DOKEZO Mradi wa Starcity ni hatari kwa Wakazi wa Morogoro

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Chanazi

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2010
Posts
212
Reaction score
64
Katikati ya eneo la Kitungwa na Nanenane MOROGORO kuna huu mradi wa Star City wenye Viwanja vingi ambavyo havija endelezwa kwasababu mbalimbali! Serikali ya mkoa iingilie kati kwa manufaa ya wengi kwani eneo hilo sasa ni tishio la usalama! Eneo limekua

1. Maficho ya Wezi, Eneo hili linatishia usalama wa wakazi wa karibu kwa kutumika kufuga wezi na kua maskani ya uharifu.

2. Kuzuia maendeleo ya Mji, eneo la mradi wa StarCity ni eneo kubwa lililopo takribani kilometer 8 tu kutokea katikati ya Mji, pori hili linakosa maendeleo kwasababu wamiliki wa mradi wana uza maeneo kwa masharti magumu na bei kubwa hali inayo sababisha kudorola kwa maendeleo eneo hilo kubwa!

3. Migogoro Kati ya Binadamu na Wanyama waharibifu, Nyoka wakubwa na wanyama wadogo wadogo wanaweza kushambulia watu au kuharibu mazao, kusababisha hasara kubwa kwa wakazi.

Inaombwa Mamlaka husika ziingilie kati kwa Maendeleo ya Mji wa MOROGORO na kudhibiti uhalifu, hakuna Mji unao kua Pori kubwa katikati ya Mji!
 
Na ile road ni mbaya ya kwenda Tungi naomba kila siku wale watoto wafike salama home aiseee.
 
Changamoto sana !! Hawataki kuuza Viwanja kwa bei rafiki wanasababisha Mji una Pori katikati !!
 
Hilo eneo kwa kweli linarudisha nyuma maendeleo ya mji. Hao starcity ni utapeli mtupu na ujanjaujanja hakuna lolote wanalofanya. Serikali itwae hilo eneo kwa manufaa ya umma. Nashangaa hospital ya rufaa tuliohaidiwa kujengwa inaenda kujengwa kiyegegea badala ya kulitumia hilo eneo.
 
Katikati ya eneo la Kitungwa na Nanenane MOROGORO kuna huu mradi wa Star City wenye Viwanja vingi ambavyo havija endelezwa kwasababu mbalimbali! Serikali ya mkoa iingilie kati kwa manufaa ya wengi kwani eneo hilo sasa ni tishio la usalama! Eneo limekua

1. Maficho ya Wezi, Eneo hili linatishia usalama wa wakazi wa karibu kwa kutumika kufuga wezi na kua maskani ya uharifu.

2. Kuzuia maendeleo ya Mji, eneo la mradi wa StarCity ni eneo kubwa lililopo takribani kilometer 8 tu kutokea katikati ya Mji, pori hili linakosa maendeleo kwasababu wamiliki wa mradi wana uza maeneo kwa masharti magumu na bei kubwa hali inayo sababisha kudorola kwa maendeleo eneo hilo kubwa!

3. Migogoro Kati ya Binadamu na Wanyama waharibifu, Nyoka wakubwa na wanyama wadogo wadogo wanaweza kushambulia watu au kuharibu mazao, kusababisha hasara kubwa kwa wakazi.

Inaombwa Mamlaka husika ziingilie kati kwa Maendeleo ya Mji wa MOROGORO na kudhibiti uhalifu, hakuna Mji unao kua Pori kubwa katikati ya Mji!
Liko njia ya kwenda wapi? Vizuri utufahamishe ili tuweze kuchangia, kuna pori jingine Magadu nalo linatisha, hili linamilikiwa na Jeshi la Wananchi na SUA.
 
Kama unatoka 88 kuelekea kingolwira mkono wa kushoto kwenye mashamba ya katani
Hilo halitishi kama lile la SUA Apopo Magadu Iringa Road ya zamani, huko kuna misitu ya miombo ile ya miaka ya 50.
 
SUA nao ni tatizo, wana maeneo mengi tu wameacha mapori na vibaka wanayatumia kupora bodaboda na raia. Ukiingia campus ya mazimbu mpaka Lukobe ni mapori tu
 
Mapori kila kona Moro, na hawayaendelezi yanafanya Mji unakua porini! Na maficho ya waharifu
 
Changamoto sana huu Mji wetu!
 
Mapori kila kona Moro, na hawayaendelezi yanafanya Mji unakua porini! Na maficho ya waharifu
Mwanzo niliamini polisi wanajificha juu ya mlima hivyo wanaweza kuwaona waharifu kwa urahisi, kumbe sivyo, niligundua wanakimbia vumbi jekundu huku chini..
 
Ni mradi wa zamani sana kwa kuuona, kwanini hauuziki? Kwamba morogoro inakuwa taratibu kiasi hiko?

Ingekuwa Dodoma pangeshajaa.
 
Tatizo lingine watu wamenunua hivyo viwanja kama asset ili vije viwanufaishe baadae. Kuna watu wazito tu wamenunua hivyo viwanja. Hilo nalo ni tatizo ndio maana mji hauendelei. Watu wanajenga pembezoni mwa mji hali ya kuwa katkat ya mji bado kuna viwanja
 
SUA nao ni tatizo, wana maeneo mengi tu wameacha mapori na vibaka wanayatumia kupora bodaboda na raia. Ukiingia campus ya mazimbu mpaka Lukobe ni mapori tu
Mapori ni sehemu ya shule kwa Sua. Maana kuna watu wanasomea digriii ya misitu pia na Nyuki
 
Tatizo lingine watu wamenunua hivyo viwanja kama asset ili vije viwanufaishe baadae. Kuna watu wazito tu wamenunua hivyo viwanja. Hilo nalo ni tatizo ndio maana mji hauendelei. Watu wanajenga pembezoni mwa mji hali ya kuwa katkat ya mji bado kuna viwanja
anhaaa now nimeelewa .
 
Back
Top Bottom