Mac Alpho
JF-Expert Member
- Aug 5, 2019
- 13,953
- 27,825
Mkuu unamjua NSANGANO?Inshallah mkuu..mie niko based zaidi machimbo ya Geita! Ingawa kwa sasa nachungulia chungulia tu chimbo lililopuka...!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu unamjua NSANGANO?Inshallah mkuu..mie niko based zaidi machimbo ya Geita! Ingawa kwa sasa nachungulia chungulia tu chimbo lililopuka...!
Kweli kaka umepambana lakini naomba tuwasiliane namba 0629696362Hongera boss.
Ila sisi vijana huwez kutuona kwenye thread kama hizi, ila za mateso mtu anayopitia ndipo utakukuta huko, au tuliyempekua tukakuta sintofahamu( utapeli) ndio utatukuta huko, pengine hapa tumekupekua thread zote na comment zako zote humu tukakuta hauna chembe ya utapeli, kwahio huwez kutuona wengi ndio mana unaona ndani ya masaa 17 kuna comment 5 tu.
Ila naamini ume inspire wale wenye mlengo wa kuingia huko kwenye dhahabu.
Wangari Maathai umeona hii?
Ukiwa mtu wa machimbo na umepita nyarugusu geita ni lazima umjue Nsangano,naamini mdau pia atakua familiar na jina hiloMkuu unamjua NSANGANO?
Wewe utakuwa unamjua, humu kuna I'd moja ni ya mke wake.Ukiwa mtu wa machimbo na umepita nyarugusu geita ni lazima umjue Nsangano,naamini mdau pia atakua familiar na jina hilo
Wewe utakuwa unamjua, humu kuna I'd moja ni ya mke wake
This is Jf bro hadi mkewe yupo huku kwa ma great thinkersWewe utakuwa unamjua, humu kuna I'd moja ni ya mke wake.
Tunakushukuru sana kiongoz kwa mchango wako. Je vipimo vya kutambua purity ya dhahabu ni bei gan?Nitakujibu kwa majibu marefu kidogo, kuwa mvumilivu, tiririka nami.
Majibu haya ni kwa mujibu wa my personal experience (nimezaliwa na kukulia katika moj ya maeneo ya uchimbaji wa madini ya dhahabu nchini Tanzania)
Hivyo kunaweza kuwa na mabadiliko kidogo katika hoja zangu kulingana na hali ilivyo katika maeneo yenye madini nchini.
Tutazame kwanza mabadiliko ya trends za teknolojia za kupata dhahabu na nyakati zake.
1. Kuokota dhahabu maeneo mbalimbali (kwenye surface land) hasa ya maeneo ya mitoni, n.k :
Hizi ni zama za zamani sana, hasa kabla ya uhuru na kabla ya kuja watu weupe barani Afrika. Kama umeshawahi kusikia kwamba zamani dhahabu zilikua zinatumika kama "kete" za kuchezea bao. It was that simple, that abundant.
2. Kuchimba ili kupata "mchanga wa dhahabu" na kuosha ili kuipata dhahabu yenyewe (kusekesa/kuchekecha, kupiga kalai):
Hapa kilichokua kinatafutwa ni "mchanga wa dhahabu", na hatimaye unaoshwa kwa njia nilizotaja hapo juu ili kupata madini ya dhahabu. Ni njia ambayo inahitaji maji na kinachopatikana hapa tunaweza kusema ni "pure gold".
3. Kuchimba mashimo marefu (long bases) ili kutafuta MIAMBA inayoambatana na dhahabu:
Katika njia hii miamba hiyo hulainishwa (kuwa mawe madogo madogo), kutwangwa (kupata unga unga) na hatimaye "kukamatishwa" kwa kutumia Mercury ili kupata dhahabu. Mercury inafanya selective extraction ya gold kutoka kwenye unga (Ore) inayojumuisha metali nyingine.
Baada ya kazi ya Mercury, yale mabaki ("baada ya dhahabu" kuwa extracted) yalikua ama yakitupwa, au kutunzwa kwa ajili ya kurudia zoezi la extraction ya Mercury wakati ujao yatakapokua mengi zaidi. Logic hapa ni kwamba Mercury haifanyi extraction ya 100%. Katika point namba 5 tutaanzia hapa kwenye haya MABAKI au MARUDIO au MASAINENTI.
4. Kutumia "vipimio" (Gold detectors) kupata dhahabu:
Hii hasa ni kwa ajili ya kupata dhahabu zilizo kwenye surface (hazikuonekana kwa macho na kuokotwa hapo zamani), zile za kwenye "mchanga wa dhahabu" na kwa uchache kwenye "miamba yenye dhahabu".
