Mrejesho: Baada ya kupitia msoto mkali wa bei kali za vifurushi vya data, nimehamia na kutulia Tigo post paid, nimepunguza gharama zaidi ya maradufu

Mrejesho: Baada ya kupitia msoto mkali wa bei kali za vifurushi vya data, nimehamia na kutulia Tigo post paid, nimepunguza gharama zaidi ya maradufu

NetMaster

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2022
Posts
1,454
Reaction score
4,925
Mabando haya ghali yaliniumiza sana hasa nikiwa mtu mwenye kipato cha kawaida, Vuta picha tu kwamba MB 900 hazijafika hata GB ni elf 2 halafu umetumia nusu saa tu unapokea sms "umetumia asilimia 75%...." 😬 , nilikuwa najikuta, nilikwangua sana vocha.

Ndipo nilipoweza kupata suluhisho.

Ni miezi mitatu sasa nina enjoy internet bila stress kwa bei chee, mabando hayaniumizi tena kichwa wala kunivurugia bajeti, 😁.

KUHUSU POSTPAID

Muhimu: Nime update post haya ni mabando mapya kwa wateja wapya, Kwa sisi tuliojisali mwanzoni mabadilko hayatuhusu.

1691686870276.png



FqJFRoaWAAEyIy9.jpg

Postpaid ni malipo baada ya matumizi, unatumia sasa unalipa baada ya matumizi, ni tofauti na vifurushi tulivyovizoea vinavyoitwa prepaid tunailipia kabla.

Kujisajili postpaid inabidi uende ofisi za tigo ukiwa na tin namba, na kitambulisho cha kupiga kura, Nida, udereva, n.k. (Kama huna Tin mbadala ni kutumia hawa wanaosajili lain mtaani wapo wenye connection ila inabidi uwape ya maji)

Siku unayosajiliwa utalipia pesa kulingana na kifurushi, Mfano ukitaka kusajiliwa bando la elf 15 lenye GB 15, itabidi ulipe elf 15, hii hela inaitwa security fee.

Kila mwezi mpya ukifika ile saa sita usiku unaungwa upya, mfano bando la Gb 15 ikifika saa sita zinaingia upya GB 15.

Muda wa malipo ni tarehe 1 hadi tarehe 10, ukichelewa kulipa laini inafungwa, itafunguliwa hadi ulipe deni. haimaanishi kwamba huwezi kutumia bando jipya mpaka ulipie, Hapana! bando utaendelea kulitumia bila kizuizi ila hakikisha unafanya malipo ndani ya muda.

Bando la kwanza unaposajiliwa utapimiwa kulingana na siku zilizobaki, mfano ukisajiliwa tarehe 11 kwenye mwezi wenye siku 30 hapo zimebaki siku 20, kwa kifurushi cha gb 15 utapewa bando la siku 20 sawa na GB 10 ( siku20/siku30 x gb 15), mwezi mpya ukifika utadaiwa bando la siku 20 sawa na elf 10 (siku 20/siku30 x 15,000) ulipie ndani ya tarehe 1 hadi 10, baada ya hapo utakua unapewa kifurushi kamili na kulipia kiasi kamili. hata ukijisajili tarehe 30 utapimiwa bando la siku 1 ila ikifika tarehe 1 utapewa bando kamili, Kesho yake tarehe 1 ya mwezi mpya utadaiwa bando la siku 1, malipo ni tarehe 1 hadi tarehe 10.


NETWORK

Kabla hujajiunga hakikisha maeneo yako yana network ya tigo, tumia line yoyote ya tigo kupima kama network inakamata, usije fanya kosa la kusajili bila kutesti mitambo.

Kama maeneo network ni changamoto inabidi ununue pocket router kifaa kidogo tu kina uwezo mkubwa wa kukusanya network kuzidi simu, unaichaji unaweka dirishani ama juu ya mlango, zipo tigo zinauzwa.
 
Inapendeza kama upo located mahali kuna covarage nzuri, mnara haupo overloaded na watu kiasi cha kupunguza bandwidth

Wenye kujua kama Konnect internet ipo reliable au lah
 
Mabando haya ghali yaliniumiza sana hasa nikiwa mtu mwenye kipato vya kawaida, Just imagine MB 500 ni buku alafu hata hujatumia dakika 10 unapokea sms "umetumia asilimia 75%...." 😬 Daaaah!! Yaani unaweza jikuta unaunga hilo bando zaidi ya mara 4 kwa siku,

