Pre GE2025 Mradi wa uboreshaji wa miji Tanzania (TACTIC) Geita Mjini, Mbunge alalama ubabaishaji wa mkandarasi, Tuliahidi mradi kukamilika kabla ya uchaguzi

Pre GE2025 Mradi wa uboreshaji wa miji Tanzania (TACTIC) Geita Mjini, Mbunge alalama ubabaishaji wa mkandarasi, Tuliahidi mradi kukamilika kabla ya uchaguzi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Mbunge wa Geita Mjini, Constantine Kanyasu, amemshutumu mkandarasi anayetekeleza mradi wa uboreshaji wa miji Tanzania (TACTIC) mjini Geita, akimtaja kuwa hana uwezo, hana mtaji, na anakosa wataalamu wa kutekeleza mradi huo kwa ufanisi.

Kauli hiyo ya Kanyasu imekuja siku moja baada ya Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martine Shigella, kuagiza kuwa mkandarasi huyo asiongezewe muda zaidi wa kukamilisha kazi, kwani ameshindwa kutimiza matakwa ya mkataba.

Mradi wa TACTIC mjini Geita unatekelezwa na kampuni ya Sichuan and Bridge Group Corporation Limited, huku ukisimamiwa na wahandisi washauri M/s Luptan Consultants Limited na SAFI Consultants Limited. Mradi huu unahusisha ujenzi wa kilomita 17 za barabara kwa gharama ya shilingi bilioni 22, ukiwa unafadhiliwa na Benki ya Dunia (WB).

Soma pia: Pre GE2025 Miradi kuelekea Uchaguzi Mkuu: Mhandisi Kundo akagua mradi wa maji unaonufaisha zaidi ya wakazi 200,000 Chalinze

Mkataba wa mradi huo ulisainiwa tarehe 25 Oktoba 2023, ukitarajiwa kukamilika ndani ya miezi 15, kufikia tarehe 19 Februari 2025. Hata hivyo, hadi kufikia tarehe 4 Machi 2025, utekelezaji wa mradi huo ulikuwa umefikia asilimia 37 pekee.

MKUU WA MKOA: HAKUNA ONGEZEKO LA MUDA

Mkuu wa Mkoa, Martine Shigella, alitoa maagizo hayo katika kikao cha Bodi ya Barabara, akisisitiza kuwa baada ya mkataba wa awali kuisha na mkandarasi kupewa nyongeza ya miezi mitatu, hatakiwi kupewa muda zaidi.

Aliagiza Ofisi ya Katibu Tawala wa Mkoa kushirikiana na TAKUKURU kuchunguza iwapo fedha alizolipwa mkandarasi zinawiana na kazi aliyoifanya, ili hatua zichukuliwe iwapo kuna ubadhirifu.

"Mkandarasi huyu ameshindwa kazi. Kama ndani ya miezi 18 ameweza tu kukamilisha asilimia 37 ya kazi, haiwezekani kwamba miezi mitatu iliyobaki atamaliza asilimia 63," alisema Shigella.

Aliongeza kuwa wananchi walitangaziwa kuwa barabara hizo zingekuwa tayari kabla ya uchaguzi, lakini hadi sasa hazijakamilika, hali inayosababisha usumbufu mkubwa.

HALMASHAURI YA GEITA: MKANDARASI ALIOMBA ONGEZEKO LA MUDA

Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Geita, Ndalo Samson, alisema baada ya mkataba wa awali kumalizika Februari 19, 2025, mkandarasi aliomba kuongezewa muda wa zaidi ya miezi sita.


TUJIKUMBIUSHE KILICHOTOKEA SIKU ZA NYUMA KUHUSU MRADI HUU
Januari 31, 2025: Mkuu wa TAKUKURU Geita, Azan Taita alisema Mkandarasi hana uwezo wa kutekeleza mradi huo na kwamba anashauri mkataba uvunjwe

Agosti 27, 2024: Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI anayeshughulika na Miundombinu, Mhandisi Rogatus Mativila alisema Mkandarasi huyo yupo nyuma kwa Asilimia 26.
 
Back
Top Bottom