Mradi wa nyumba za kupanga wa Dr. Hussein Mwinyi Dar


...achilia mbali drainage systems, hata maji safi ya bomba pressure imekuwa ndogo miaka kadhaa sasa mitaa ya Upanga.
Same applies all over city centre, Drainage system ni ile ya Mjerumani.

Hilo ni tatizo jingine ambalo Mipango jiji wameamua kulifungia macho, labda kutokana na kauli kama hizi...

 
Itakuwa kazi sna kuniamisha kuwa kiongozi anatakiwa awe na li-mjengo kama hili! I may have thousand reasons kujustify maneno yangu, hasa hasa tunaposema kiongozi!
 
Itakuwa kazi sna kuniamisha kuwa kiongozi anatakiwa awe na li-mjengo kama hili! I may have thousand reasons kujustify maneno yangu, hasa hasa tunaposema kiongozi!

Na huyu Kikwete anasema kwamba sasa kuna haja ya kutenganisha siasa na biashara lakini wala hayuko more specific. Je, kauli hii inamaanisha nini kwa wale wafanyabiashara ambao pia ni wanasiasa ambao sasa hivi wamejaa tele katika nafasi mbali mbali kuanzia Wabunge, Wakuu wa Wilaya/Mikoa na Mawaziri.

Je, hawa wataambiwa kama watanaka kuendelea kuwemo kwenye siasa wafunge mabiashara yao au ni kauli ya usanii tu kama kauli nyingine nyingi za Kikwete!? Kuna miezi 7 tu kabla ya uchaguzi mkuu Kikwete inabidi aweke wazi siasa na biashara zitatenganishwa vipi?
 
Bubu,
Don't you ever take Kikwete's word to the bank. Ana kipawa cha kusema maneno mazuri lakini subiri katika utekelezaji/utendaji. Unakumbuka aliyosema kuhusu madini? Unakumbuka alisemaje kuhusu Richmond na hela zetu? Kiongozi unaposema kitu lazima uwe umeshafikiria mkakati wa kutekeleza kile unachokisema, ama sivyo zitabaki ngonjera tu.
 

Naam Mkuu Jasusi kauli zake zite ni usanii mtupu. Hakuna hata moja katika kauli zake alizowahi kuzitoa zimekuwa na matokeo mazuri..unayakumbuka mabilioni ya Kikwete? Yote yaliishia kwa mafisadi hata kuzungumzia nani aliyepewa mabilioni yale sasa hawataki kuwataja, imekuwa ni siri kubwa sana.
 

Fundi,
Umeiona, ni Win Win all the way!
 
na sio drainage system tu, na barabara pia hazitoshi yaani concetration yetu ya majengo/maendeleo yapo sehemu moja tu, mjini, kariakoo, upanga, sasa tunakuja magomeni, mikocheni, masaki, mwananyama, mwenge, ubungo ambako kote huko kuna foleni za kumfaa mtu.
 
Kwenye hili kumsema Dr Mwinyi kama mtu binafsi nafikiri tunamuonea.
Tuulaumu mfumo tuliojichagulia kuendesha nchi. Hii ni biashara, tena inalipa bila jasho.

Mosi, sheria na kanuni tulizonazo hazikatazi kiongozi kuwa mfayabiashara, na i bet zaidi ya asilimia 90% ya viongozi wetu ni wafanyabiashara, tofauti ni ukubwa wa biashara.

Pili, kama mradi huu utajengwa palipokua nyumbani kwake seaview(wakauziwa kama viongozi wengine) basi ni deal ambayo hata leo kama kuna JF member ananyumba au plot mitaa ile(maana ni nyumba kama kumi tu pale) zenye viwanya vikubwa(around an acre) na vinapakana directly na Indian ocean kwa nyuma, basi ani-pm namimi ntampa deal kama hiyo tena kwa mabenki ya kuchagua.

Tukumbuke kwenye Real Estate, location makes all the difference. Majirani zake pale walikua mzee Malechela, Kida, na zamani alikuwepo Shelukindo. Hilo eneo ukijenga prime apartments una guarantee ya kupangisha kila moja kwa USD 2000-3000 kwa mwezi.

Benki wakishaona specifications za finished apartments na wakatazama location, wao watakwambia uwaachie hati ya plot, na project mtai manage pamoja mpaka mkopo uishe.

Sanasana watataka uwe na kianzio cha ujenzi ambacho kinarange kati ya 10% -25% ya thamani ya mradi ambacho unaweza uwa nacho au kuomba mkopo kwenye banks mbili au tatu
tofauti wakakubaliana.

Option ya pili ni kuingia mkataba na mwekezaji kwa maana ya B.O.T

Hiyo miradi ipo mingi tu Upanga, and NO, majengo mengi yanayoota Upanga wenye hati ni wazalendo hawajayauza. Mwekezaji anakuja na terms, mkielewana anakubali uweke jina lako kwenye bango. Deals nyingi ni kuwa mwenyewe utapewa apartments mbili au tatu uzimiliki, zinazobaki zinakua za mwekezaji na atapangisha na kula faida for 15 to 25years depending na u-sharp wa kunegotiate, na baada ya hapo mali yote inarudi kwa owner wa hati.

