Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
KOMREDI KAWAIDA - MRADI WA B.B.T USIPOFANYA VIZURI TUTAWALAUMU WIZARA YA KILIMO
Kilombero. Wakati Wizara ya Kilimo ikitekeleza mradi wa Jenga Kesho Iliyo Bora (BBT), Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM (UVCCM), Mohammed Kawaida amesema chochote kitakachokwama lawama ataitupia wizara hiyo.
Kauli yake hiyo, inatokana na kile alichoeleza kuwa, Rais Samia Suluhu Hassan ametoa fedha nyingi kugharimia sekta ya kilimo na jukumu la wizara hiyo ni kutekeleza.
Kawaida ametoa kauli hiyo leo, Jumatano ya Aprili 19, 2023 akihotubia vijana baada ya kutembelea mradi wa BBT Kituo cha Chuo cha Taifa cha Sukari wilayani Kilombero Mkoa wa Morogoro.
"Wizara ya Kilimo imepewa imani kubwa kwa ajenda ya 2030, mradi wa BBT na mambo mengine lukuki," amesema.
Kwa sababu ya imani iliyopewa wizara hiyo, amesema chochote kikikwama UVCCM na vijana wengine watailaumu Wizara ya Kilimo kwa kushindwa kutekeleza.
"Chochote kikikwama UVCCM na vijana wengine Tanzania tutakayemlaumu ni Wizara ya Kilimo na sio Rais Samia, kwa sababu yeye ametoa fedha nyingi katika Wizara hiyo," ameeleza.
Kauli hiyo ya Kawaida ni kama inapigia msumari wa kile kilichowahi kuelezwa na Rais Samia kuhusu mradi wa BBT, kwamba hata kusikia umekwama.
"Sitaki kusikia tumeshindwa, hakuna kushindwa lazima twende na lazima tufanikiwe,” alisema Rais Samia Machi 20, 2023 wakati wa uzinduzi wa mradi huo.
Onyo lake hilo liliambatana na onyo kwa Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe alipomwambia: “Nataka kuwaambia nimekusudia kwenye hili na sitavumilia Bashe na wenzio pale nitakapotoa fedha za wavuja jasho wa Tanzania ziende kwenye matumizi ya kilimo zikazalishe na fedha ile ikachezewe, sitavumilia,” alisema.