Mrejesho biashara ya madini ya dhahabu second season

Bufa

Nikujibu hilo la elution, machinery, kemikali na maabara kwa pamoja, with respect to Chunya.

Elution kwa sasa bado ni chache (ukilinganisha na idadi ya Leaching plants ambazo ndio feeder facilities za Elution), na bado ni uwekezaji wenye tija. Lakini ni uwekezaji unaohitaji capital kubwa, na risks (kwa maoni yangu) ni chache.

Machinery na Chemicals hii ni biashara ambayo unaweza kuifanya kwa pamoja. Na kwa maoni yangu ningependekeza uanze na hii (ikikupendeza).

Maabara:
Hizi zipo chache, na mahitaji ya uchimbaji ambao ni based on informed facts (kujua kwenye sampuli kuna dhahabu kiasi gani kabla ya kufanya maamuzi) unazidi kuongezeka.
Hapa napo ni mahala pa zuri kuwekeza.

NB: Majibu yangu ni ya jumla sana, nimeacha "mashimo mengi" ya wenzangu kukosoa, kurekebisha, kuboresha n.k ili kukupatia ushauri bora na utakaokufaa wewe na wengine watakopitia uzi huu.
 
vijana tusibaki kulalamika kwa kuilaumu serikali kushindwa kutuajiri, bali tuziibue fursa

- Kote umeelezea vizuri, kwenye hicho kipengele tu ndiyo umeharibu kila kitu kwa kuwaona wengine walalamishi...
 
Mkuu hizo CIP na CIL major plants ni "bigger versions" za hizi normal Leaching plants.

Kinachoongezeka ni ukubwa wa mzigo unachenjuliwa at a time na ufanisi wa zoezi la uchenjuaji.

Katika kuongeza ufanisi wa uchenjuaji, inajumuisha kuongeza jotoridi la kinachochenjuliwa. Sasa hii warming of Ore inakula umeme si mchezo.

Na kwa ujumla kwa sababu intake yake ni kubwa, basi inahitaji malighafi nyingi sana (mawe au mchanga) ili hii plant iendeshwe kwa tija.
Sitaki kwenda kwenye details za nini kinatokea na hata tukapata CIP (Carbon in pulp) na CIL (Carbon in leach) processes, ila kwa juu juu hizi ni namna mbili "activated Carbon" inawekwa ili kukamata dhahabu kutoka kwenye material inayoozeshwa.

Kwa Chunya nafahamu kuna jamaa anaitwa Aidan Msigwa (Mdimmi) anayo hii plant.

Makadirio ya uwekezaji wake, haiwezi kupungua 1B.
(Kama nakosea wadau watakuja ku correct).

Asante sana mkuu, nilikua sijawahi kusikia hii nitaifanyia kazi.
 
Bufa

Nikujibu hilo la elution, machinery, kemikali na maabara kwa pamoja, with respect to Chunya.

Elution kwa sasa bado ni chache (ukilinganisha na idadi ya Leaching plants ambazo ndio feeder facilities za Elution), na bado ni uwekezaji wenye tija. Lakini ni uwekezaji unaohitaji capital kubwa, na risks (kwa maoni yangu) ni chache.

Machinery na Chemicals hii ni biashara ambayo unaweza kuifanya kwa pamoja. Na kwa maoni yangu ningependekeza uanze na hii (ikikupendeza).

Maabara:
Hizi zipo chache, na mahitaji ya uchimbaji ambao ni based on informed facts (kujua kwenye sampuli kuna dhahabu kiasi gani kabla ya kufanya maamuzi) unazidi kuongezeka.
Hapa napo ni mahala pa zuri kuwekeza.

NB: Majibu yangu ni ya jumla sana, nimeacha "mashimo mengi" ya wenzangu kukosoa, kurekebisha, kuboresha n.k ili kukupatia ushauri bora na utakaokufaa wewe na wengine watakopitia uzi huu.

Asante sana mkuu. Nimekupata vizuri. Nitafanyia kazi, usichoke kutupa your expertise ni darasa tosha.
 
Mkuu, kwanza hongera kwa tafiti unazofanya ili ufanye informed decision. Kama ilivyokuwa kwenye biashara yoyote ile, wapo ambao mambo yanadoda na ambao mambo yanawaendea vema.
Lakini moja ya mbinu ambazo wafanyabiashara kadhaa wanatumia ni kutengeneza "chain of dependency" kwa maana ya kwamba yeye anauza kemikali, anauza machinery na ana elution. Hivyo wale anaowauzia kemikali na mitambo ndio haohao watakua ni wateja wake kwenye elution plant wakishakuza mzigo.

Elution ni uwekezaji mkubwa hivyo unahitaji tafiti ya kutosha kabla ya ku execute, napenda unavyokusanya taarifa. Wewe ni mfano wa muwekezaji smart, keep it up.

The chain of dependency is the key. Asante sana mkuu for your inputs. Nashukuru sana.
 