Tuache kutupia kila kitu banner ya ufisadi. Tutapoteza maana ya vita takatifu. Mafisadi wanachotaka ndio hiki, kwamba kila mwenye biashara ni fisadi( kwa maana ya ubadhirifu kwa kutumia ofisi ya umma). Tusichukie, badala yake, kuna maeneo sasa hivi Gezaulole, na kuendelea, tuchangamke tukanunue mashamba sasa hivi ili baadae mji ukikua, atajipendekeza mwekezaji, na wewe utaanza kuitwa fisadi sababu enzi hizo kutakua ni prime area.

Mnaoita ufisadi nawachallenge mtu yeyote mwenye property kwenye ile line aliopo mzee Malechela(ni nyumba kama 10 tu pale zinazoipa mgongo Indian Ocean) aje na write-up kama hiyo halafu aone kama hatopata mkopo wa kujenga luxury apartments wa USD10m au hata 20m.

Why is that? LOCATION, LOCATION and LOCATION.
1.City Centre(10minutes kwa foleni ya sasa, zamani 2-5minutes), include convinience for night-life, shopping, proximity to best hotels and restaurants.
2. Full Indian Ocean View in the backyard.
3. Big plot, 1 acre plot.
4. Utulivu(most quite prime location with minimum crime rates similar to Oysterbay Laibon st)
5. Tarmac road inapita usoni kwa plot.
6. Prime private hospital(Agakhan) within 3 minutes.

Kama kuna yeyote anayejua anything about Real Estate Market ya Dar es Salaam, namchallenge aje na property with similar features and i will show him the BANK.

Tuwe reasonable wakuu, kama hamjui ulizeni mtaambiwa.
 
Alwatan,
Well said. Lakini swali linabaki pale pale. Mwinyi alipataje hayo majengo au jengo? Jasusi au August kweli wanayo nafasi sawa kama Hussein Mwinyi? Hapo ndipo panapogomba. Alipewa hilo jengo na baba yake na hapo ndipo misingi ya ufisadi inapoingia.
 

wenyewe wanasema "thats the crux of the matter"...
 

Mkuu, good question.

Kama nilivyosema tatizo letu ni mfumo tuliojichagulia. Swali hilo mwenyewe wa kujibu ni Mkapa na Magufuli walipoamua kuuza nyumba za serikali.

Dr Mwinyi alihamia nyumba ambayo kabla yake alikua anakaa marehemu Dr Chiduo akiwa waziri wa afya pale Sea View. Baada ya uza uza ya Magufuli ndipo nayeye aliponunua kama watumishi wengine 3000 waliouziwa nyumba za serikali. So it has nothing to do na yeye kupewa nyumba na baba yake.

Kama ni crux of the matter basi ni Mkapa na Magufuli.
 
Hivi lets say mimi ni mtoto wa kiongozi, naandika business plan yangu kisha naenda benki kuomba mkopo.
Loan officer wa benki anaangalia ile aplication anaona last name NZITO! ananipa mkopo kwa sababu ya nguvu ya jina.

Hapo mnaweza mkanilaumu kweli? Au mkasema nimefanya ufisadi?
 

Mimi siwezi kukulaumu.Nime raise same point earlier, kwamba tuonyeshe ufisadi aliofanya huy mtu uko wapi.Otherwise tunaweza kumlaumu mtu aliyefuata process to the letter na kupata advantage ya swift service kwa sababu ya jina, advantage ambayo inatakiwa kupewa Watanzania wote, na kama haifanywi kwa Watanzania wote si kosa la Mwinyi, bali ni la watoa huduma.

Nakataa kumu indict mtu kwa sababu ya kukosekana ushahidi wa nguvu.
 
kwa hiyo ni serikali ndiyo iliyo mpa mtaji almost free of charge wakati mimi na wewe tumenyimwa, ndipo ufisadi wenyewe unapoanza, na tunapo mshikia bango dr sio kama tuna personal vandetta nae lakini ndio mwanzo wa kudai kilicho chetu, ndio maana ukipitia post zangu humu kuna mahali nilitaja watu kununua nyumba za tpdc wakati sio wafanyakazi wa tpdc maeneo ya upanga. na kule kwenye thread ya nyumba za serikali nilisha sema the best option ilikuwa hiyo government agency kujenga hizo apartment na kupangisha iwe kwa mfanyakazi au mtu binafsi nk.
kuna siku wenye mali watataka mali zao, hapo ndipo nguo itachanika.
 
Mzee Mwinyi anasema kuwa - Azimio la Arusha halijafa!..mengine jazeni wenyewe.

