Mradi wa Kufua Umeme Rufiji (MW 2115) uchimbaji kina cha lango la kuingilia maji kwenye mitambo wakamilika

Mradi wa Kufua Umeme Rufiji (MW 2115) uchimbaji kina cha lango la kuingilia maji kwenye mitambo wakamilika

mkiluvya

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2019
Posts
809
Reaction score
729
1591253904131.png

Ujenzi wa eneo la lango (Water Intake) la kuingilia maji kwenda kwenye mitambo ya kufua umeme katika Mradi wa Julius Nyerere (Mw 2115) unatarajiwa kukamilika Februari 2022.

Mhandisi Dismas Mbote, Mhandisi wa ujenzi njia za maji pamoja na Bwawa kwenye Mradi wa Julius Nyerere amesema utekelezaji wa njia hiyo ulianza Mwezi Oktoba 2019. Aliongeza kuwa kazi ya uchimbaji wa lango imekamilika kwa kuchimbwa kina cha mita 53 ambapo hivi sasa kazi inayoendelea ni uondoaji wa kifusi na uchimbaji wa mahandaki matatu yatakayotumika kupitisha maji.

“Vifusi ambavyo vinachimbwa katika mradi huu wa Julius Nyerere havitupwi, mawe yanasagwa na kuwa mchanga, kokoto na mawe mbalimbali ambayo hutumika kwenye ujenzi”, alisema Mhandisi Mbote.

Aidha, zitafanyika kazi za kuchoronga miamba pamoja na kuimarisha kuta kwa zege. Maji yatakayofua umeme kabla ya kwenda kwenye mitambo ya kufua umeme yataingia kwanza kwenye lango. Sambamba na hayo imeletwa mashine ya kuchoronga miamba ambayo ni ya kwanza kwa Tanzania na inayotarajiwa kuongeza kasi katika uchimbaji wa mahandaki ya kupeleka maji kwenye mitambo. Handaki la kwanza litakuwa na urefu wa mita 350, la pili mita 410 na la tano mita 570 hadi kwenye mitambo ya kufua umeme.

PIA SOMA

TUHUMA ZA UFISADI NA HUJUMA

HISTORIA

Muwakumbuke na Wafanyakazi sasa. Yale madaraja yao yapande kwa wakati. Miaka zaidi ya 5 ya kuwaumiza kwa kisingizio cha kujenga hiyo miradi, inatosha. Na wenyewe wangependa waishi maisha bora kama wengine.
 
[emoji848][emoji848][emoji848][emoji144][emoji144][emoji144][emoji144][emoji124][emoji124][emoji124][emoji124]

Jr[emoji769]
 
Hivi huu mradi ukikamilika kutakuwa na mambo ya power rationing tena?

Mpaka sasa kuna mafanikio makubwa ukilinganisha na awamu 2 (miongo miwili) zilizopita. Na huu mradi ukikamilika, bila shaka hilo tatizo la umeme na mgao usio na kichwa wala miguu utaisha kabisa! Ingawa bado kuna umuhimu wa kutafuta vyanzo vingi zaidi ili kuifikia Tanzania ya kweli ya Viwanda ifikapo hiyo 2025.

All in all, kwenye ujenzi wa Mamiradi Makubwa Makubwa, awamu hii ya 5 imejitahidi sana! Ila ukija kwenye maisha ya Watanzania walio wengi, hakika maisha yamekuwa ni magumu sana kutokana na kukosekana kwa hela mtaani. Kuna umuhimu wa kuulegeza uchumi ili ulete ahueni kwa mwananchi mmoja mmoja. Vyuma havilainiki kabisa.
 
Nimekupata vizuri kaka.
Ila mi naona nchi yetu ni changa bado kiuchumi kuweza kubalance eqn sehemu zote mbili; kuna upande utaumia tu.. Ila nikuhakikishie ni suala la muda tu.
 
Utafeli huo kama treni ya moshi no suala LA muda tuuu
 
Uchawi sio mpaka uloge! Huu nao ni uchawi.
kaka Leo ni 4/6/2020/ mark my words nakupa miaka mitatu tuombe uhai hakuna pesa kujenga hiyo kitu ma wazungu wameshakataa kitoa pesa tatizo tatizo mnasoma Uhuru na mzalendo !!!??.
 
kaka Leo ni 4/6/2020/ mark my words nakupa miaka mitatu tuombe uhai hakuna pesa kujenga hiyo kitu ma wazungu wameshakataa kitoa pesa tatizo tatizo mnasoma Uhuru na mzalendo !!!??.
Hakuna siku Chadema waliwahi kuiombea mafaniko nchi hii.Siku zote maombi yenu ni kushindwa tu.Badala ya kuomba mradi huu muhimu kwa maendeleo na ustawi wa nchi ufanikiwe na uishe wewe unaomba usiishe. Nina shaka na kiwango chako cha uzalendo. Au dishi litakuwa kimeyumba....
 
Ccm huunga mkono kila kitu ndio maana nchi ni shithole kila kitu ni hovyo kwakuwa wapumbavu uunganga mkono kila kitu ili kuwafurahisha watawala
Angalia elimu
Angalia suala LA ajira
Angalia mini ilivyo ovyo
Hizo Hosp mnazo sifia ni gate of heaven hakuna kitu
Etc since 1960's yet ..........https://jamii.app/JFUserGuide you
 
Ccm huunga mkono kila kitu ndio maana nchi ni shithole kila kitu ni hovyo kwakuwa wapumbavu uunganga mkono kila kitu ili kuwafurahisha watawala
Angalia elimu
Angalia suala LA ajira
Angalia mini ilivyo ovyo
Hizo Hosp mnazo sifia ni gate of heaven hakuna kitu
Etc since 1960's yet ..........**** you
[/QUOTE
Awali nilidhani ninajadiliana na mtu timamu...Kumbe!
 
Aiseee do you think you are intelligent enough than me???
 
Kazi nzuri sana ila Sasa yasijekuwa Yale ya gesi ya mtwara tuliambiwa gesi ikifika dar itaanza kuzalisha umeme utashuka bei ukabaki stori Sasa kwa uvumilivu wa watanzania tunaomba kweli likikamilika umeme ushuke bei angalao watu wafurahie machungu waliyopitia. Watu tupikie umeme tuachane na mkaa unaondelea kuleta athari kwenye mazingira
 
Back
Top Bottom