Mkuu IBRA wa PILI usimbishie Narubongo kuwa faida ya dhahabu ni 2000 hadi 3000 kwa gram. Mkuu iko ivii, inategemea na maeneo. Kwa sababu ya ushindani wa kibiashara unakuta sehemu watu wanainunua dhahabu kwa bei ya juu kuzidi hata bei elekezi ya serikali. Hivyo huambulia faida kiduchu au kupata hasara. Yapo maeneo wanunuzi wa dhahabu wanapata faida maradufu sababu wanaelewana na wananunua dhahabu kwa bei elekezi. Mfano Mimi juzi nilikuwa sokoni nikiwa na 93g nilipoyeyusha ikatoka 91g. Polini nimetumia mil. 7.5, narudi na mil 9.2. Hapo hata Kama nimekaa wiki mbili bado inalipa mnoo.
Million 7 upo na gram 93 uko gram moja bei gani mkuu uku Mozambique gram laki
 
Mkuu, Nasikia kuna elution zimetelekezwa kwa kukosa mzigo. Hii unaongeleaje, haiwezi kuwa changamoto hasa kwa elution mpya?
hii ni changamoto haswa hasa kama ww ni mgeni wa maeneo haya,hii imesababishwa na historia ya nyuma wakati elution zinaanza kujengwa hapa chunya,wasukuma kutoka mwanza ndo waliintroduce hii technology kwa hapa chunya so walikuwa wanawaibia sana watu kwenye kufanya processing, baadae wazawa nao wakaanza kujenga zao jambo lililosababisha elution nyingi za mwanzo na hasa za wageni kukosa wateja hivyo nyingi zinefungwa na wao kurudi kwao,so kama ww ni mgeni itakuwa kazi sana kuaminiwa haraka haraka na kupata wateja jambo la msingi ni kutengeneza connection kubwa
 
Asante mkuu nitafanyia kazi.
 
Hakika wewe umetema pointi za maana na zinazoonyesha uhalisia wa biashara tofauti na wengi wetu hupenda kusikia stori za vijiweni, maake kama faida ingekuwa kubwa sana tunavyoaminishwa basi wengi wangefanya.
Kwan wanaofanya hii biashara n wachache?
 
Mkuu IBRA wa PILI usimbishie Narubongo kuwa faida ya dhahabu ni 2000 hadi 3000 kwa gram. Mkuu iko ivii, inategemea na maeneo. Kwa sababu ya ushindani wa kibiashara unakuta sehemu watu wanainunua dhahabu kwa bei ya juu kuzidi hata bei elekezi ya serikali. Hivyo huambulia faida kiduchu au kupata hasara. Yapo maeneo wanunuzi wa dhahabu wanapata faida maradufu sababu wanaelewana na wananunua dhahabu kwa bei elekezi. Mfano Mimi juzi nilikuwa sokoni nikiwa na 93g nilipoyeyusha ikatoka 91g. Polini nimetumia mil. 7.5, narudi na mil 9.2. Hapo hata Kama nimekaa wiki mbili bado inalipa mnoo.
Mkuu, wewe ni hazina

Kuna mtu nilimuuliza kuhusu hii biashara, aliruka futi 100 [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mil 40 ni mtaji wa jikoni, dealer (mara nyingi muhindi) anakuwa na watu hata 20 na zaidi anaowadhamini majikoni, kila mtu wa jikoni ana dealer wake maalum kama ilivyo kota ana mtu wake maalum jikoni, mtu akitoka elusion anachoma akipata kilo 4 anampigia dealer kuna 4kg au na zaidi dealer anamtumia 400m bank ndo mnalipwa baada ya siku 1 mpaka 3 ila kipindi mnasubiri huwa kuna vimilioni vya advance mnapewa. Kila mwezi dealer anatakiwa kuexport zaidi ya kilo 10 kwa mara moja ili iwe biashara.
Biashara ya dhahabu ni huyu anamkusanyia yule na faida ni ndogo sana tofauti na mnavyodanganyana, kawaida gram 1 faida ni sh 2000-3000, unakusanya dhahabu ya mil 4 ukienda jikoni kuchoma unapata faida isiyozidi elfu 50 au ukarudi na hasara ya malaki kama si mamilioni.
Kuna soko la kimataifa lipo Nairobi kwa ukanda huu
Mkuu 4 kilos umezitaja kiwepesi sana.
 
nikupe hongera nyingi kwa uthubutu na moyo wa kupambana kwa kusimamia kile unachokiamini bila kujali ugumu wa njia uliyopitia.
 
Mkuu 4 kilos umezitaja kiwepesi sana.
[emoji23][emoji23][emoji23] hayo makilo tulipiga miaka 10 iliyopita kwa marudio ya kutwanga kwa kinu. Kwahaya ya sasa unatafuta hela ya kula tu siyo kujenga magorofa. Sikutaka ligi humu kusema unatoka elution na nusu kilo mpaka kilo 2 kwa hali ya sasa
 
Back
Top Bottom