Huyu naye ni msanii. Mwalimu alipokuwa hai na kutamka kwamba Azimio la Arusha wameliua hata mguno wa kupinga kauli ya Mwalimu hakutoa, leo miaka chungu nzima baadaye ndiyo anajidai kutoa kauli ambayo wengi wetu tunajua ni uwongo wa hali ya juu.
 

Mazee kama information zako ni accurate, umemaliza mjadala.

Jamaa kama kafuata proces sawa na watumishi wengine wa serikali huwezi kumlaumu directly yeye kama Mwinyi.

Kama unataka kulaumu laumu proces nzima ya kuuza nyumba za serikali, ambayo Mwinyi alikuwa kinda low on the food chain. Yeye alifanya kile ambacho watumishi wote tu walifanya. Kwangu mimi hili kama ni la uhakika linamtolea lawama.
 
Huyu naye ni msanii. Mwalimu alipokuwa hai na kutamka kwamba Azimio la Arusha wameliua hata mguno wa kupinga kauli ya Mwalimu hakutoa, leo miaka chungu nzima baadaye ndiyo anajidai kutoa kauli ambayo wengi wetu tunajua ni uwongo wa hali ya juu.

Tatizo Mwinyi alikuwa rais lakini kama haelewi nini kinaendelea.

Naona siku hizi watu wana over use epitaph ya "rais ana nia nzuri lakini anakwamishwa na watendaji wake" to the extent ya kui dilute ukweli wake, kwa maana ya kwamba inatumika kama utetezi kwa rais hata katika issues ambazo rais anazielewa vizuri. Kwa hiyo mimi mara nyingi huwa napinga usanii huu.

Ubovu wa Mwinyi ni kwamba katika enzi yake ni kweli rais alikuwa anapelekwa pelekwa tu. Kukupa mfano mmoja, wakati Jaji Nyalali alipotoa ripoti iliyoletea vyama vingi, rais Mwinyi hakuwa anajua chochote kuhusu vyama vingi, akauliza nani anaelewa haya mambo vizuri, George Liundi akaanza kumsomesha rais, Mwinyi akamwambia kazi ya kusimamia process ya vyama vingi ni yako, ndivyo Liundi alivyopata kuwa Msajili wa vyama vya siasa, kutoka nhapo Liundi akisema kitu kwa Mwinyi mwinyi anapitisha tu.Ndivyo alivyokuwa anafanya kazi Mwinyi, kama walii, anateua wapambe wake halafu anawaachia wafanye wanavyotaka, complete trust.

Kwa hiyo mimi siwezi kushangaa kama Mwinyi sincerely alifikiri kwamba "haliui" Azimio la Arusha, huku liutenants wake wakijua kwamba hilo ndilo lengo. Sijui for sure, inawezekana alijua, lakini inawezekana pia kwamba alikuwa railroaded na liutenants wake.

Hususan kwa sababu Mwinyi alivyochukua nchi, kulikuwa na ki beef kati ya Mwinyi na Nyerere, rejea mpaka insurbodination ya marehemu Tim Apiyo aliyekuwa anatoa mambo Ikulu na kumpelekea Nyerere, ndiyo maana Mwinyi akamuondoa na kumuweka Paul Rupia kama PS kiongozi.

In my opinion Nyerere alikuwa ana exercise right yake ku opine and all, lakini katika nchi ambayo alikuwa demigod kama enzi zile Tanzania kulikuwa na better ways of doing that than kumu undermine a sitting president openly.I don't agree totally with Joseph Warioba's assertion that a president as the symbol of sovereignty should be treated almost like a Tsar with deference, after all even the Tsars and Caesars were challenged, but on the other hand a president is truly the living symbol of soveregnity if there ever was one, so I can understand where Mzee Warioba's assertion is coming from, na Nyerere, god bless his soul, alisema vitu ambavyo vilikuwa necessary kusemwa, lakini tone yake ilikuwa rather cavalier, ni kama alikuwa anamake a subtle statement kwamba yeye bado alikuwa rais anayem remote control Mwinyi, kitu kilicho mu alienate Mwinyi even further from Nyerere. Na kwa sababu Mwinyi si mtu wa kujibizana mzee wa watu, hakutaka kujibizana na Nyerere, akampa eminence tu kwa kusema "Nyerere ni kama mlima Kilimanjaro, mimi ni kama kichuguu" no humbler words have been spoken by a Tanzanian president.

Ingawa wapenda kupindua mambo na waswahili tunaweza kusema kwamba ukimya na humility ya Mwinyi inaweza kuwa na a deep retaliation kuliko inavyoonekana kwa juu juu, kwamba hata kumlinganisha Nyerere na mlima Kilimanjaro hakukuwa sifa kama inavyofikiriwa, bali kijembe kwamba Nyerere ameshafikia mwisho wa career yake na amekuwa "larger than life" na dormant ambaye hawezi kulipuka/ kukua kama mlima Kilimanjaro, wakati Mwinyi ndiye aliyekuwa katika peak ya career yake na ana potential ya kukua haraka na kuleta economic activity kama kichuguu kilivyo busy.

But that could just be my over-analysis.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…