2019
JF-Expert Member
- Dec 31, 2018
- 3,130
- 4,735
Toka napata akili naskia sana neno Kilimanjaro, katika utafiti pia ni vitu vingi sana vina majina hayo. Toka niingie JF watu wanaotoka Kilimanjaro wanatajwa kwa ubaya kwa mazuri pia. Kutokana na mabishano ambayo nimeshuhudia kwenye majukwaa humu kuhusu wachaga na mkoa mzima nikatamani sana ipo siku nitaenda.
TRC warahisiha ndoto:
Nikakumbuka pia kuna usafiri unasifiwa sana kwa bei ndogo na uzuri wake. Nilikuwa free kama siku 7 hivi nikaamua wacha niende Kilimanjaro sina ndugu nitalala guest tu mpaka nione ukweli mana sio kwa misifa hiyo. Wachagga wamekuwa wakijitamba sana kwao kuzuri,makazi bora, nyumba nzuri,🦆 la kutosha hususa mwisho wa mwaka.
Nikachukua Deluxe yangu tar 30 ilikua j5 nauli 23,500 tu. Kwanza pongezi kwa JPM na pole kwa wanaobeza juhudi zake. Ila jamaa anapambana sana, anakosolewa sana kaskazini lakini kawapunguzia sana shida.
Sikuwahi kusafiri na treni umbali mrefu ila niliipenda safari. Nje mandhari nzuri ya kupendeza nchi yetu mradi wa SGR ulivyofikia n.k
Balaa linaanza kwenye treni: nilichoona kwenye treni unaweza kuhisi ndio sherehe au bata la mwaka mpya wenyewe. Watu wa pande zote TZ wamo sikujua kama labda nao wanaenda Moshi mwisho wa mwaka ama la. Watu wanajua kutumia pesa bana,full shangwe kujiachia unaweza kutamani kusikuche. Uzuri wa kwenye treni naamini unaweza kuamua kula mwisho wa mwaka huko tu kwa kusafiri na kurudi nalo.
Baada ya watu kujidunga ifaavyo(kupiga maji) mzozo ukatoke watu wakataka kushikana,kuna jamaa mmoja alikua anaongea lafudhi ya kisukuma alipandisha na madem flan hivi kama machotara. Ile watu kushika na kuita polisi cha kushangaza jamaa alijigamba hakuna mtu wa kumwambia lolote humo ndani. Alikuja polisi lakini jamaa alimdharau sana na kutaka kugombana nae ile dhana ya "unanijua mimi ni nani" yule jamaa aliitumia vizuri na yule polisi kuogopa kweli. Wengi walihisi labda ni usalama wa taifa.
Nafika Moshi saa 12 asubuhi mapema kabisa, stesheni kuna mishe mishe za hapa na pale lakini kwa muda huo maeneo mengine kumepoa.
Nilizunguka baadhi ya mitaa ili kuvuta muda.
Kulipokucha nikaacha kutembea sasa kwenda nje ya mji kidogo japo sikuzunguka wilaya zote ila nitaweka picha na maeneo niliyotembelea tu.
Nilitamani sana kwenda kupanda mlima lakini bajeti yangu haikuruhusu ukizingatia safari sikupanga mapema.
Stendi Moshi asubuhi, kusafi sana.
Karibu na chuo cha Mwenge kwa Dar ni kama Kijichi Mtoni hiyo mijengo.
Barabara ya kwenda Chuo cha Manyamapori Mweka.
Marangu
Kibosho
Maeneo ya Boro.
Ukweli ni kwamba japo hakuna gorofa nyingi, lakini sehemu za watu kuishi zimejengwa vizuri. Nyumba za matope niliona chache sana ila hakuna nyumba isiyo na njia.
Mtori mzuri sana Polisi mes, hii bakuli mpaka sijui inaitwaje(Wachagga mtanisaidia)
Redstone club maarufu na kubwa sana Moshi niliambiwa mwisho wa mwaka hujaa sana.
HITIMISHO: Nataka ikiwezekana nifanye utali wa ndani kila mwisho wa mwaka kwa kwenda mikoa tofauti kujionea mandhari za huko. Nikipata nauli ntaenda Dodoma mwaka huu mwishoni nikaone, ila Moshi ni pazuri japo sikumaliza mkoa mzima, nilitamani kupita kote bajeti yangu ikawa ndogo. Kongole kwa Wachagga, Wapare na Wasambaa mana ndio wengi wapo huko sana kujisifia kwenu sio bure nimeona angalau kidogo.