Mradi wa elimu mbadala kwa wanafunzi waliokatisha masomo SEQUIP - AEP haujafanya malipo kwa muda wa miezi mitatu mfululizo bila taarifa yoyote

Mradi wa elimu mbadala kwa wanafunzi waliokatisha masomo SEQUIP - AEP haujafanya malipo kwa muda wa miezi mitatu mfululizo bila taarifa yoyote

A

Anonymous

Guest
Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (IAE) inatekeleza mradi wa kuwarudisha watoto wa kike waliokatisha masomo kupata elimu kwa njia mbadala (SEQUIP) chini ya programu ya Altenative Education Pathway (AEP). Mradi huu unafadhiliwa na Benki Kuu ya Dunia na unatekelezwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI.

Mpaka sasa wawezeshaji katika mradi huu (walimu) hawajalipwa posho zao kwa muda wa miezi mitatu tangu mwezi Agosti, 2024. (Yaani malipo ya mwisho yalikuwa ni mwezi wa saba, 2024. Hata hivyo, tangu kuanza kwa mradi huu malipo yamekuwa yakisua sua yakivushwa mpaka mwezi mmoja mbele yaani malipo ya mwezi wa kwanza unalipwa mwezi wa pili mwishoni au watatu kabisa mwanzoni.

Wasimamizi na waratibu wa vituo husika hawatoi taarifa yoyote kuhusu kucheleweshwa kwa malipo hayo huku wakiendelea kusisitiza walimu kufundisha kwa kujitolea huku walimu wakiendelea kufanya hivyo. Je, ipo wapi haki ya mwalimu katika mradi huu? Je, ni sahihi kufanya kazi bila kupewa ujira na bila taarifa yoyote?

Ni tumaini letu kuwa tutapata majibu sahihi kutoka mamlaka husika. Asante.

1.PNG
rais.PNG
 
Mradi wa SEQUIP - AEP unafadhiliwa na Benki ya Dunia na unatekelezwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI. Mradi huu unalenga kuwarudisha watoto wa kike waliokatisha masomo kwa sababu mbalimbali kupitia elimu mbadala (Alternative Education Pathway).

Mpaka sasa umepita muda wa miezi mitatu mfululizo wawezeshaji (walimu) katika mradi huu hawajalipwa stahiki zao bila taarifa yoyote. Malipo yamelipwa kwa mara ya mwisho mwezi Julai, 2024.

Hata hivyo, tangu kuanzishwa kwa mradi huu malipo yamekuwa yakisuasua kwa malipo ya mwezi husika (yaani malipo ya mwezi wa kwanza yamekuwa yakilpwa mwezi wa pili mwishoni au wa tatu mwanzoni) hali inayopelekea walimu kufanya kazi kwa manung'uniko.

Tunaomba mamlaka husika itoe ufafanuzi juu ya malipo kwa watumishi hao kwani mpaka sasa hakuna taarifa yoyote ile.

rais.PNG
 
Hamna kitu washenzi hawa
Unatukana na kazi unaitaka, sasa kati ya wao na wewe nani ni mshenzi... we umeona hulipwi achana nayo uende unakolipwa. .. ile hela yako ikifika muda utalipwa tu. Heshimu watu heshimu kazi.
 
Unatukana na kazi unaitaka, sasa kati ya wao na wewe nani ni mshenzi... we umeona hulipwi achana nayo uende unakolipwa. .. ile hela yako ikifika muda utalipwa tu. Heshimu watu heshimu kazi.
Ila kweli ngoja niidelete kwanza. Asante mwanangu
 
Pesa zime pigwa na mtu mweusi .wala sio muekezaji
 
Back
Top Bottom