A
Anonymous
Guest
Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (IAE) inatekeleza mradi wa kuwarudisha watoto wa kike waliokatisha masomo kupata elimu kwa njia mbadala (SEQUIP) chini ya programu ya Altenative Education Pathway (AEP). Mradi huu unafadhiliwa na Benki Kuu ya Dunia na unatekelezwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI.
Mpaka sasa wawezeshaji katika mradi huu (walimu) hawajalipwa posho zao kwa muda wa miezi mitatu tangu mwezi Agosti, 2024. (Yaani malipo ya mwisho yalikuwa ni mwezi wa saba, 2024. Hata hivyo, tangu kuanza kwa mradi huu malipo yamekuwa yakisua sua yakivushwa mpaka mwezi mmoja mbele yaani malipo ya mwezi wa kwanza unalipwa mwezi wa pili mwishoni au watatu kabisa mwanzoni.
Wasimamizi na waratibu wa vituo husika hawatoi taarifa yoyote kuhusu kucheleweshwa kwa malipo hayo huku wakiendelea kusisitiza walimu kufundisha kwa kujitolea huku walimu wakiendelea kufanya hivyo. Je, ipo wapi haki ya mwalimu katika mradi huu? Je, ni sahihi kufanya kazi bila kupewa ujira na bila taarifa yoyote?
Ni tumaini letu kuwa tutapata majibu sahihi kutoka mamlaka husika. Asante.