Mrejesho biashara ya madini ya dhahabu second season

Mrejesho biashara ya madini ya dhahabu second season

Mil 40 ni mtaji wa jikoni, dealer (mara nyingi muhindi) anakuwa na watu hata 20 na zaidi anaowadhamini majikoni, kila mtu wa jikoni ana dealer wake maalum kama ilivyo kota ana mtu wake maalum jikoni, mtu akitoka elusion anachoma akipata kilo 4 anampigia dealer kuna 4kg au na zaidi dealer anamtumia 400m bank ndo mnalipwa baada ya siku 1 mpaka 3 ila kipindi mnasubiri huwa kuna vimilioni vya advance mnapewa. Kila mwezi dealer anatakiwa kuexport zaidi ya kilo 10 kwa mara moja ili iwe biashara.
Biashara ya dhahabu ni huyu anamkusanyia yule na faida ni ndogo sana tofauti na mnavyodanganyana, kawaida gram 1 faida ni sh 2000-3000, unakusanya dhahabu ya mil 4 ukienda jikoni kuchoma unapata faida isiyozidi elfu 50 au ukarudi na hasara ya malaki kama si mamilioni.
Kuna soko la kimataifa lipo Nairobi kwa ukanda huu
Ndugu we muongo faida EF 2 au EF 3
Nina rafik angu anachukua dhahabu msumbiji eneo la kaguruwe ana kuja uza dar kila baada ya wiki moja,
gram 100 Sawa na milioni 10 gram ananunua laki sokoni inacheza laki na 25 ivi,
this time Mara ya mwisho katoka dar na faida ya 1.8million akitoa process zingne ndio anabaki na iyo 1.8 m
Au labda sijaelewa maelezo yako vizuri lakin kama ndio ayo hapo juu faida ef 3 big no ukitaka nikupe na namba ya simu muulize ata kwambia na kama upo dar wiki hii anakuja apo kuuza dhahabu muulize.
 
Mkuu unataka kusema biashara hii haina faida kama ambavyo tunataka kuamini hapa ?
 
Kumbe maneno ya kuambiwa halafu unataka kubishana na ... hiyo bei ya 98,000-105,000 kwa mbichi ndo inayotembea hata hapa nilipo sasa hivi nashangaa huyo jamaa yako kwanini aende mbali huko msumbiji wakati angeenda hapo handeni angepata kwa bei hiyo hiyo.
Ukipeleka dhahabu jikoni au sokoni ni lazima ipigwe moto na hapa lazima uzito utapungua ndio maana kota ananunua 100,000 anapewa jikoni 108,000-110,000 baada ya kutoa tozo zote kutegemea na %ge purity, hapa ametengeneza faida ya elfu 2 au 3 kama sio hasara. Ukiwa na gram 50 zinaweza kupungua gram 3-7 kutegemea na aina ya dhahabu. Jana bei ilikuwa 130,000 jikoni so ukitoa mrabaha, vat unachobaki nacho ni hicho wewe hujazingatia haya.. na huyo jamaa yako hiyo ni pure smuggling watch out
 
Mkuu unataka kusema biashara hii haina faida kama ambavyo tunataka kuamini hapa ?
Kuwa makini na habari za namna hii, mtu kapewa stori kwenye daladala anakuja kuleta uzi. Bei ya dhahabu ni ile ile popote uendapo usitegemee kupata super profit
 
Hii biashara ni tofaut na tunavyohadithiana.kwanza inahtaj roho ngumu na ukatil ndani yake.na ukiwa mtu Wa dini huwezi Fanya hii bizn..kiufup kwenye biashara kama hz kutoboa ni ngekewa ya MTU.ili upate faida ni lazima uwe mdanganyifu.faida ya dhahabu inatokana na umenunuaje na ubora wake..mana sio kwamba hiyo 130000 ni kwa kila dhahabu.apana hiyo ni kwa zile pure yani karat 24.na wengi wanafeli kwenye hili unaenda porini unanunua kwa 95000 per gram.unakuja sokoni unakuta ni karat 18 ambayo ukitajiwa bei unaweza lia.bei unambiwa hii tunanunua 75000.ukipiga hesabu apo kila grm imekata 20000.bado ikichomwa inapungua.kama ulikuwa umebeba grm 50 lazma ikate 2.5,au tatu kabisa.kwa hiyo apo ni kucheza na soko +asilimia na kuminya mzani.ukipoteza point moja ni sawa na kudondisha 10000..ila ukiipatia unawezatoa ushuda aljazeera au CNN.
 
Mkuu Wangari Maathai kwa ufahamu na uzoefu wako, mtaji wa milioni 40 unatosha kuanzia kusafirisha (kihalali) madini ya dhahabu kwenda nje ya nchi ?

Ukiacha UAE (Dubai) ni eneo gani jingine unashauri mtu akauze madini nje ya nchi ambako kuna soko la uhakika ?
Mkuu wengi walikua wanapeleka pia kenya wale wenye mitaji ya kati...
inatosha! Kata vibali ..!
Nadhani leseni ya kukuwezesha kuuza nje madini moja ya kigezo ni mtaji kuanzia 100m, chini ya hapo utatakiwa kukata leseni ya brocker.
 
