituo kimoja cha Burundi na upande mwingine ni wa Tanzania na kunatarajiwa kuwa na huduma zote muhimu, Mkandarasi anayehusika na eneo hili ni kampuni kutoka Uganda.”
Kuhusu kinachoendelea kwa sasa katika ujenzi wa kituo hicho ni ‘designing’ ambayo ipo katika hatua za mwishomwisho kabla ya kuanza kwa ujenzi rasmi.
Ameeleza kuwa baadhi ya faida ya mradi wa kituo hicho ni kusaidia kupunguza usumbufu kwa kuwa hali ilivyo watu wanaovuka Mpakani wanalazimika kufanyiwa ukaguzi pande zote mbili, mradi ukikamilika ukaguzi utakuwa unafanyika wa upande mmoja.
Alipotakiwa kuelezea kuhusu gharama ya ujenzi huo amebainisha kwa kuwa bado mradi upo katika hatua ya designing, gharama halisi bado hazijajulikana.
Akielezea kuhusu mradi wote anaeleza umegawanyika katika hatua nne, kwanza ni Manyovu - Kasulu (Kilometa 68.25), pili ni Kidyama-Mvugwe (Kilometa 70.5), tatu ni Mvugwe – Nduta (Kilometa 59) na nne ni Nduta-Kabingo (Kilometa 62.25).