Mradi wa nyumba za kupanga wa Dr. Hussein Mwinyi Dar

Haya kampeni za uraisi wa Zanzibar zinavuta kasi hivo... hii post imekaa kikampeni hivi... je ya wezekana huyu Hussein ni tishio kwa wagombea fulani na mleta mada katumwa...? Is just my reflection... only a thought to ponder about...
 
good post, sasa hii iko poa, ile ya vyoo kidogo ilikuwa to de extreme!!!

Watanzania tuna assets nyingi sana tatizo ni kwamba hatujarasimisha na hapo ndipo wajanja wachache wanatuzidi na sisi kubaki kulalama!!!
 

Are you sure yupo peke yake kwenye hiyo investment? Je kama ana wabia?
 

Mwanafalsafa kaongelea kwamba huna uhakika kwamba hizi hela ametoa yeye peke yake au kama kuna kundi la watu.


Lakini, hata kama ni zake yeye mwenyewe, kuwa na hela nyingi si dhambi, na mimi leo nikija kupata deal legit la kunipa $ 10 m, naweza nisitake kutaja deal langu ni nini. Obviously Mwinyi kuwa Waziri kunazidisha haja ya transparency, kwa sababu yeye si mfanyabiashara wa kawaida, kwa hiyo in this case ninaweza ku stomach hili swali la "amepataje pesa" kirahisi zaidi.

Lakini katika mfumo wa biashara huria, kumuuliza mtu "umepataje pesa" ni ushamba, ni habari za a police state, citizen spying on citizen, kuturudisha nyuma kwenye ulanguzi, magendo, uzembe na uzururaji, mambo ya ki Sokoine. In the wake of the current catharsis, some would say desperate times warrant desperate measures, but I beg to differ and refuse to use "Mtego wa panya uwanasao waliokusudiwa na wasiokusudiwa". Above all, everybody is innocent until proven guilty, and even having $ 10 m is not enough of a "reasonable doubt".

Kwa hiyo, mtu akija kuuliza "fulani kapata wapi $ 10 m" mimi nitamuuliza vipi kama kukujibu hilo swali ni trade secret? Vipi kama huyu mtu kapata hela hizi legitimately, lakini kwa vile anajua wabongo walivyo geza geza wakijua tu mitkas yake kesho na wao wana open shop na kuwa competitors? Mtu kama huyu (save for the public office of Mwinyi) ana haki ya kukataa ku declare business zake publicly. Hii ndiyo free trade ninayoijua mimi, kama mnataka (mfanyabiashara wa kawaida)a fanye declaration itabidi m file katika relevant sources kwamba huyu bwana tuna mashaka na biashara zake, na sababu ni hizi na hizi, na sababu hizo ni lazima zi raise kwenye level ya "reasonable doubt".
 
Unahitaji tu kuwa na jina Mwinyi - hutakosa wateteaji tena, rukhsa tu. Kwani Shs. 10,000,000,000 kitu gani ? Mbona Benki wanazigawa kama njugu. ? Bahati yake, angekuwa Rostamu angekiona cha moto, hata biashara ya nyuma ya utumwa kwenye familia haingesaidia kitu. Collateral ? Mwinyi jina kubwa ati - kuna mwenye zaidi ?
 

Mwingine anaweza kusema unahitaji kuwa na jina tu la Mwinyi, hata ukinunua njugu na bigijii barabarani watu watapiga kelele umenunua kwa ufisadi.

Si Mwinyi bwana?

Hatukatai Mwinyi anaweza kuwa fisadi.

Lakini, mnaweza kutuonyesha ufisadi wenyewe?
 
ufisadi unaanza kwenye kupata kiwanja hapo Sea View, mimi nimetafuta saana kiwanja hapo to 1980 kabla alhaji hajawa Rahisi sikupata kiwanja.
August,
Si kiwanja tu. Hili jengo la Mwinyi lilikuwa mojawapo ya majengo yaliyotaifishwa wakati wa Azimio la Arusha. Nasikia (sina ushahidi) alipewa jengo hilo na baba yake yeye akalifanyia tu ukarabati. Kwa hiyo wale wanaouliza kuwa alipata wapi pesa za mtaji jibu ni hilo. August na Jasusi wasingeweza kuipata nafasi ya upendeleo kama huo na hapo ndipo ufisadi unapoingia. Kumbuka huyu alishawahi kupewa tenda ya kuleta magari ya jeshi wakati baba yake ni rais. Huo pia kweli siyo ufisadi ni nini?
 

Sasa hapa mnaanza kuongea, albeit hesitantly.

Jasusi kama ungeweza kuvalidate madai watu wangeweza kuwabana hapa hii process ya baba kumpa mtoto jengo lililotaifishwa ilikuwaje, mambo ya conflict of interest yameendaje etc etc.

At least unakuwa na kitu concrete cha kusema ufisadi umeanzia hapa, hata kama mtu anataka kuanza uchunguzi anajua aanzie wapi.

Sio unapiga simu Fire Brigade wanakuuliza moto uko wapi unashindwa hata kutoa address!
 
Kinyambiss,
Ningekuomba na wewe uende benki tuone utajenga apartments ngapi. Ukishafanya hivyo rudi hapa ututukane sote kuwa ni wapumbavu.
Mkuu Jasusi,

Lakini tuwe waangalifu pia; tutaishia kuwaita Watanzania wenzetu wote wezi huku wageni wanatuibia kilaini.

Kuna wageni chungu nzima wanajenga apartments hapo Dar na wala hatuwashikii bango lakini tukimwona Mtanzania anafanya hivyo, tunaanza kumwita mwizi kabla hata hatujajua pesa katoa wapi.

