Mshombsy
JF-Expert Member
- Mar 15, 2013
- 372
- 180
Unaweza kuwa na hoja Mkuu Mshombsy lakini kumbuka, ukiwepo mfumo bora wa usafiri wa umma utashawishi watu wengi kuutumia badala ya kuendesha magari binafsi kila wanapokwenda kazini na hii itachangia kupunguza foleni zisizo za lazima.
Vilevile, inawezekana foleni isipungue sana hiyo itawaathiri wanaoendesha magari binafsi lakini kwa vile mabasi haya yanakuwa na njia yake maalum hutumia muda mfupi sana kufika katikati ya mji na yatapendelewa na watu wengi wanaokwenda kazini. tumeyaona kwenye treni za Mwakyembe.
Hizo fly-over mnazopendekeza zinasaidia lakini peke yake sio dawa ya foleni mjini, bali ni combination ya yatua mbalimbali ikiwemo kuboresha usafiri wa umma.
Ni kweli uyasemayo mkuu ila kumbuka hiyo inaenda sambamba na ujenzi wa maegesho nje kidogo ya mji, huduma kwa maana ya wingi wa hayo mabasi kuondoa kugombania kuingia.
Wengi wanapenda kupanda daladala lakini kero zake ndo shida. Mabasi yanayo challenge kubwa kwa utamaduni wa mweusi kutojua umuhimu wa mali za umma
Last edited by a moderator:









