Mradi wa Bandari Bagamoyo bila uwazi wa ubovu wa mkataba, ni usaliti wa Bandari zilizopo

Sina vyombo vya dola nyuma yangu kunisaidia kutangazwa mshindi, japo nina uhakika kura nitapata toka kwa wananchi.
Mkuu unaowaona walianza hivyohivyo usiogope
 
Kaa kwa kutulia, na uhakikishe maua hapo kwenye kaburi la dhalimu yananyeshewa. Tulipokuwa tunahoji mikataba ikae wazi, mlikuwa kimya maana mlikuwa kwenye chain ya upigaji, sasa hivi mmeoshwa mikono na mafuta taa mnalialia hapa.
Umekaa kizamani sana wewe, Hata hivyo, ninachoamini hata wewe ni mtu duni sana na dhaifu mno Mbele ya kifo, kwa kuwa hata huwezi amini iwapo kejeli zako hizi zikawa ni za mwisho nawe ukazikwa kama itakavyokuwa kwa kila mwenye mwili, Hekimika kijana
 
Hapana kwanza tuimarishe bandari ya DSM, tuzibe myanya yote ya rushwa na upotevu wa mapato ya serikali.
Ripoti ya CAG 2020 ilibainisha changamoto kibao TPA na kasoro hizo zimekuwa zikijirudia amabazo zimepelekea kutokea ubadhirifu wa kutisha ktk bandari ya DSM, sasa leo hii bado hatujadhibiti bandari ya DSM wanataka kutushawiishi kujenga bandari ya B.moyo!!! ili wapigaji na wabadhirifu wale vizuri!!! Hapana!
kwanza tunataka matokeo mazuri ktk bandari ya DSM

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wachina wanatisha sana. Kama huamini nenda Zambia. Mradi ni wa muhimu lakini umilikiwe na serikali hata kwa kukopa ila si kwa ubia. Wenzetu ni wajanja wa mikataba ya kumataifa. Tunaweza kuishia kuwa wabeba mizigo ya wachina.
 
Kuna siri gani ambayo inatupa hofu kuhusu huu mradi??
 
Kwa hiyo kujenga Airport Dodoma unauwa airport Dar au? Umeshaambiwa Bandari ya Dar imefika kikomo haina uwezo na wala haitakuwa na uwezo wa kupokea meli kubwa za kisasa ni lazima bandari mpya ijengwe kuendana na mahitaji ya biashara duniani. Bandari ni biashara ya ushindani duniani ndio maana hata Airport hazibaki the same tumejenga Terminal 3 sababu Terminal 2 haina uwezo tena lakini haina maana Terminal 2 umeuliwa inafanya kazi kwa uwezo wake. Kwa ufupi bandari ya Dar imefika kikomo uwezo wake. umeambiwa jana tukifanya mchezo bandari ya Dar itabaki kama kituo cha daladala.
 
Ngoja tuone... Kuna mambo yanafanywa kwa manufaa ya wachache...
 
Umekaa kizamani sana wewe, Hata hivyo, ninachoamini hata wewe ni mtu duni sana na dhaifu mno Mbele ya kifo, kwa kuwa hata huwezi amini iwapo kejeli zako hizi zikawa ni za mwisho nawe ukazikwa kama itakavyokuwa kwa kila mwenye mwili, Hekimika kijana

Mimi hata nikifa poa tu maana sijifanyi mzalendo na mcha Mungu, ila yeye dhalimu sasa.
 
kwa nini tunadhani JPM pamoja na aliyekuwa mgombea Uraisi kupitia Chadema 2015 mh EL wamekuwa waongo kuukataa huu mradi kwamba hauna manufaa yoyote kwa nchi yetu?
Huyo jiwe alikuwa mzandiki, mwongo na mfitini. Kwa miaka 5 tu alitudanganya:-
-ndege zinaleta faida akafanya mpk bongo movie ya gawio
-uchumi unakuwa kwa 7%
-tunajenga miradi ya kimkakati kwa fedha zetu za ndani
..n.k

Kwann umwamini mtu kama huyu?

Kwann tusidhani mzee Kikwete na SSH wako sahihi? Mzee Kikwete hajawahi kudanganya kwa miaka 10.
 
Na wewe 10%
 
Isije kuwa msoga king ana mpush mama hio agenda .

Aisee Kama uwepo wa huo mradi utaathiri bandari zetu Bora wakauacha

Na Kama utakuwepo Basi tuwe na percentage za kutosha kwenye gawio .

Na lazima mipaka iwekwe kwenye operation kujua hii inahudumia wapi na hii wapi
 
Unataka uwazi wa bandari ya Bagamoyo. Mbona huulizi mkataba wa ununuzi was ndege? Bunge halijaidhinisha lakini wanaofahamu ununuzi ni Mwendazake na mpwaye ambaye wakati huo alikuwa Paymaster General!
 
Justification ya kwamba mikataba yote ya siku za nyuma haikuwahi kuwekwa wazi na kwa hiyo hata huu wa bagamoyo tusihoji haina mashiko.

Ni kweli kabisa kwamba mikataba ya siku za nyuma haikuwahi kuwekwa wazi kwa Umma kusoma na kutoa mapendekezo.

Hayo yalikuwa makosa.

Sasa Je makosa yaendelee kufanyika au yarekebishwe kwa kuanza kuweka mikataba wazi na kusomwa na wananchi na kutoa mapendekezo?

Off course watasema labda ilikuwa inapelekwa bungeni kwa wawakilishi wa wananchi, sawa lakini ufanisi wa bunge ukoje?

Yani historia ikoje? Uzoefu Je?

Je Kuna mkataba wowote ambao uliwahi kataliwa na bunge kwa sababu moja ama nyingine?

Ni upi huo ? ai ni ipi hiyo?

Au Ndiyo kusema bunge la rubber stamp?

Lile la “ ndiyooooooooo” kwa kila kitu?

Tutafakali zaidi.
 
Kwani bakwata wanasemaje kuhusu Hilo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…