Mrejesho, Baada ya kuokota kipochi cha mzungu kilichokuwa na pete

Mrejesho, Baada ya kuokota kipochi cha mzungu kilichokuwa na pete

Chris wood

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2020
Posts
1,667
Reaction score
5,043
Kama ambavyo nilivyokuwa nimeleta bandiko, weekend wakati nilikuwa nikizunguka huku na kule, nilipita mahali nikakaa wakati naondoka niliokota kipochi kidogo ambacho ndani nilikuta kunapete 3.

Nilikuja kutaka ushauri humu ni jinsi gani na wapi ninaweza kuzipiga bei kwani zilikuwa zikionekana niza gharama, Bila matarajio nilikutana na maneno ya wadau humu kutaka nifanye utaratibu wa kumrudishia mwenye mali pete zake.

Jana asubuhi nilirudi mahali pale na kuacha taarifa, lakini jambo la kustaajabisha, nilikuta siku ile ile yule mama alirudi kuulizia pale, walimpigia simu nikamsubiri pale alivyofika nikamkabidhi pete zake.

Yule mama alitoa dola 100 akanipatia, akanipatia card ya mawasiliano akanishukuru sana kisha akaondoka.

20210808_072932.jpg

PIA, SOMA: - Mzungu kasahau kipochi chenye pete. Hivi zinaweza kuwa na thamani gani?
 
Na akakubatiza jina la kizungu kabisa?

Eti Chris Wood.

Hebu jipe jina la mti wowote wewe.

Chris Mbuyu, Chris Mpodo, Chris Mpingo.
Mimi ni shabiki ndaki ndaki wa huyo jamaa, mshambuliaji machachali wa bunley
 
Hongera. Sasa, mimi ninaongezea hapa kidogo. Ni ngumu kwa waTZ lakini hatunabudi kubadilika. Tukijikuta kwenye hali kama hii, yani KUMSAIDIA mtu kwa kumrejeshea mali zake, aliyepata ajali, n.k, kama kweli lengo ni uungwana na kutenda haki, basi tusiwe na mawazo ya kupewa zawadi ya aina yoyote.

Zawadi ijitokeze kama ziada tu. Ukiwaza sana, unaweza hata kuikataa kama inafaa. Mara nyingi mimi nikijikuta kwenye matukio kama haya,ninawaza sana pindi kilichomtokea mwenzangu kitanikuta. Yani huw aninajiweka nafasi ya mhusika.Tubadilike
 
Huu ndiyo uungwana. Tunatakiwa kuheshimu mali za wengine.

Mimi wiki iliyopita kwenye train pia miliokota simu moja matata sana ya Samsung, nilivyofika kwenye kituo changu cha kushukia, niliichukua ile simu na kuipeleka kwenye ofisi za shirika la reli.

Wana kitengo cha lost and found.

Tuendelee kujifunza uaminifu.
 
Mawasiliano aliokuachia usimtafute Leo Wala kesho Kama n namba ya simu yakwao sio ya bongo hapo tengeneza connection lakibabe mpe hata mwez Kama unakiraruraru Basi after two weeks msalimie.

Ongea nae connection za pesa huwez just huko kwao wapo vip naamini unabusara hvyo utanzania(Africa) hautauonyesha hapo.

Mpe dili akukusanyie makorokoro mpaki kwenye container mpige pesa
 
sio wazungu wa sku hzi ndugu..😁
 
Hongera. Sasa, mimi ninaongezea hapa kidogo. Ni ngumu kwa waTZ lakini hatunabudi kubadilika. Tukijikuta kwenye hali kama hii, yani KUMSAIDIA mtu kwa kumrejeshea mali zake, aliyepata ajali, n.k, kama kweli lengo ni uungwana na kutenda haki, basi tusiwe na mawazo ya kupewa zawadi ya aina yoyote.

Zawadi ijitokeze kama ziada tu. Ukiwaza sana, unaweza hata kuikataa kama inafaa. Mara nyingi mimi nikijikuta kwenye matukio kama haya,ninawaza sana pindi kilichomtokea mwenzangu kitanikuta. Yani huw aninajiweka nafasi ya mhusika.Tubadilike
Umeandika vizuri sana ndugu. Ila ukosefu wa pesa ndio unasababisha hayo yote
 
Mungu Mkuu, sasa mimi nilitoa ushauri mzuri uliotukuka na wenye nanufaa makubwa kwako na kwangu nikiwa mshauri mzuri na mwenye hekima.

Wacha Mungu aitwe Mungu.

Naomba mgao wangu angalau robo ya hiyo endapo itakupendeza.
 
Back
Top Bottom