Mrejesho: Baada ya kupitia msoto mkali wa bei kali za vifurushi vya data, nimehamia na kutulia Tigo post paid, nimepunguza gharama zaidi ya maradufu

NetMaster

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2022
Posts
1,454
Reaction score
4,925
Mabando haya ghali yaliniumiza sana hasa nikiwa mtu mwenye kipato cha kawaida, Vuta picha tu kwamba MB 900 hazijafika hata GB ni elf 2 halafu umetumia nusu saa tu unapokea sms "umetumia asilimia 75%...." 😬 , nilikuwa najikuta, nilikwangua sana vocha.

Ndipo nilipoweza kupata suluhisho.

Ni miezi mitatu sasa nina enjoy internet bila stress kwa bei chee, mabando hayaniumizi tena kichwa wala kunivurugia bajeti, 😁.

KUHUSU POSTPAID

Muhimu: Nime update post haya ni mabando mapya kwa wateja wapya, Kwa sisi tuliojisali mwanzoni mabadilko hayatuhusu.





Postpaid ni malipo baada ya matumizi, unatumia sasa unalipa baada ya matumizi, ni tofauti na vifurushi tulivyovizoea vinavyoitwa prepaid tunailipia kabla.

Kujisajili postpaid inabidi uende ofisi za tigo ukiwa na tin namba, na kitambulisho cha kupiga kura, Nida, udereva, n.k. (Kama huna Tin mbadala ni kutumia hawa wanaosajili lain mtaani wapo wenye connection ila inabidi uwape ya maji)

Siku unayosajiliwa utalipia pesa kulingana na kifurushi, Mfano ukitaka kusajiliwa bando la elf 15 lenye GB 15, itabidi ulipe elf 15, hii hela inaitwa security fee.

Kila mwezi mpya ukifika ile saa sita usiku unaungwa upya, mfano bando la Gb 15 ikifika saa sita zinaingia upya GB 15.

Muda wa malipo ni tarehe 1 hadi tarehe 10, ukichelewa kulipa laini inafungwa, itafunguliwa hadi ulipe deni. haimaanishi kwamba huwezi kutumia bando jipya mpaka ulipie, Hapana! bando utaendelea kulitumia bila kizuizi ila hakikisha unafanya malipo ndani ya muda.

Bando la kwanza unaposajiliwa utapimiwa kulingana na siku zilizobaki, mfano ukisajiliwa tarehe 11 kwenye mwezi wenye siku 30 hapo zimebaki siku 20, kwa kifurushi cha gb 15 utapewa bando la siku 20 sawa na GB 10 ( siku20/siku30 x gb 15), mwezi mpya ukifika utadaiwa bando la siku 20 sawa na elf 10 (siku 20/siku30 x 15,000) ulipie ndani ya tarehe 1 hadi 10, baada ya hapo utakua unapewa kifurushi kamili na kulipia kiasi kamili. hata ukijisajili tarehe 30 utapimiwa bando la siku 1 ila ikifika tarehe 1 utapewa bando kamili, Kesho yake tarehe 1 ya mwezi mpya utadaiwa bando la siku 1, malipo ni tarehe 1 hadi tarehe 10.


NETWORK

Kabla hujajiunga hakikisha maeneo yako yana network ya tigo, tumia line yoyote ya tigo kupima kama network inakamata, usije fanya kosa la kusajili bila kutesti mitambo.

Kama maeneo network ni changamoto inabidi ununue pocket router kifaa kidogo tu kina uwezo mkubwa wa kukusanya network kuzidi simu, unaichaji unaweka dirishani ama juu ya mlango, zipo tigo zinauzwa.
 
Inapendeza kama upo located mahali kuna covarage nzuri, mnara haupo overloaded na watu kiasi cha kupunguza bandwidth

Wenye kujua kama Konnect internet ipo reliable au lah
 
Nipo na hiyo huduma kwa mwezi wa pili sasa, kwanza huduma iko poa, pili hawaibi bando kama vifurushi vya kawaida. Natumia kile elfu 25 napata zangu GB 30
 
MBADALA

NB: 1 Mbps (megabits kwa sekunde) ni sawa na 0.125 MBps (Megabytes kwa sekunde), Mb ni tofauti na MB yenye herufi kubwa tuliyozoea wengi, ndio hizi tunatumia tunapodownload muvi, miziki, n.k. Hivyo ukiona speed ni 10 Mbps herufi ndogo zidisha na 0.125 unapata MB 1..25 kwa sekunde, hapa unaweza kushusha file la MB 1 kwa sekunde, usije changanya

A. Kuna postpaid ya voda inaitwa supakasi maalum kwa majumbani ama maofisini, wanakufungia antenna nyumbani au ofisini kwako, malipo utalipa kwa speed na si kwa GB, Vifurushi vyao kuna cha speed ya 10 Mbps kwa sekunde kwa shilingi 115,000 na kingine ni speed ya 20 Mbps kwa sekunde kwa shilingi 165,000 .... Kishika uchumba chao (security fee) ni gharama ya kifurushi ulichochagua kwa miezi miwili na kinarudi ukikamilisha mkataba kikamilifu, Huduma hii hupatikana zaidi kwenye minara ya mjini, kuona orodha kamili ya miji inayo support hii huduma ingia >> hapa <<

B. Kama upo eneo lenye nguzo za ttcl na nyaya zile za simu zipo, nenda ttcl uongee na fundi mwambie unataka huduma ya ADSL, kwenye miji midogo mfano kama Mafinga huduma hii ni ubakika maana mji ni mdogo hata nguzo ni chache na ikitokea imeanguka ni rahisi kurekebisha, pia ule uhuni wa miji na majiji makubwa ya wezi hasa mateja kuiba cable haukufika miji midogo, mziki upo miji mikubwa yenye nguzo kibao, kuna mitaa nguzo zipo ila hakuna nyaya kwa miaka, wahuni waliiba na kwenda kuziuza, pia kwavile miji ni mikubwa na nguzo ni kibao basi haya matatizo ya nguzo kupinda au kudondoka ni kawaida, hadi ttcl waje kutengeneza ni panapo majaliwa, kama upo miji mikubwa inapendeza uwe maeneo ya kati / centre kwenye ofisi nyingi za serikali zinazotumia simu za ttcl.

Mahitaji, utanunua router ya elf 55 ofisini kwao watakuja kukuwekea, Malipo ni elf 25 kila mwezi na speed ni 4 Mbps kwa sekunde bila kikomo, vifurushi zaidi cheki >> hapa <<

View attachment 2376428

C. Maeneo mengi ya centre kwenye majiji ttcl wamepitisha fiber, kwenye nguzo zao kuna waya wa ziada mnene ukichana na ule mwembamba wa simu za mezani ambao nao pia nimeelezea namna ya kupata internet yake, kama upo eneo lenye nyaya hizi za fibre nenda kawacheki wakuwekee, malipo ni elf 55 kila mwezi una enjoy speed nzuri kabisa 20 Mbps kwa sekunde, vifurushi zaidi cheki >> hapa <<
 
Ila internet ya Tigo daah, au basi tu.
 
Ila internet ya Tigo daah, au basi tu.
Ndio maana nimekuwa muwazi sijaificha hii changamoto, yani mida hii kuanzia saa mbili hadi saa tano usiku hata mzuka wa kutumia net unakakata, speed ni kobe,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…