Umeandika vizuri sana ndugu. Ila ukosefu wa pesa ndio unasababisha hayo yote
Asante. Huwezi amini, hii ni tabia tu,wala si ukosefu wa pesa au umasikini. Utaona tabia hii inakua kadiri tunavyosonga mbele. Kadiri ukirudisha miaka nyuma,utaona kiwango cha utu kinaongezeka, na kadiri jamii inavyosonga mbele ndivyo utu na uungwana hupungua. Hivyo, ni malezi kijamii. Hapo utashangaa kuna watz wengi wanakuona wa ajabu,mshamba,boya n.k., ukimrudishia mwenye chake.
Basi tunatekwa na falsafa hii na kujikuta tunapoteza utu. Hufikirii kesho kwako itakuwaje. Hujawahi kuona mtz awe bosi au mfanyakazi wa kawaida, awe ana fursa ama hana, ukienda kwake unakuta mapazia ya ofisini, sahani za ofisini, n.k. Unajiuliza, huyu mtu hana pesa za kununua sahani ama mapazia? Hata kwenye visherehe vyetu vya harusi, unakuta mtu (mwanakamati) hana njaa yoyote,lakini akipiga hata 50,000 anajiona mjaanja. Ni tabia tu.
Kuna miaka fulani kipindi hicho ninasikiliza redio. Redio Zanzibar ilikuwa na utaratibu muda fulani panatangazwa vitu vilivyopotea na mahali pa kuvipata. Sina hakika kama bado hii kitu ipo huko. Aidha, Somalia, si taifa moja. Zipo Somalia kama mbili ama tatu hivi(sina hakika sana).
Sasa kuna Somalia moja ina utulivu, si hii tunayoijua ya Elshabaab. Ni ka nchi fulani hivi masikini lakini kako peace kishenzi. Eti muda wa kuswali(wengi wao ni waislamu), mtu anaefanya bishara ya kubadilisha fedha (mara nyingi wapo sokoni tu na meza zao), wanaacha pesa kama nyanya juu ya meza wanaenda kuswali msikitini. Hebu fikiria kitu kama hiki.
TABIA HUTENGENEZWA