Nitakujibu kwa majibu marefu kidogo, kuwa mvumilivu, tiririka nami.
Majibu haya ni kwa mujibu wa my personal experience (nimezaliwa na kukulia katika moj ya maeneo ya uchimbaji wa madini ya dhahabu nchini Tanzania)
Hivyo kunaweza kuwa na mabadiliko kidogo katika hoja zangu kulingana na hali ilivyo katika maeneo yenye madini nchini.
Tutazame kwanza mabadiliko ya trends za teknolojia za kupata dhahabu na nyakati zake.
1. Kuokota dhahabu maeneo mbalimbali (kwenye surface land) hasa ya maeneo ya mitoni, n.k :
Hizi ni zama za zamani sana, hasa kabla ya uhuru na kabla ya kuja watu weupe barani Afrika. Kama umeshawahi kusikia kwamba zamani dhahabu zilikua zinatumika kama "kete" za kuchezea bao. It was that simple, that abundant.
2. Kuchimba ili kupata "mchanga wa dhahabu" na kuosha ili kuipata dhahabu yenyewe (kusekesa/kuchekecha, kupiga kalai):
Hapa kilichokua kinatafutwa ni "mchanga wa dhahabu", na hatimaye unaoshwa kwa njia nilizotaja hapo juu ili kupata madini ya dhahabu. Ni njia ambayo inahitaji maji na kinachopatikana hapa tunaweza kusema ni "pure gold".
3. Kuchimba mashimo marefu (long bases) ili kutafuta MIAMBA inayoambatana na dhahabu:
Katika njia hii miamba hiyo hulainishwa (kuwa mawe madogo madogo), kutwangwa (kupata unga unga) na hatimaye "kukamatishwa" kwa kutumia Mercury ili kupata dhahabu. Mercury inafanya selective extraction ya gold kutoka kwenye unga (Ore) inayojumuisha metali nyingine.
Baada ya kazi ya Mercury, yale mabaki ("baada ya dhahabu" kuwa extracted) yalikua ama yakitupwa, au kutunzwa kwa ajili ya kurudia zoezi la extraction ya Mercury wakati ujao yatakapokua mengi zaidi. Logic hapa ni kwamba Mercury haifanyi extraction ya 100%. Katika point namba 5 tutaanzia hapa kwenye haya MABAKI au MARUDIO au MASAINENTI.
4. Kutumia "vipimio" (Gold detectors) kupata dhahabu:
Hii hasa ni kwa ajili ya kupata dhahabu zilizo kwenye surface (hazikuonekana kwa macho na kuokotwa hapo zamani), zile za kwenye "mchanga wa dhahabu" na kwa uchache kwenye "miamba yenye dhahabu".
Kwa huku kwetu, teknolojia hii imeanza kuchipukia mwaka 2000, imekuja ku peak miaka ya 2005-2010. Kuanzia miaka ya 2010 kuja juu vipimio vilianza kupungua kutokana na uhaba wa "aina ya dhahabu" ambazo vinagundua. Hivyo wenye vipimio walianza kwenda maeneo ya mbali (kutoka huku niliko) ili kutafuta dhahabu zinazoweza kutambuliwa na hivi vipimio. Mfano Mpanda, Maeneo ya nchi ya Msumbiji, Zambia n.k
Ila kwa ujumla ni kwamba kwa sasa kumiliki kipimio imekua kama ni old fashioned way ya kutafuta dhahabu, siku za kulala njaa zinakua ni nyingi sana. Kwa maneno mengine hapa nakuambia kwamba kuwa makini sana kama kweli utaamua kuleta hivyo vifaa. Hali yake ndivyo ilivyo.
Mifano ya "aina" za vipimio (gold detectors) iliyokua maarufu ni kama vile GP, SD, XT, GMT, Fisher, n.k
5. Ujio wa "Leaching plants" pamoja na "Elution" ili KUOZESHA "marudio" (Rejea point namba 3 hapo juu) na hatimaye kupata kupata dhahabu:
Yale mabaki au marudio baada ya shughuli ya Mercury, hapa yanaozeshwa kwa kutumia kemikali kadhaa kwenye mtambo wa uchenjuaji dhahabu na hatimaye kuchomwa ili kuipata dhahabu yenyewe.
Kutokana na hili, the more marudio unazalisha, the more likely kwamba utachenjua mara nyingi na hivyo utapata dhahabu kwa wingi zaidi.
Maana yake sasa, utahitaji maeneo mengi yenye miamba ya dhahabu, utahitaji mitambo mingi ya kusaga mawe (yanaitwa makarasha, yaani crushers) kutengeneza "marudio" mengi zaidi.
Kwa sasa teknolojia hii ya kumiliki "makarasha" ndio ina peak sana kwa "huku kwetu".
6. CIP & CIL Major plants:
Hii ni advanced level ya njia namba 5 hapo juu, inakua na ufanisi mkubwa zaidi katika kuozesha, inachukua large volumes ya marudio at a time na pia ina extract more gold.
Hata hivyo inahitaji mtaji mkubwa na miundombinu thabiti (hasa umeme) ili kuiendesha. Kwahiyo hizi bado ni chache sana.
Unaweza ukaona kuwa katika scenario zote 6 hapo juu (of course kuna zaidi) utaona dhahabu ni ileile, ila kinachobadilika ni TEKNOLOJIA inayotumika kuipata.
Hivyo nakusihi ufanye maamuzi juu ya biashara hiyo kulingana na uhalisia wa mambo yalivyo.
NB: Hii inahusu zaidi wachimbaji wadogo na angalau kidogo wachimbaji wa kati.
Andiko langu si msimamo wa sekta ya madini ya nchi nzima, ila angalau kwa 80% liamini na uliafuate.
Ukitaka nieleze fursa "za kibiashara" zilizopo katika sekta ya madini na mnyororo wake wa thamani, nitafanya mambo mawili yafuatayo:-
A. Nitakuomba unipe muda
B. Nitakueleza kinagaubaga.
Uwe na siku njema.