Kwa kutumia teknolojia aliyojifunza nchini China katika shamba la maskani yake, Augustine Phiri ameweza kuongeza mavuno ya mahindi katika shamba la mfano nchini Malawi, kutoka tani 2.1 kwa ekari moja mwaka 2023 hadi tani 8 kwa ekari moja mwaka huu, ikiwa ni karibu mara nne ya mavuno ya mwaka jana.
Mwaka 2019, Augustine Phiri alipata fursa ya kusomea teknolojia ya kilimo kwa miaka mitatu nchini China, ikiwa ni sehemu ya Mradi wa Sayansi na Teknolojia ya Kilimo wa China na Afrika. Mradi huu ulikutanisha wanafunzi 34 kutoka nchi nane za Afrika kwa lengo la kuonheza ufahamu wao na ujuzi halisi katika kilimo cha kisasa, mradi ambao ulizinduliwa mwaka 2019 na Chuo Kikuu ch Kilimo cha China katika Kituo cha Mfano cha Quzhou kilichoko mkoani Hebei, kaskazini mwa China. Mpaka sasa, jumla ya wanafunzi wa kigeni 91 kutoka nchi 12 za Afrika wameshiriki kwenye mradi huo.
Mwanafunzi mwingine wa program hiyo, Francina Lerata Kuwali, ameeleza athari mbaya ya hali ya hewa ya El Nino nchini Malawi, nchi ambayo imeshuhudia ukame na mafuriko ya mara kwa mara katika miaka ya karibuni. Francina anasema, wakati wakipata mafunzo, mwaka wa kwanza walimaliza kozi zote za nadharia na mafunzo ya kivitendo nchini China. Katika mwaka wa pili, walitumia ujuzi walioupata nchini China katika nchi zao za Afrika, na katika mwaka wa tatu, walirejea nchini China ili kuandika na kutetea tasnifu zao. Anasema katika mchakato huo wote, waadhiri waliwapa miongozo kwa kupitia mtandao wa kijamii wa WeChat, huku masuala muhimu yakitatuliwa kupitia mikutano iliyokuwa ikifanyika kwenye mtandao.
Jiao anasema, wanafunzi wa kigeni wanachukua nafasi muhimu sana katika kuwapa moyo wakulima wa Afrika kujihusisha na majaribio, na kuwasaidia kumudu na kutangaza teknolojia bora za kilimo. Kwa kujumuisha ufahamu walioupata nchini China na hali halisi ya kilimo barani Afrika, wanafunzi wanasaidia matumizi ya teknolojia hizo, na hatimaye kuongeza uzalishaji kwa wakilima wadogo.
Baada ya kurejea nchini China hivi karibuni akitokea nchini Kenya, Jiao anaeleza mipango ya baadaye inayojumuisha kupanua Mradi wa Sayansi na Teknolojia ya Kilimo wa China na Afrika katika nchi nyingine za Afrika kama Kenya, Zambia na Ethiopia.
Jiao anasema, China inalisha zaidi ya watu bilioni 1.4 ikiwa na asilimia 9 tu ya ardhi inayofaa kwa kilimo duniani. Teknolojia ya kilimo inafaa mahitaji ya wakulima wadogo wa barani Afrika, na kilimo cha Afrika kinaweza kunufaika sana kutokana na ujuzi wa kilimo wa China.