Tukija kwenye vpn nako ni maumivu tu, siku yoyote inafungiwa hakuna uhakika, unakuta mtandao unakubali vpn ila unaweza kutumia mb 300 tu kwa siku, vpn zinamaliza sana chaji, vpn unakuta haipo stable inakata kata inabidi uwe unaizima na kuiwasha kila baada ya dakika kadhaa, unakuta speed ya vpn ni slow kama konokono, kuwasha hotspot ili utumie wifi mpaka uweke apps za ziada na zinatumia sana chaji, vpn nyingine inakubali kutumika asubuhi tu, matapeli wa vpn nao washaona fursa yani ukijiroga kuwatumia hela ya vpn unaambulia block ama kutumiwa vpn mdebwedo zenye matatizo niliyotaja, masnich nao hawapo mbali wakiona mnafaidi mbinu mpya ya vpn wao wanaenda kuwachoma wazi wazi kwenye comments za page za mitandao ya simu, just imagine!! šŸ˜‚šŸ˜‚.. Shida zote za nini hizi ?? Mi nimeamua nilipie tu kihalali nipate huduma kwa uhakika kwa bei chee...

yapata miezi mitatu nina enjoy internet bila stress kwa bei chee, mabando hayaniumizi tena kichwa wala kunivurugia bajeti, Nilikuwa wapiiii (kwa sauti ya Manara 😁😁)...

Mizigo hii ipo kama ifuatavyo, kwa hesabu nilizopiga Gb 1 haizidi shilingi 850, unateleza mwezi mzima.

25,000 - Gb 30
40,000 - GB 50
50,000 - GB 65
60,000 - GB 80
75,000 - GB 100

Ni halali kabisa wala sio mabando ya mchongo, Hii ni TIGO POSTPAID... ni mwezi wa tatu huu natumia kifurushi mojawapo na kiukweli ni ahueni mpaka huwa najilaumu niilikuwa wapi muda wote huu aisee, laiti ningejua mapema ningekuwa nimeokoa gharama kibao yani.

KUHUSU POSTPAID

Postpaid ni malipo baada ya matumizi, ni tofauti na prepaid tunazolipia kwanza ili tupewe huduma.

Hii postpaid ni kwamba kila tarehe 1 ikifika unaungwa upya automatically kifurushi ulichochagua, Bili yako utakuwa unalipia mwezi unaofata katika dirisha la siku 12 kuanzia tarehe 1 hadi 12,

USAJILI

Kujisajili utasaini mkataba na tigo kukubali kufanya malipo kila mwezi kwa mwaka mzima, Utalipia kishika uchumba wanachokiita "security fee" kwa gharama sawa na kifurushi utachochagua, mfano kwa mkataba wa gb 30 kila mwezi utalipia security fee elf 25, unapojisajili hutalipia chochote zaidi ya security fee, malipo ya bando utaloungwa utalipia mwezi ujao katika dirisha la siku 12 za mwanzo.

MALIPO YA BANDO LA KWANZA

bando la kwanza utalopewa unapojisajili utapimiwa kulingana na siku za matumizi zilizobaki kwenye mwezi, mfano kwa mwezi wenye siku 30, ukienda kujiunga tarehe 11 hapa ni kwamba kuanzia tarehe hio hadi tarehe 30 zimebaki siku 20, mfano kwa kifurushi cha elf 25 kwa gb 30 hapa utapewa GB 20 ( 20/30 * gb 30),,, bili yako itapigiwa hesabu kuwa shilingi 16,666 (20/30 * elf 30) ambayo utalipa mwezi ujao kwa zile siku 12 za mwanzo... Miezi inayofata utakua unapewa gb 30 na kulipia elf 25.

KURUDISHIWA SECURITY FEE

Security fee utarudishiwa pesa taslimu cash endapo ukiweza kutimiza malipo ya kila mwezi kwa mwaka mzima,,

UKICHELEWESHA MALIPO

ikifika tarehe 13 bado hujalipia watafungia laini zako za tigo, kufungua laini ni mpaka uende tigo ulipe deni ndio zitafunguliwa lakini security fee hutarudishiwa, toa taarifa mapema kusimamisha mkataba ili kupunguza deni, usipotoa taarifa mapema na ikafika tarehe 1 system yao ikiunga bando lengine deni linazidi.

NETWORK

Kabla hujajiunga hakikisha maeneo unayoshinda yana mtandao, tumia line ya kawaida ya tigo weka kifurushi hata cha siku kujiridhisha kama internet yao ipo stable, ubora utaoupata ndio huo huo utaupata ukijisajili postpaid, usije fanya kosa la kusajili bila kufanya research.

KIFURUSHI GANI KIZURI.

Kwa ushauri chagua kifurushi ambacho kipato chako kinaweza kukimudu kwa uhakika kila mwezi maana ukichelewesha malipo hurudishiwi security fee na ukitaka kujiunga tena inabidi ulipe madeni unayodaiwa kwenye mkataba uliopita na utalipia upya kishika uchumba kwenye mkataba mpya.

CHANGAMOTO.