Kwa huku kwetu, teknolojia hii imeanza kuchipukia mwaka 2000, imekuja ku peak miaka ya 2005-2010. Kuanzia miaka ya 2010 kuja juu vipimio vilianza kupungua kutokana na uhaba wa "aina ya dhahabu" ambazo vinagundua. Hivyo wenye vipimio walianza kwenda maeneo ya mbali (kutoka huku niliko) ili kutafuta dhahabu zinazoweza kutambuliwa na hivi vipimio. Mfano Mpanda, Maeneo ya nchi ya Msumbiji, Zambia n.k
Ila kwa ujumla ni kwamba kwa sasa kumiliki kipimio imekua kama ni old fashioned way ya kutafuta dhahabu, siku za kulala njaa zinakua ni nyingi sana. Kwa maneno mengine hapa nakuambia kwamba kuwa makini sana kama kweli utaamua kuleta hivyo vifaa. Hali yake ndivyo ilivyo.
Mifano ya "aina" za vipimio (gold detectors) iliyokua maarufu ni kama vile GP, SD, XT, GMT, Fisher, n.k
5. Ujio wa "Leaching plants" pamoja na "Elution" ili KUOZESHA "marudio" (Rejea point namba 3 hapo juu) na hatimaye kupata kupata dhahabu:
Yale mabaki au marudio baada ya shughuli ya Mercury, hapa yanaozeshwa kwa kutumia kemikali kadhaa kwenye mtambo wa uchenjuaji dhahabu na hatimaye kuchomwa ili kuipata dhahabu yenyewe.
Kutokana na hili, the more marudio unazalisha, the more likely kwamba utachenjua mara nyingi na hivyo utapata dhahabu kwa wingi zaidi.
Maana yake sasa, utahitaji maeneo mengi yenye miamba ya dhahabu, utahitaji mitambo mingi ya kusaga mawe (yanaitwa makarasha, yaani crushers) kutengeneza "marudio" mengi zaidi.
Kwa sasa teknolojia hii ya kumiliki "makarasha" ndio ina peak sana kwa "huku kwetu".
6. CIP & CIL Major plants:
Hii ni advanced level ya njia namba 5 hapo juu, inakua na ufanisi mkubwa zaidi katika kuozesha, inachukua large volumes ya marudio at a time na pia ina extract more gold.
Hata hivyo inahitaji mtaji mkubwa na miundombinu thabiti (hasa umeme) ili kuiendesha. Kwahiyo hizi bado ni chache sana.
Unaweza ukaona kuwa katika scenario zote 6 hapo juu (of course kuna zaidi) utaona dhahabu ni ileile, ila kinachobadilika ni TEKNOLOJIA inayotumika kuipata.
Hivyo nakusihi ufanye maamuzi juu ya biashara hiyo kulingana na uhalisia wa mambo yalivyo.
NB: Hii inahusu zaidi wachimbaji wadogo na angalau kidogo wachimbaji wa kati.
Andiko langu si msimamo wa sekta ya madini ya nchi nzima, ila angalau kwa 80% liamini na uliafuate.
Ukitaka nieleze fursa "za kibiashara" zilizopo katika sekta ya madini na mnyororo wake wa thamani, nitafanya mambo mawili yafuatayo:-
A. Nitakuomba unipe muda
B. Nitakueleza kinagaubaga.
Uwe na siku njema.
Sifahamu kwa sasa, labda nifuatilieTunakushukuru sana kiongoz kwa mchango wako. Je vipimo vya kutambua purity ya dhahabu ni bei gan?
Sent from my SM-J810F using JamiiForums mobile app
Unachosema ni kweli kuna wachangiaji wachache kwenye NYUZI za aina hii, LAKINI mimi nadhani sababu mojawapo ya uchache wa uchangiaji ni UGUMU WA WALETA NYUZI kujibu maswali au kutoa maelezo kwa wana JF wanao uliza ili kujua nyendo zote ikiwa ni pamoja na mafanikio na changamoto alizokutana nazo mtoa UZI! Hali kama hii inakatisha tamaa kuchangia au kuuliza maswali kwa nia na lengo la kutaka kujua! Kwa mfano, kuna mwana JF kamuuliza mleta UZI yuko chimbo gani, na mkoa gani!? Yeye kanyamaza kimya. Katika hali hii wewe mwingine utauliza kweli!? TUJISAHIHISHE kama tunataka kusaidiana KIMAWAZO humu JF.Hakika, something is wrong somewhere.
