Mbu
JF-Expert Member
- Jan 11, 2007
- 12,752
- 7,861
Mkuu Mbu, mimi wasiwasi wangu katika haya maghorofa yanayoibuka kama uyoga ni kuhusu drainage system. Je nazo zinaongezwa ili kukidhi mahitaji makubwa ya ongezeko la watu katika maeneo mbali mbali ya Jiji au bado ni zile zile za mwaka 47!? Kama haziongezwi basi baada ya miaka michache maeneo mengi kama ya Upanga, Oysterbay etc na kwingineko ambapo sasa hivi hakuna tatizo la maji machafu hali itabadilka na maeneo haya kuharibika sana kutokana na mafuriko ya maji machafu.
...achilia mbali drainage systems, hata maji safi ya bomba pressure imekuwa ndogo miaka kadhaa sasa mitaa ya Upanga.
Same applies all over city centre, Drainage system ni ile ya Mjerumani.
Hilo ni tatizo jingine ambalo Mipango jiji wameamua kulifungia macho, labda kutokana na kauli kama hizi...
Kikwete awaonya Ardhi
Atangaza yu pamoja na Magufuli kusafisha wizara
Ninyi mna nafasi nzuri na muhimu. Itumieni vizuri kwa kupanga miji vizuri. Mkifanya vizuri mtaweza kupunguza tatizo hili kwa robo tatu. Hakuna atakayewatisha ikiwa mimi na waziri wetu tuko pamoja nanyi. Akitokea mtu wa kuwasumbua nileteeni.
Tujirekebishe kurudi kwenye mstari. Baada ya miaka miwli tutaangalia, watakaokuwa wameshindwa watatuwia radhi,Awali, Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Martin Madekwe, alisema utaratibu wa shirika hilo kushirikiana na sekta binafsi katika kujenga majengo mbalimbali ulianza mwaka 1990.source; http://www.freemedia.co.tz/daima/2006/8/16/habari3.phpAlisema kuwa mradi wa Sea View ulibuniwa kwa lengo la kuondoa jengo dogo chakavu ambalo lilikuwa na ghorofa mbili. Alisema jengo la sasa lina ghorofa 10.
Mradi huu umegharimu sh bilioni tatu. Shirika linapata kodi ya pango ya sh milioni 2.8 kwa mwezi ukilinganisha na sh 151,000 kwa jengo la zamani.
Pamoja na manufaa yote haya, bado shirika linakumbana na vikwazo vingi. Baadhi ya wapangaji wetu wakisaidiana na watu wengine wasiopenda maendeleo, wanapinga sera hii ya uendelezaji wa maeneo. Wao wanataka miji ibaki kama ilivyo.