FP,Dah Nimepitwa na mambo:
Hivi mfanyakazi wa SERIKALINI anayefanya kazi zake kwa haki bila rushwa anaweza kukusanya (baada ya kulipia ada na matumizi ya familia) au kuwa na mali za shillingi billioni hata moja?
Jamani kukaa kwetu nje sana isiwe sababu ya kutojua hali halisi ya TZ. Kama u mtu wa haki na hakuna kupindisha mambo hata ukifanya kazi miaka 50 serikalini huwezi kuwa na billioni moja worth of ASSETS.
Na hujengi au kupanga kujenga Nyumba ya billion kumi kama huna ASSETs au collateral security angalau ya 2.5billion.
Mi nadhani Jasusi alikuwa na points tatizo alimhusisha Dr Mheshmiwa moja kwa moja ikaonekana ni PERSONAL.
FP
Kama ni kuhitimisha mjadala, nadhani hilo umelifanya vizuri tu. Mengine yote yatakuwa ni mazungumzo baada ya habari.