Mramba alipokuwa SIDO pia waziri wa viwanda aliweza

Mramba alipokuwa SIDO pia waziri wa viwanda aliweza

MPadmire

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2006
Posts
3,957
Reaction score
3,245
Mh. Mramba alipokuwa Mkurugenzi wa Viwanda vidogo vidogo (SIDO) aliweza. Aliiongoza SIDO vizuri sana kuliko SIDO ya sasa ambayo haiwezi kusomesha wataalamu au kuwatumia wataalamu wa VETA. Pia Mramba aliweza kuendeleza vizuri Wizara ya Viwanda na Biashara.

Hapa Tanzania tuna matunda kibao, lakini nashangaa tunanunua juice ya matunda kutoka Kenya.

Kenya wana Kiwanda cha Kutengeneza Juice fresh za DEL MONTE. Hicho kiwanda cha DELMONTE Wanatoa juice za machungwa, maembe, mananasi n.k

Na watu wengi wanazipenda hizi juice kwa sababu ni juice halisi. sio juice za Machemicali.

Sasa mawaziri wa Tanzania kipindi hiki wanafanya nini? wapo wizarani kuchuma pesa na kujineemesha au wanafanya kazi gani. Wana uzalendo gani na nchi hii??
 
Inawezekana ni Hodari kwa Kazi ya utaalamu zaidi kuliko na kabla ya kuingia kwenye list ya mafisadi
 
Hata pale Mkuu Rombo alianzisha kiwanda cha kutengeneza vibiriti.......sasa hivi ni magofu........labda kama kimefufuliwa juzi...........
 
Jamaa alianzia NDC alikuwa kada mzuri na mwaminifu tuu . Mpaka pale alipozinduka naye akaanza. Huyo naweza kumwita Fisadi makini. Sema tu ukishakuwa fisadi bwana .....ah ushachafuka. Kajenga Kibo Palace pale Arusha alivyoona anafuatiliwa akaipiga bei kwa Uhuru Kenyatta. Jamaa infact yeye ameingia share kwenye baadhi ya makampuni kwa hiyo hayuko moja kwa moja kwenye umiliki na hutaweza kutrace pesa yake ni mjanja mno ndio maana namwita Fisadi Makini. Nani asiyependa pesa humu JF?
 
Back
Top Bottom