Wala siwezi kuwaficha hapa, huu mtandao wa tigo ikifika saa mbili na nusu usiku hadi saa tano speed huwa inashuka na hii sio kwa postpaid pekee, ni kwa wateja wote mtandao unasumbua mida hii.... muda huu labda uwe unafanya browsing ya kawaida, kuchati au kucheki picha, tofauti na hapo utapata taabu kucheki video, kupiga video call, kudownload mafaili, n.k

MBADALA

Kuna postpaid ya voda inaitwa supakasi maalum kwa majumbani ama maofisini, wanakufungia antenna nyumbani au ofisini kwako, malipo utalipa kwa speed na si kwa GB, Vifurushi vyao kuna cha speed ya MB 1.25 kwa sekunde kwa shilingi 115,000 na kingine ni speed ya MB 2.5 kwa sekunde kwa shilingi 165,000 .... Kishika uchumba chao (security fee) ni gharama ya kifurushi ulichochagua kwa miezi miwili na kinarudi ukikamilisha mkataba kikamilifu, Huduma hii hupatikana zaidi kwenye minara ya mjini karibu kila mkoa, ingia google usechi supakasi utaona orodha kamili ya miji inayo support hii huduma.

..........................................

Yote kwa yote hii huduma ni nzuri inaokoa sana hasa kwa wale ambao vifurushi vya wiki wanaunga kila baada ya siku mbili šŸ˜‚
Nipo na hiyo huduma kwa mwezi wa pili sasa, kwanza huduma iko poa, pili hawaibi bando kama vifurushi vya kawaida. Natumia kile elfu 25 napata zangu GB 30
 
MBADALA

NB: 1 Mbps (megabits kwa sekunde) ni sawa na 0.125 MBps (Megabytes kwa sekunde), Mb ni tofauti na MB yenye herufi kubwa tuliyozoea wengi, ndio hizi tunatumia tunapodownload muvi, miziki, n.k. Hivyo ukiona speed ni 10 Mbps herufi ndogo zidisha na 0.125 unapata MB 1..25 kwa sekunde, hapa unaweza kushusha file la MB 1 kwa sekunde, usije changanya

A. Kuna postpaid ya voda inaitwa supakasi maalum kwa majumbani ama maofisini, wanakufungia antenna nyumbani au ofisini kwako, malipo utalipa kwa speed na si kwa GB, Vifurushi vyao kuna cha speed ya 10 Mbps kwa sekunde kwa shilingi 115,000 na kingine ni speed ya 20 Mbps kwa sekunde kwa shilingi 165,000 .... Kishika uchumba chao (security fee) ni gharama ya kifurushi ulichochagua kwa miezi miwili na kinarudi ukikamilisha mkataba kikamilifu, Huduma hii hupatikana zaidi kwenye minara ya mjini, kuona orodha kamili ya miji inayo support hii huduma ingia >> hapa <<

B. Kama upo eneo lenye nguzo za ttcl na nyaya zile za simu zipo, nenda ttcl uongee na fundi mwambie unataka huduma ya ADSL, kwenye miji midogo mfano kama Mafinga huduma hii ni ubakika maana mji ni mdogo hata nguzo ni chache na ikitokea imeanguka ni rahisi kurekebisha, pia ule uhuni wa miji na majiji makubwa ya wezi hasa mateja kuiba cable haukufika miji midogo, mziki upo miji mikubwa yenye nguzo kibao, kuna mitaa nguzo zipo ila hakuna nyaya kwa miaka, wahuni waliiba na kwenda kuziuza, pia kwavile miji ni mikubwa na nguzo ni kibao basi haya matatizo ya nguzo kupinda au kudondoka ni kawaida, hadi ttcl waje kutengeneza ni panapo majaliwa, kama upo miji mikubwa inapendeza uwe maeneo ya kati / centre kwenye ofisi nyingi za serikali zinazotumia simu za ttcl.

Mahitaji, utanunua router ya elf 55 ofisini kwao watakuja kukuwekea, Malipo ni elf 25 kila mwezi na speed ni 4 Mbps kwa sekunde bila kikomo, vifurushi zaidi cheki >> hapa <<

View attachment 2376428

C. Maeneo mengi ya centre kwenye majiji ttcl wamepitisha fiber, kwenye nguzo zao kuna waya wa ziada mnene ukichana na ule mwembamba wa simu za mezani ambao nao pia nimeelezea namna ya kupata internet yake, kama upo eneo lenye nyaya hizi za fibre nenda kawacheki wakuwekee, malipo ni elf 55 kila mwezi una enjoy speed nzuri kabisa 20 Mbps kwa sekunde, vifurushi zaidi cheki >> hapa <<
 
Ila internet ya Tigo daah, au basi tu.
Ndio maana nimekuwa muwazi sijaificha hii changamoto, yani mida hii kuanzia saa mbili hadi saa tano usiku hata mzuka wa kutumia net unakakata, speed ni kobe,
 
Back
Top Bottom