elivina shambuni
JF-Expert Member
- May 31, 2018
- 461
- 295
Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi alitembelea mradi wa ujenzi wa meli ya kisasa ambayo ni meli kubwa kuliko zote katika Ukanda wa Afrika Mashariki pamoja na ujenzi wa chelezo kwa ajili ya matengenezo na marekebisho ya meli mbalimbali ikiwa ni uwekezaji unaofanywa na Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
Aidha, Dkt. Abbasi aliongeza kuwa ujenzi wa meli mpya itakayokuwa na uwezo wa kubeba abiria 1, 200 umefikia asilimia 33 ya ujenzi na utakamilika mapema mwaka 2021, ambapo Serikali imewekeza zaidi ya TZS Bilioni 150, kwenye mradi ya meli pamoja na ujenzi wa chelezo.
Aidha, Dkt. Abbasi alishuhudia ukarabati unaoendelea katika meli ya MV. Victoria, ambayo baada ya kukamilika itasaidia kutoa huduma bora za usafiri kwenye eneo la Ziwa Victoria.
Vilevile, akiwa ziarani hapo Dkt. Abbasi alisema kuwa ipo miradi mingi kwenye eneo la Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika, inatakayo gharimu zaidi ya TZS Bilioni 300.
Aliongeza kuwa hivi karibuni, Serikali itasaini makubaliano ya utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa meli katika eneo la Ziwa Tanganyika na uundaji wa meli 3 mpya na za kisasa katika eneo la Ziwa Nyasa.
Akitaja, meli zilizokamilika kutokana na utekelezaji wa ahadi za Serikali hadi sasa kuwa ni meli za mbili za mizigo za MV. Ruvuma, na meli kubwa ya kisasa ya abiria ya MV. Mbeya II na ambayo tayari imeanza kazi.
Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli, Eric Hamissi, alisema kuwa ujenzi wa meli hiyo mpya unaendelea vizuri, na Septemba 30, mwaka huu vifaa mbalimbali kwa ajili ya ujenzi wa vilianza kuletwa na sasa kazi ya uunganishwaji wa vyuma imeshaanza.
Aliongeza kuwa, ujenzi wa chelezo umefikia 53%, na ifikapo Machi mwakani chelezo itanza kutumika kwa ajili ya ujenzi wa meli mpya.
Aidha, Bw. Hamissi alisema anaishukuru Serikali kwa ujenzi miradi hii miwili pamoja na ya ukarabariti wa MV. Butiama na MV. Victoria inayoendelea kwani itaigharimu Serikali TZS Bilioni 150, na hadi sasa Serikali imeshatoa TZS Bilioni 70.8, sawa na 47% ya miradi yote minne