Inabidi tusiwe negative sana pale tunapoona Watanzania wenzetu wanafanikiwa. Ndio kunaweza kuwa na wezi lakini wengine huenda wanafanikiwa shauri ya kujituma na kuchapa kazi kwao.
 

Now its getting interesting!!!! let me recharge my battery!!
 
Hawa masultan mliwaweka wenyewe madarakani sasa mnalaumu nini enyi wadanganyika?
 
matatizo ya viwanja bongo linajulikana, ubadilishaji wa open space kuwa kiwanja cha mtu kwa makazi au biashara unajulikana bei za viwanja mwaka 80 ilikuwa ni bei ya serikali tshs 3,000.00 unapata kiwanja tatizo ni urasimu na kujua na ufisadi. je unataka niseme nini zaidi ya hiyo.

katika uislamu wanasema haramu huendelea kuwa haramu, sasa hata ukisema leo hii fulani anazo 10bn au kakopa lakini source ya kufika hapo ni ufisadi mtu atabaki kuwa fisadi. juzi juzi hapa tulisikia Alhaji ana mashamba kilombero/ some where in morogoro, je ulikuwa unajua hayo?

sheria za utawala bora au manunuzi zinaona utumiaji wa wakala badala ya kununua toka kwa mtengenezaji ni ufisadi lakini mambo hayo tanzania yanafanyika kila siku, je wajua ni vingapi vya kifisadi vinapitishwa hapo? na yakizungumzwa serikali/viongozi watachukua miaka mitatu wako kimya na kununua magazeti au report tuhuma zisijulikane kwa watu au kusema oh ndio kosa limetokea lakini huko mbele tunatarajia kupeleka mswada bunge ili kuzui jambo kama hilo lisitokee tena.

kwa wenzetu tutasema ufisadi ha upo kwa sababu wewe ukienda ardhi unapewa namba ya kumuona muhusika, lakini bongo waweza kushinda ardhi siku nzima na mtu wa kumuona usimuone, ukapeleka application wa kwanza kutaka kiwanja fulani akapewa wa mwisho, sasa sijui hicho kitu wewe utakiita nini, kama sio ufisadi.

hadithi ya bagdhad unaijua au uliwahi isikia, chavda nk ipo siku haya yote yata toka wazi wazi ndipo hapo wote tutasema kumbe ilikuwa hivi?
 
Naona bongo usiwe kiongozi tu watu watakuita 'fisadi'
 
Mkuu Mtanzania,
Nakubaliana kabisa.Ni kweli kuna wageni wengi wanajenga hivi sasa apartments au hata nyumba kama anavyofanya balozi wa zamani wa Marekani Rev. Stith. Lakini hawa inajulikana wamekuja na fedha zao za kuwekeza. Katika kesi ya Mwinyi, kama nilivyosema awali katika bandiko jengine, huyu hakujenga. Alirithi jengo na kulibadilisha tu kuwa apartments.Suali linakuja, je alilipataje jengo hilo? Ningependa kuona Watanzania wenzangu wakihangaika na uwekezaji. Kama jamaa kasota na lori lake ameuza ndizi kutoka Moshi hadi Dar mwaka nenda rudi na kajiwekea akiba, akiamua kuporomosha jengo Dar au Moshi nitakuwa wa kwanza kusema "more power to him."
 
10 bil Tsh Mtanzania civil servant hujawahi kufanya hata biashara ya baa, hata hayo mabenk yanayokupa pesa hiyo lazima uwe na collaterals za kutosha! Ni rahisi kuja na hitimisho Angekuwa Ballabou, au R. Mengi, au Aboud watu wange-jump kwenye conclusion haraka hiyvo? Watu wana reason nenda wewe na kijumba chako cha Mil5 kama utapewa hata hizo Mil 20!
Hapa We dare to talk Bwana Usianze kuita watu majina ya kilevi levi hapa
 
Kiranga,
Ningekuwa bongo sasa hivi mbona hii ni kazi ndogo tu? Remember I am Jasusi, no?
 

Jamani Manafalsafa kauliza swali zuri tu halijajibiwa...Vipi kama ana wabia???????
 
mtoa rushwa na mpokea rushwa wote lile neno alilotumia mwalimu mali manganya?
na kama unasema ni enterprneur tupe faili la biashara zake na kodi anayo lipa na pia uhaki katika kufanya biashara zake dhidi ya mtu mwingine. na kumbuka kuna kisa kilitokea ilipokuwa ofisi ya zambia airways kuchukulia na familia ya kwanza wakati huo, wakati kiutaratibu hiyo sehemu ilitakiwa iwe available kwa applicant wa kwanza, sasa hiyo utasema ni fair play, kuna loliondo gate, kuna dhahabu kusafirishwa nje, kuna uwanja wa kia kukodishwa kwa $1000.00 kwa mwezi kwa miaka 25 nk hadithi ni ndefu hata hatuwezi kuimaliza leo , bali tunakupa viashiria vya mchezo mchafu.
 
Balantanda,
Kama kuna wabia then it should be transparent. Wafahamike.

Tatizo hapa sio Dk Mwinyi,tatizo ni huyu mletaji wa thread mwenyewe kaleta mada ambayo haijakamilika,iko nusunusu na hata hiyo attachment aliyoiweka haifunguki...Matokeo yake watu tumeanza kujadili kitu ambacho kimsingi hakijitoshelezi/hakijakamilika...Tumeanza tu kutoa tuhuma za ufisadi kwa Dk Mwinyi pasipo hata kujua uhakika wa taarifa yenyewe(ni bora ingekuwa hata kwenye tetesi basi)

Ni vema mletaji wa thread hii akaja hapa kusahihisha taarifa yake hii ikiwa ni pamoja na kuiweka vizuri attachment yake ili tuweze kujadili kitu kilichokamilika na kinachoeleweka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…