Mradi wa maji Butimba umekwama, wafanyakazi wagoma

Nyanswe Nsame

Senior Member
Joined
Jul 9, 2019
Posts
165
Reaction score
181
Mradi wa maji Butimba umekwama, wafanyakazi wagoma

Wafanyakazi 200 katika mradi wa chanzo cha maji Butimba wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza wamegoma kwa kile kinachotajwa wameshindwa kulipwa mishahara yao.

Mradi huo unaojengwa kwa gharama ya zaidi ya shilingi bilioni 60, lakini wafanyakazi ambao wengi wao ni vibarua wanashindwa kulipwa? Rais chukua hatua.

Mradi huu licha ya wafanyakazi kugoma kuna makandokando mengi sana, ikiwemo mkandarasi kuchelewesha kuukamilisha kwa wakati.

Mwaka jana, makamu wa Rais, DK. Philip Mpango alipofanya ziara mkoani Mwanza na kutembelea mradi huo, mkandarasi aliahidi kukabidhi mradi Desemba mwaka jana lakini mpaka sasa mradi ni kama umekwama hata usambazaji wa mabomba haujafanyika.

Mradi huu unajengwa na kampuni ya M/S Sogea Satom na kusimamiwa na Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira.

Mpaka muda, Mkurugenzi wa Mwauwasa Jiji la Mwanza Leonard Msenyere na Katibu wa chama cha wafanyakazi mkoa wa Mwanza amefika kwenye eneo la tukio kuzungumza na mkandarasi wa mradi huo.
 
Nikishasema hakuna waziri wa hovyo kama yule wa maji?

USSR
 
Back
Top Bottom