mcrounmj
JF-Expert Member
- Feb 26, 2016
- 380
- 889
Panapo majaaliwa ya mwenyezi Mungu tumekutana tena kwenye kikao cha wapambanaji. Wakuu wa jukwaa hili hususani vijana nawasalimu kwa Salam adhimu ya mama yetu Samia Suluhu Hassan......
Bila kuwachosha ni kuwa tangu nimeianza safari yangu ya kibiashara nimekuwa nikiwashirikisha hatua ninazopitia, ups and downs na Mambo lukuki. Nikiri tu kuwa kufanya biashara na ikakua siyo kitu kidogo. Inahitaji uvumilivu, umakini na bidii.
Mwaka Jana 2020 June nilikuja kwenye jukwaa hili kuomba ushauri juu ya kuanzisha biashara ya madini ya dhahabu. Watu wengi walinishauri, walinitia moyo na kunikatisha tamaa pia. Nilifanikiwa kukata leseni na vibali vingine na kuanza biashara kama blocker. Pamoja kuwa na mtaji mdogo yaani mpaka napata vibali ilikuwa imebaki milioni nne tu na changamoto nyingine lakini kutokea June nianze biashara hadi December nilikuwa nimefikisha milioni kumi na upuuzi (ndani ya miezi sita).
Nimeianza January ya mwaka huu na moto zaidi, kwanza nikiwa na uzoefu wa kutosha na pili nikiwa nimeshapata connection na watu tofautitofauti.
Malengo yangu ilikuwa mpaka kufika June ya mwaka huu kuanzia January niwe na zaidi ya milioni ishirini na hapo ninunue karasha nianze kukuza mlima na biashara ya dhahabu nikiendelea nayo.
To be honest guys, malengo yamefika kabla ya muda. Ninachokisubiri ni kwenda kuchonga karasha tu niwe na mwalo wangu. Tangu nimeianza biashara hii Sasa naenda kukamilisha mwaka mmoja this June. Vivyo kwa ukuaji wa kiwango hicho naona kama ushindi mkubwa mno kwangu.
Nimeandika na nimekuwa nikiandika my ways to success ili ku share na vijana wenzangu kwa sababu naamini njia niliyopita kufika hapa lipo kundi kubwa la vijana wanapita na pengine wanahisi wamepotea. Mimi ni mhanga wa wahitimu wa chuo kikuuu waliokosa ajira. Niliamua kupambana na umasikini nikifanya vibarua vyote vya halali nikikusanya vipande vya sarafu ili nipate mtaji.
Changamoto ni nyingi mno. Ni lazima ujifunze kuzipunguza zenye kupunguzika, ubalansi matumizi yako na biashara. Katika kipindi cha mwaka mzima kuna muda nimeanguka, nimetapeliwa zaidi ya milioni mbili kwa siku moja, zipo siku nimenunua mzigo kwenye kuuza ulikata zaidi ya milioni mbili, n.k n.k...
Cha mwisho ni kwamba vijana tusibaki kulalamika kwa kuilaumu serikali kushindwa kutuajiri, bali tuziibue fursa na kisha tuidai serikali ijenge mazingira rafiki katika kukuza biashara zetu. Wanajukwaa hususani vijana, giza ni nene safari ni ndefu lakini tutatoboa.
#kikaochawapambanaji