Mradi wa Kufua Umeme Rufiji (MW 2115) uchimbaji kina cha lango la kuingilia maji kwenye mitambo wakamilika

Mradi wa Kufua Umeme Rufiji (MW 2115) uchimbaji kina cha lango la kuingilia maji kwenye mitambo wakamilika

magufuri kaza mwendo tupo nyuma yako, Hii hapo hawajakuta madini kweli
 
Kazi nzuri sana ila Sasa yasijekuwa Yale ya gesi ya mtwara tuliambiwa gesi ikifika dar itaanza kuzalisha umeme utashuka bei ukabaki stori Sasa kwa uvumilivu wa watanzania tunaomba kweli likikamilika umeme ushuke bei angalao watu wafurahie machungu waliyopitia. Watu tupikie umeme tuachane na mkaa unaondelea kuleta athari kwenye mazingira

Kipaumbele Cha umeme wa maji badala ya Gesi... Ni sawa na kuacha kutumia jiko la Gesi na kuanza kutumia jiko la mkaa....
 
Muwakumbuke na Wafanyakazi sasa. Yale madaraja yao yapande kwa wakati. Miaka zaidi ya 5 ya kuwaumiza kwa kisingizio cha kujenga hiyo miradi, inatosha. Na wenyewe wangependa waishi maisha bora kama wengine.
Hata akiongozewa mingine mitano, hatakaa atapandishe mishahara wala madaraja. Labda madaraja ya Kigongo kwa sababu maalum.
 
Muwakumbuke na Wafanyakazi sasa. Yale madaraja yao yapande kwa wakati. Miaka zaidi ya 5 ya kuwaumiza kwa kisingizio cha kujenga hiyo miradi, inatosha. Na wenyewe wangependa waishi maisha bora kama wengine.

Wafanye maamuzi magumu ya kumuacha mwajiri
 
Kipaumbele Cha umeme wa maji badala ya Gesi... Ni sawa na kuacha kutumia jiko la Gesi na kuanza kutumia jiko la mkaa....

Gas pekee haiwezi kuwa ndio njia sahihi ya kuzalisha nishati. Kuna upepo, Jua, makaa ya nawe etc. Hata nuclear ikibidi. Tuache kukariri mambo
 
Gas pekee haiwezi kuwa ndio njia sahihi ya kuzalisha nishati. Kuna upepo, Jua, makaa ya nawe etc. Hata nuclear ikibidi. Tuache kukariri mambo

Sijakataa hiyo njia mbadala wa kuzalisha umeme... Nimewaza tu kwamba teknolojia ya matumizi ya maji ni ya kizamani na matumizi ya Gesi Ni ya kisasa zaidi...
 
Hakuna siku Chadema waliwahi kuiombea mafaniko nchi hii.Siku zote maombi yenu ni kushindwa tu.Badala ya kuomba mradi huu muhimu kwa maendeleo na ustawi wa nchi ufanikiwe na uishe wewe unaomba usiishe. Nina shaka na kiwango chako cha uzalendo. Au dishi litakuwa kimeyumba....
Nyinyi husapot kila kitu mwisho was siku nchi ni shit hole !!!! Chadema hupingwa kwakua huona mbali ?!?? Hivi tren ya moshi IPO!????
 
kaka Leo ni 4/6/2020/ mark my words nakupa miaka mitatu tuombe uhai hakuna pesa kujenga hiyo kitu ma wazungu wameshakataa kitoa pesa tatizo tatizo mnasoma Uhuru na mzalendo !!!??.
Hata watalii kipindi hiki cha Corona mlisema hawaji mwisho wa siku mkaumbuka
 
Mpaka sasa kuna mafanikio makubwa ukilinganisha na awamu 2 (miongo miwili) zilizopita. Na huu mradi ukikamilika, bila shaka hilo tatizo la umeme na mgao usio na kichwa wala miguu utaisha kabisa! Ingawa bado kuna umuhimu wa kutafuta vyanzo vingi zaidi ili kuifikia Tanzania ya kweli ya Viwanda ifikapo hiyo 2025.

All in all, kwenye ujenzi wa Mamiradi Makubwa Makubwa, awamu hii ya 5 imejitahidi sana! Ila ukija kwenye maisha ya Watanzania walio wengi, hakika maisha yamekuwa ni magumu sana kutokana na kukosekana kwa hela mtaani. Kuna umuhimu wa kuulegeza uchumi ili ulete ahueni kwa mwananchi mmoja mmoja. Vyuma havilainiki kabisa.
Nadhani baada ya BOT kushusha riba tarehe 13 may, hela itaongezeka mtaani
 
Back
Top Bottom