Kwa hivi vilio vya ajira kila siku humu jukwaani na kwingineko katika hali ya kawaida ungetarajia uzi huu uwe umefurika watu wakitoa pongezi, kujifunza na kuuliza ni jinsi gani na wao wanaweza pita njia hii ama fursa nyingine zinazo ambatana na njia hii.
mcrounmj hebu tupe details za mchakato wote hasa hasa kwenye ununuzi wa dhahabu wewe kama BROKER na uuzaji wake na pia ni masoko yapi unatumia na ikiwezekana tupe experience yako ya namna ulivyo tapeliwa na baadaye kuinuka kwani ulisema kuwa hadi unaingia machimboni ulikuwa na balance ya 2M/-! Je hiyo ndiyo ilikufikisha kwenye 20M/= ya sasa AU ILIKUWAJE!?Mkuu nipo Chunya Mbeya.
Yes, safi kabisa kwa maelezo ya KISOMI kutoka kwa MSOMI mpambanaji! Keep it up mcrounmj!Wakuu napata napata msg nyingi pm. Labda niseme tu kuwa hii biashara ya madini ni kama biashara zingine. Ukiwa serious unatoboa na ukiifanyia masihara hela haichelewi kukata. Kama umehamasika na hii biashara nakushauri nenda sehemu za migodi kaanze kazi. Utakutana na wazoefu wa maeneo husika utajifunza toka kwao. Anza kidogo kidogo ukiwa unausoma mchezo.
Kitu kingine mimi naweza kukushauri kitu kwa mjibu wa mazingira yangu kumbe nimekulisha tangopori kwa mazingira utakayokuwepo. Mfano kuna mdau juzi aliuliza "ni mtaji wa kiasi gani unaweza kuanza nao".... Kwa mjibu wa uzoefu wangu na nature ya eneo nilishauli angalau milioni nne. Kumbe yapo maeneo ambayo hata mtaji wa laki tatu unatosha. Hii ni kwa mjibu wa mdau Wangari Maathai, nami nakubaliana naye!
Hivyo wakuu nawashauri tutembelee maeneo ya migodi tuliyonayo karibu. Wapo wanunuzi wa siku nyingi tuwatumie hao kupata taarifa sahihi kutegemeana na eneo. Tofauti na hivyo Mimi sitajibu pm wala kutoa namba maana kama ilivyo jamii forum imekuwa ni kichaka ambacho wapo twiga, Simba, mbweha, sungura, chatu, swala n.k n.k, itoshe tu kusema maswali tumalizie hapahapa
Cha mwisho, kwa wale tutakaofanikiwa kuianza hii biashara tujitahi kufuata sheria za nchi kwa kuepusha utoroshaji, kununulia kwenye masoko yanayotambuliwa na serikali, kuorodhesha kwenye daftari la kumbukumbu za manunuzi na mauzo ya dhahabu na kisha kuuza kwenye masoko yaliyo kwenye wilaya au mikoa na unabaki na list za mauzo. Lipa kodi uliyokadiliwa na tra. Hapo biashara utaiona tamu.
Cha
Ila Master Dealer anaweza kupeleka popote ikiwa ni pamoja na Kenya ingawa nadhani masharti ya hiyo leseni ni magumu kidogo au siyo Wangari Maathai?Saidia katika hili.Mkuu hairuhusiwi kuuza madini nje ya mkoa hadi uwe na vibali..hao broker ndo hao hao wanunua dhahabu...! Lakini inategemea na akili yako na usmart wako tu mkuu kusafirisha..Kenya soko ni zuri zaidi .kama unaweza tambaa na maji usk mzima unaibukia huko unauza...ila ni risk unapokonywa na hupat ng'o!
Sheria zimewekwa ili zivunjwe😜!
"DHAHABU ILIYOPEMBULIWA" una maana ni ile safi au ni ile ya wachimbaji wadogo wadogo ambayo haijasafishwa!? Nifafanulie Msomi wangu!Cha msingi pesa itoshe kukata leseni na leseni ni kama laki nne au tano kutegemeana. Hapo kuna scale ya kugrade uzito wa dhahabu inauzwa laki mbili na nusu, jumla unakuwa kama laki saba hivyo, hujakarabati chumba, na vitu vingine vidogovidogo, almost milioni inaisha kwenye maandalizi. Guys usilogwe ukaanza kununua bila kukata leseni, kwenu watakusahau.
Wakikukamata ni uhujumu uchumi, hawana msamaha. Hapo Sasa ukikamilisha vibali anza na mtaji angalau wa milioni moja. Hapo utakuwa na uhakika wa kwenda sokoni angalau gram kumi na...
Chengine kama ndo unaanza nakushauri usinunue mawe au fero, utajuta na hiyo ndiyo kamali pure. Wewe ukiwa mgeni jikite kununua dhahabu iliyopembuliwa fullstop.
