Mrejesho, Baada ya kuokota kipochi cha mzungu kilichokuwa na pete

Mrejesho, Baada ya kuokota kipochi cha mzungu kilichokuwa na pete

Feel sad

Na kweli wajuzi walisema utajutia kama amekupa 100 usd inaonyesha wazi thamani zake zilikuwa 100,000 usd hapo ni mill 240 zakitanzania da
 
Hizo Pete haikua mali yake,acha tamaa mkuu,riziki anatoa Mungu na nina imani atamlipa zaidi ya thamani ya hizo Pete,uaminifu unalipa.
Mungu ndo alimjalia huenda mzungu anaenda kumvisha lesbian au msagaji mwenzake Kweli jamaa amekuja JUHA amgempa Ile ya tatu mbaya mbaya
 
Mungu ndo alimjalia huenda mzungu anaenda kumvisha lesbian au msagaji mwenzake Kweli jamaa amekuja JUHA amgempa Ile ya tatu mbaya mbaya
Mungu alikua anampima imani yake,hayo ya kusema "huenda..." huo ni utabiri wako na hauna ithbati yeyote,siku ukija kupoteza kitu chako cha thamani ndio utajua thamani ya uaminifu.
 
Chris, naona kama umesahau vile au kazi zimekutinga, samahani kwa usumbufu ila baadae ninasafiri kwenda Moshi, nikirudi nitakuletea mbege.
Nakumbushia kamgao kangu kwa ushauri uliotukuka.
 
Mawasiliano aliokuachia usimtafute Leo Wala kesho Kama n namba ya simu yakwao sio ya bongo hapo tengeneza connection lakibabe mpe hata mwez Kama unakiraruraru Basi after two weeks msalimie.

Ongea nae connection za pesa huwez just huko kwao wapo vip naamini unabusara hvyo utanzania(Africa) hautauonyesha hapo.

Mpe dili akukusanyie makorokoro mpaki kwenye container mpige pesa
Sio kila mzungu ana hela nimeishi nje miaka zaidi ya mitano wengi chokesti
 
Hiyo kadi ya mawasiliano haina maana sana kwako kwa sababu kutema yai tu hata la kumwitia mbwa ni mtihani, labda utafute mkalimani au muwasiliane kwa njia ya ishara......chukua hiyo 100 tambaa.
 
Umeandika vizuri sana ndugu. Ila ukosefu wa pesa ndio unasababisha hayo yote
Asante. Huwezi amini, hii ni tabia tu,wala si ukosefu wa pesa au umasikini. Utaona tabia hii inakua kadiri tunavyosonga mbele. Kadiri ukirudisha miaka nyuma,utaona kiwango cha utu kinaongezeka, na kadiri jamii inavyosonga mbele ndivyo utu na uungwana hupungua. Hivyo, ni malezi kijamii. Hapo utashangaa kuna watz wengi wanakuona wa ajabu,mshamba,boya n.k., ukimrudishia mwenye chake.

Basi tunatekwa na falsafa hii na kujikuta tunapoteza utu. Hufikirii kesho kwako itakuwaje. Hujawahi kuona mtz awe bosi au mfanyakazi wa kawaida, awe ana fursa ama hana, ukienda kwake unakuta mapazia ya ofisini, sahani za ofisini, n.k. Unajiuliza, huyu mtu hana pesa za kununua sahani ama mapazia? Hata kwenye visherehe vyetu vya harusi, unakuta mtu (mwanakamati) hana njaa yoyote,lakini akipiga hata 50,000 anajiona mjaanja. Ni tabia tu.

Kuna miaka fulani kipindi hicho ninasikiliza redio. Redio Zanzibar ilikuwa na utaratibu muda fulani panatangazwa vitu vilivyopotea na mahali pa kuvipata. Sina hakika kama bado hii kitu ipo huko. Aidha, Somalia, si taifa moja. Zipo Somalia kama mbili ama tatu hivi(sina hakika sana).

Sasa kuna Somalia moja ina utulivu, si hii tunayoijua ya Elshabaab. Ni ka nchi fulani hivi masikini lakini kako peace kishenzi. Eti muda wa kuswali(wengi wao ni waislamu), mtu anaefanya bishara ya kubadilisha fedha (mara nyingi wapo sokoni tu na meza zao), wanaacha pesa kama nyanya juu ya meza wanaenda kuswali msikitini. Hebu fikiria kitu kama hiki.

TABIA HUTENGENEZWA
 
Mkuu kama huna passport kata kabisa itege, viza ipo njiani L.A, Stockholm, Copenhagen sijui Rosenborg utawasalimia
 
Kawaida kwa watu waliostaarabika.

Kuna siku nimetoka safari zangu huko naenda huku katika panda shuka na mabasi nirudi nyumbani hamad nashtuka niko mwepesi kucheck hivi walet halipo na bus lile linaondoka.

Nililikimbilia mpaka likapotea wapi.

Nikakata tamaa narudi kwangu sina mia.

Ndani ya walet kulikua vizuri euro na dola za kutosha acha vitambulisho leseni kila kitu.

Kwa kawaida yetu angepata mswahili ile hupati.

Nilipigiwa simu nikaenda nikapewa wallet nzima nzima km nilivyoiacha.

Sikudhani kukuta hela ila niliikuta vilevile.

Aisee uaminifu mzuri sana.

Siku ingine simu jamaa akatuma email akanipa.

Toka hapo.

Na mimi narudisha chochote nnachoona
 
Hongera Kaka mm nilikushauri urudi pale pale na bahati nzuri umeona matokeo yake .Wewe kwelin ni muungwana nimependa ulivofanya safi kabisa na hiyo ndio rizki yako tmia kwa mahitaji yako muhimu inaweza ikakutoa kama ni mtu wa biashara kama umekwenda kula bata basi hata lisaa halifiki unarudi kuleee ulikotokaa laki mbili na thelathini unaweza kuzungushia hata kununua nazi kwa jumla shamabi na kuleta sokoni ukauuza reja reja ndio mpango mzima.
 
Back
Top Bottom