Mradi wa Bagamoyo ulitakiwa uanze kabla ya Bwawa la Nyerere, Rais Samia umetuheshimisha

Mradi wa Bagamoyo ulitakiwa uanze kabla ya Bwawa la Nyerere, Rais Samia umetuheshimisha

Jamani mimi sijaelewa, ina maana mradi wa bwawa la kufua umeme unaachwa katikati? Au vyote vitafanyika kwa pamoja?
Kumbuka watumishi wameishi kwa taabu ya mishahara kwa 5yrs ili mradi wa umeme uendelee, hivyo kuuuacha ni sawa na kufuja hela za watumishi
 
Katika akili tu ya kawaida Nchi kuwa na project ya kuzalisha umeme wa bei nafuu na kutengeneza Lango la kupitisha mizigo kutoka nchi zingne hv ni lipi linatakiwa kuanza??hv ni lipi kati la hayo likiwepo kwamza kitaleta uwakika wa kuzalishwa viwanda na ajira..hv ni lipi katika hilo litaleta ahueni kwa mwananchi mmoja mmoja??
 
Katika vitu ambavyo sielewi ni ujenzi wa bandari mpya wakati hizi za zamani zinatushinda kuziendeleza.

Nitasimama na Marehemu Magufuli kwenye suala hili.
 
Natumaini hayo mazungumzo kwa upande wa serikali yetu yatajumuisha watu makini na wenye uelewa mpana wa uchumi wa kisasa. Yale yaliyosemwa na hayati na yapewe kipaumbele kwenye mijadala.

Tuliweza kwenye madini mpaka imeundwa hiyo kampuni ya Twiga natumaini umakini huo huo utakuwepo tutakapokuwa tukiongea na hao wawekezaji.
Kama unampenda sana mwendazake mfuate huko chato, wakati wake umeshapita
 
Mkuu sa iv watu wote waliokuwa adui wa serikal ni marafik wa serikal subr tu uone huko mbele
Hawa watu ndio wanapiga kelele shule hazina madawati hospital hazina dawa.

Halafu tunataka kujiingiza kwenye miradi isiyo ya maana...mtu anadiriki kusema eti umeme sio muhimu kama bandari si atakuwa mwehu kabisa huyo.
 
Wale mnaoongea juu ya mkataba 2a Bagamoyo nini kinazuia kuuweka huo mkataba hapa ili kila mmoja ausome la sivyo kama vile JPM alisema mkataba ulikuwa na shida lkn HAKUTUONYESHA sasa na wewe UWEKE.
La sivyo bado mwingine atakuja na kusema ulikuwa wa hovyo
 
Ombi Kwa mama Samia sio kila alichokikataa Magufuli yeye akirudishe na kukikubali, asijisahau Kwamba kazungukwa na wapigaji na mafisadi Papa wenye ngozi ya kondoo
 
Hizi nadharia zote zinazoibuka kuhusu huu mradi zinazimwa na maneno mawili tu; UMEOUNA MKATABA, na zaidi haya maneno mawili yanawafaa zaidi wote wanaotaka haya mazungumzo yaendelezwe.
Unafikiri mkataba utauona hadharani huo ni mkataba wa kibiashara siyo wa kuuziana maandazi nazani mleta mada kadadavua kwa point za msingi.
 
Mataga ni kina nani? Utabaki na hilo jina mataga huku umasikini unakutafuna na wenzio wanapiga hela!

Usifikiri unapotetea ujinga unamkomoa Magufuli na familia yake hapana! Wanakomoka familia na ukoo wako huko vijijini
Kwani ukoo wako unaishi nchi nyingine zaid ya hii?
 
Back
Top Bottom