Mradi wa ujenzi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano nchini Zambia uliofadhiliwa na China wakamilika

Mradi wa ujenzi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano nchini Zambia uliofadhiliwa na China wakamilika

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
1654065408934.png


Hafla ya kukabidhi Kituo cha Kimataifa cha Mikutano kilichojengwa kwa ufadhili wa China imefanyika jana katika mji mkuu wa Zambia, Lusaka..

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Rais wa Zambia Hakainde Hichilema amesema, tangu Zambia ipate uhuru, China imetoa misaada mingi katika juhudi za kuhimiza maendeleo ya kiuchumi na kijamii ikiwemo ujenzi wa Reli ya TAZARA. Ameongeza kuwa, katika miaka ya karibuni, nchi hizo mbili zimeshirikiana katika sekta mbalimbali ikiwemo ujenzi wa miundombinu, nishati, usafiri wa anga, afya, na elimu, ambayo imenufaisha watu wa pande zote mbili. Rais Hichilema amesema anatarajjia nchi hizo mbili zitaendelea kushirikiana katika siku zijazo, na kampuni nyingi zaidi za China zitawekeza nchini Zambia huku bidhaa nyingi zaidi za Zambia zikiingia kwenye soko la China.

Naye Balozi wa China nchini Zambia Du Xiaohui amesema, kukamilika kwa mradi huo kumeonyesha urafiki wa jadi kati ya nchi hizo mbili na ushirikiano mzuri kati ya China na Afrika, pia ni kielelezo cha moyo wa ushirkiano wa ujenzi wa TAZARA katika zama mpya. Mkutano wa kilele wa Umoja la Afrika utafanyika mwezi Julai nchini Zambia, na anatumai kuwa kituo hicho kitasaidia kuhimiza mshikamano wa bara zima la Afrika. Amesema kuwa China inapenda kushirikiana na nchi za Afrika katika kujenga mazingira yenye uhakika, amani na maendeleo kwenye dunia ya sasa iliyoko katika hali ya sintofahamu.

Kituo cha Mkutano cha Kimataifa cha Zambia kina ukubwa wa mita za mraba elfu 24, na kinajumuisha ukumbi mmoja wa mikutano unaoweza kuchukua watu 2,500, ukumbi mwingine wa watu 1,000 na vifaa mbalimbali husika.
1654065423043.png
 
Wanazidi kuongeza deni. Wachima watachukua mpaka wake zao
 
Back
Top Bottom