Mradi wa nyumba za kupanga wa Dr. Hussein Mwinyi Dar

FP,
Kama ni kuhitimisha mjadala, nadhani hilo umelifanya vizuri tu. Mengine yote yatakuwa ni mazungumzo baada ya habari.
 
Mazao ya utandawizi. Mwl Nyerere alisema ubepari ni unyama watu hawakumuelewa jikumbushe tu kwa rejea kitabu cha Chachange(RIP) Makuwadi wa soko huria inatosha kujua tuendako na tusiulizane
 
Tunazikumbuka enzi ambazo Serikali na viongozi wake walikuwa wanawatumikia wananchi na si kufikiria kujinufaisha wao wenyewe. Picha hii (I hope itaonekana vizuri iki kwenye kitabu cha NYERERE Freedom and Socialism/Uhuru na Ujamaa) ni ya mradi wa National Housing ulianzishwa baada ya Uhuru kuwajengea wafanyakazi nyumba za bei nafuu Magomeni na Kinondoni.
 

Attachments

  • National Housing Project.jpg
    334.1 KB · Views: 69


jamani wenzetu mlio nje msiwe mnasikia ya kuambiwa ....jitahidini kila mwaka muwe mnafika nyumbani..sisi wengine tulikuwa hatuamini lakini there are so many opportunities..mimi nimekaa nje lakini siku hizi naona kama mtu anayengangania nje [na hasa wanaosahau nyumbani]..watabaki kulia wivu kila siku..zaidi ya yote maisha ya box yamepitwa na wakati..maisha ya kuwa raia wa daraja la tatu yalilipa enzi zilee za kuzamia meli na kurudi na peugeot,raba mtoni..na kutishia vishtobe..sio saa....mambo yamebadilika sana.....watu wanajitahidi sana kuwekeza....na sio wote wanawekeza kwa pesa haramu.....we should not generalise....

kwa watu walioondoka nyumbani miaka ile ..hawawezi kuamini kuwa mbongo anaweza kumiliki nyumba ...sembuse....ghorofa....lakini mimi binafsi nawajuwa wengi tu ..wanamiliki mali kwa jasho....lao, ni lazima tuondokane na tabia ya kuchukia kila mwenye kajiuwezo...kwa kufikiri ni za ufisadi....sio kila mmoja ana fursa ya kufanya ufisadi!!
 

Phil, ni kweli kujenga nyumba ya Millioni 200 inawezekana kwa mikopo na juhudi kidogo. Na hii ni kama wewe ni mfanya biashara au mfanyakazi wa makampuni ya kigeni na upo nafasi ya juu kidogo.

Kwa mfanya kazi serikalini, bila rushwa au kuwa na kampuni ambayo inapata tenda serikalini kwa kutumia rushwa au cheo chako. HAIWEZEKANI kusave na kuwa na mali za billioni MBILI. Hasa kama una business na unalipia KODI sahihi.

Issue hapa ni mfanyakazi wa serikali binafsi kuwa na uwezo wa kujenga Ghorofa ya 10 Billion TZS. Kama ni kampuni basi hatuna issue ila kibinafsi (as an individual) ni ngumu kaka. Maana collateral security ya benki ni not less than 2.5 billion worth of asset. (cash au properties)

Mie naongelea issue ya uwezo ukiwa mfanyakazi wa serikali ya BONGO. Naomba ukijibu zingatia hilo.
 
kwa nini mtoa mada awe cursed kiasi icho, inaonekana kama double standard, 10billion uyo husein mwinyi kapata wapi? labda tuanzie apo, chenge alisema ana visijisent ya 1billion nchi nzima tulimuandama sasa uyu jamaa kwa nini aiseme kapata wapi na kwa nini ionekane kawaida?
 

Bona naungana na ww mia kwa mia! Bahati mbaya au nzuri ninazifahamu mansions nyingine za mheshimiwa zilizoko Mikocheni. Ni vitu vya uhakika jamani sio masihara. Kwa wale wanaoona huu ni wivu nadhani wako very wrong. Hakuna mtu anayemwonea jamaa wivu lakini tunafahamu tunavyowalipa hao watumishi wetu (enzi za Nyerere though kwa sasa sisi ndio tunawatumikia) jamani. Kuwa na biashara ya 10 bln then kiwe ni kitu cha kawaida its completely unfair. So if possible atuambia huo u multimillionnare (in $ not TSh) kwa viwango vya Forbes ameuotoa wapi?
 
ahahahaha...hapa naona tunapiga story tuuu...hakuna jipya...sasa si afadhali huyu anawekeza 10b hapahapa nchini..je hao waliowekeza 100b canada au india mnasemaje??...atleast mh. kidogo alichotuibia anarudisha kwa wananchi..corporate social responsibility..au sio?...kuliko wanaoiba na kuishia kukaa majumba ya msajili kodi 30,000/- kwa mwaka....

BIG UP MH. DR. Mwinyi kwa kutujali watanzania hata kama umetuibia unatumia na sisi walewale ulotuibia...huo ni uzalendo tosha na mfano wa kuigwa kwa wezi wooote wanaoiba mali zetu...IBENI KISHA MTUMIE KULETA MAENDELEO AMBAYO SERIKALI YETU IMESHINDWA KUYALETA...
 
Wananchi wa Mkuranga(?) jimboni kwake amewajengea nyumba ngapi bora ili kulipa fadhila za wao kumpa kura zao na hatimaye kufanya apate madaraka na nafasi ya kuweza kuwa bilionea?
 
Wananchi wa Mkuranga(?) jimboni kwake amewajengea nyumba ngapi bora ili kulipa fadhila za wao kumpa kura zao na hatimaye kufanya apate madaraka na nafasi ya kuweza kuwa bilionea?

mmh.. dada maswali mengine haya yanaitwa ya "ugomvi"... thanks kutukumbusha.
 

Tatizo hapa si mtu kujenga ghorofa ya hayo mabilioni. Mbona wengi tuu wanajenga? Swali ni huyu mwanasiasa kawezaje kuwa na huo uwezo bila kuwa na biashara inayoeleweka? Kwenye bango, mshitiri angekuwa ni kampuni yake, maswali yangekuwa mengine. Lakini yeye bila uoga amejibandika kama mshitiri binafsi, hapo ndipo maswali yanapokuja. Kama ni msafi basi haitakuwa vigumu kueleza umma huo uwezo amepata wapi. Wenzake wakina Mengi, George Ali, Co Architecture, Ali Mafuruki n.k. tunafahamu shughuli zao kwa hiyo hatushangai wanapoporomosha maghorofa na kuwekeza kwenye miradi mingine. Si wivu bali kutaka kupata uhakika tu.

Tatizo lingine ni conflict of interest. Hivi tukipata waziri wa ardhi ambae atataka kuwekeza kwenye real estate na ili kufanikisha, aanze kununua majengo ya NHC na kuingia nao ubia! Huyo nae tutamfumbia macho kuwa anatumia nafasi yake vibaya? sasa huyu ambae wako wote kwenye kabineti kwa nini tumfumbie macho? Hata kama sheria inamruhusu lakini ni lazima tuulize.

Amandla......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…