Iselamagazi
JF-Expert Member
- Sep 26, 2011
- 6,020
- 6,161
Uchumi unalegezwaje mkuu?Mpaka sasa kuna mafanikio makubwa ukilinganisha na awamu 2 (miongo miwili) zilizopita. Na huu mradi ukikamilika, bila shaka hilo tatizo la umeme na mgao usio na kichwa wala miguu utaisha kabisa! Ingawa bado kuna umuhimu wa kutafuta vyanzo vingi zaidi ili kuifikia Tanzania ya kweli ya Viwanda ifikapo hiyo 2025.
All in all, kwenye ujenzi wa Mamiradi Makubwa Makubwa, awamu hii ya 5 imejitahidi sana! Ila ukija kwenye maisha ya Watanzania walio wengi, hakika maisha yamekuwa ni magumu sana kutokana na kukosekana kwa hela mtaani. Kuna umuhimu wa kuulegeza uchumi ili ulete ahueni kwa mwananchi mmoja mmoja. Vyuma havilainiki kabisa.
Ebu tupatie darsa na sisi wengine tufaidike na Uzi wako.