PENYE NIA PANA NJIA NA MUNGU AKIWA MBELE YA YOTE.Umeni insipire sana, nilisha sikia habari za hii biashara kupitia kipindi cha E-fm (ubaoni-ripoti ya leo) kuna mdada alikuwa ana simulia jinsi mume wake alivyo kuwa akipambana na hii biashara mpaka kufanikiwa na alianza na 2M's pekee naona na wewe una nizidishia ukali wakusaka capital ili niingie humo kupambana kazi ninayo ifanya kwa sasa balipwa 250k so ina hitaji uvumilivu ili kufikisha mtaji hata wa 3M's maana hiyo hiyo 250k nina takiwa nihakikishe na weka akiba pia nakula na vaa kwa hyo hiyo 250k ila naamini nita fika tu kikubwa ni juhudi na kumuomba sana mungu atufungulie milango iliyo fungwa.
Mimi nadhani HOJA hapa siyo faida ya hii biashara, nadhani HOJA hapa ni MTAJI na UDIRIKI. Hivi ni vitu au mambo muhimu sana kwa mtu yoyote kuingia kwenye hii biashara. Ukiwa na MTAJI mzuri unaweza kununua mzigo mkubwa na hivyo kupata faida kubwa bila kujali eti "biashara hii ina faida ndogo". Faida ndogo ndiyo inapelekea kupata faida kubwa kama una MZIGO mkubwa ambao utatokana na MTAJI na UDIRIKI wako wa kuwekeza.Hakika wewe umetema pointi za maana na zinazoonyesha uhalisia wa biashara tofauti na wengi wetu hupenda kusikia stori za vijiweni, maake kama faida ingekuwa kubwa sana tunavyoaminishwa basi wengi wangefanya.
Ila kuna maswali madogo madogo hujajibu! Kwa mfano, soko lako ni wapi? Ni hapo hapo Chunya au nje ya hapo? Na range ya selling price inakuwaje na mwisho nikitaka kuanza kazi kama Broker, nahitaji kuwa na VITENDEA KAZI gani muhimu ukiacha pesa? Wengine wanasema ni vizuri uwe na mzani na hata mashine ndogo ya kujua hii ni dhahabu au shaba n.k n.k. hii ikoje. Asante tena Msomi wangu.Wakuu December hii nitaleta mrejesho wapi nimefika. Na mwisho kabisa ilikuwa kufikia levo ya kuwa dealer. Guys keep informed.... Kuna cha kujifunza kwenye safari yangu hii. Kwahiyo June ya 2022 utakuwa ni mrejesho wangu wa mwisho. Tuombe uzima kwa mola!!
Nimeshaweka kambi mkuu,kusubiri mrejesho😃Wakuu December hii nitaleta mrejesho wapi nimefika. Na mwisho kabisa ilikuwa kufikia levo ya kuwa dealer. Guys keep informed.... Kuna cha kujifunza kwenye safari yangu hii. Kwahiyo June ya 2022 utakuwa ni mrejesho wangu wa mwisho. Tuombe uzima kwa mola!!
Soko langu ni chunya.... Porini tunanunua kuanzia themanini hadi tisini kwa gram, sokoni tunauza kwa laki mpaka laki na elfu tano kutegemea na asilimia ya dhahabuIla kuna maswali madogo madogo hujajibu! Kwa mfano, soko lako ni wapi? Ni hapo hapo Chunya au nje ya hapo? Na range ya selling price inakuwaje na mwisho nikitaka kuanza kazi kama Broker, nahitaji kuwa na VITENDEA KAZI gani muhimu ukiacha pesa? Wengine wanasema ni vizuri uwe na mzani na hata mashine ndogo ya kujua hii ni dhahabu au shaba n.k n.k. hii ikoje. Asante tena Msomi wangu.
Kuhusu vitendea kazi ni scale ya kupima uzito wa Dhahabu tu Basi. Kuhusu kuuziwa Dhahabu feki macho yataijua tu. Na saivi Dhahabu zinanunuliwa masokoni hivyo akileta mteja hautakuwa peke yako maana zipo ofisi nyingi hivyo unauliza wenzakoIla kuna maswali madogo madogo hujajibu! Kwa mfano, soko lako ni wapi? Ni hapo hapo Chunya au nje ya hapo? Na range ya selling price inakuwaje na mwisho nikitaka kuanza kazi kama Broker, nahitaji kuwa na VITENDEA KAZI gani muhimu ukiacha pesa? Wengine wanasema ni vizuri uwe na mzani na hata mashine ndogo ya kujua hii ni dhahabu au shaba n.k n.k. hii ikoje. Asante tena Msomi wangu.