Panapo majaaliwa ya mwenyezi Mungu tumekutana tena kwenye kikao cha wapambanaji. Wakuu wa jukwaa hili hususani vijana nawasalimu kwa Salam adhimu ya mama yetu Samia Suluhu Hassan......

Bila kuwachosha ni kuwa tangu nimeianza safari yangu ya kibiashara nimekuwa nikiwashirikisha hatua ninazopitia, ups and downs na Mambo lukuki. Nikiri tu kuwa kufanya biashara na ikakua siyo kitu kidogo. Inahitaji uvumilivu, umakini na bidii.

Mwaka Jana 2020 June nilikuja kwenye jukwaa hili kuomba ushauri juu ya kuanzisha biashara ya madini ya dhahabu. Watu wengi walinishauri, walinitia moyo na kunikatisha tamaa pia. Nilifanikiwa kukata leseni na vibali vingine na kuanza biashara kama blocker. Pamoja kuwa na mtaji mdogo yaani mpaka napata vibali ilikuwa imebaki milioni nne tu na changamoto nyingine lakini kutokea June nianze biashara hadi December nilikuwa nimefikisha milioni kumi na upuuzi (ndani ya miezi sita).

Nimeianza January ya mwaka huu na moto zaidi, kwanza nikiwa na uzoefu wa kutosha na pili nikiwa nimeshapata connection na watu tofautitofauti.

Malengo yangu ilikuwa mpaka kufika June ya mwaka huu kuanzia January niwe na zaidi ya milioni ishirini na hapo ninunue karasha nianze kukuza mlima na biashara ya dhahabu nikiendelea nayo.

To be honest guys, malengo yamefika kabla ya muda. Ninachokisubiri ni kwenda kuchonga karasha tu niwe na mwalo wangu. Tangu nimeianza biashara hii Sasa naenda kukamilisha mwaka mmoja this June. Vivyo kwa ukuaji wa kiwango hicho naona kama ushindi mkubwa mno kwangu.

Nimeandika na nimekuwa nikiandika my ways to success ili ku share na vijana wenzangu kwa sababu naamini njia niliyopita kufika hapa lipo kundi kubwa la vijana wanapita na pengine wanahisi wamepotea. Mimi ni mhanga wa wahitimu wa chuo kikuuu waliokosa ajira. Niliamua kupambana na umasikini nikifanya vibarua vyote vya halali nikikusanya vipande vya sarafu ili nipate mtaji.

Changamoto ni nyingi mno. Ni lazima ujifunze kuzipunguza zenye kupunguzika, ubalansi matumizi yako na biashara. Katika kipindi cha mwaka mzima kuna muda nimeanguka, nimetapeliwa zaidi ya milioni mbili kwa siku moja, zipo siku nimenunua mzigo kwenye kuuza ulikata zaidi ya milioni mbili, n.k n.k...

Cha mwisho ni kwamba vijana tusibaki kulalamika kwa kuilaumu serikali kushindwa kutuajiri, bali tuziibue fursa na kisha tuidai serikali ijenge mazingira rafiki katika kukuza biashara zetu. Wanajukwaa hususani vijana, giza ni nene safari ni ndefu lakini tutatoboa.

#kikaochawapambanaji

Hongera sana mkuu
Umenipa moyo juu ya hii biashara
Naomba mtupe maelezo kuhusu hizi leseni kwa anejua
Mwaka 2016 wakati nafatilia habar za madini nilijua kwamba leseni zinatolewa kikanda ambayo inahusisha mkoa zaid ya mmoja mfano dar,moro,tanga na pwani
Juzi nilienda ofisi za madini dar kutaka broker licence wakaniambia sheria zimebadilika na kwamba kila mkoa una broker licence yake na huwezi kutumia broker licence kwa mkoa zaid ya mmoja.
Naomba mwenye kujua atufafanulie je hizi leseni kwa sheria ya sasa zipoje?
 
Hii biashara ni tofaut na tunavyohadithiana.kwanza inahtaj roho ngumu na ukatil ndani yake.na ukiwa mtu Wa dini huwezi Fanya hii bizn..kiufup kwenye biashara kama hz kutoboa ni ngekewa ya MTU.ili upate faida ni lazima uwe mdanganyifu.faida ya dhahabu inatokana na umenunuaje na ubora wake..mana sio kwamba hiyo 130000 ni kwa kila dhahabu.apana hiyo ni kwa zile pure yani karat 24.na wengi wanafeli kwenye hili unaenda porini unanunua kwa 95000 per gram.unakuja sokoni unakuta ni karat 18 ambayo ukitajiwa bei unaweza lia.bei unambiwa hii tunanunua 75000.ukipiga hesabu apo kila grm imekata 20000.bado ikichomwa inapungua.kama ulikuwa umebeba grm 50 lazma ikate 2.5,au tatu kabisa.kwa hiyo apo ni kucheza na soko +asilimia na kuminya mzani.ukipoteza point moja ni sawa na kudondisha 10000..ila ukiipatia unawezatoa ushuda aljazeera au CNN.
Duh
 
Nadhani leseni ya kukuwezesha kuuza nje madini moja ya kigezo ni mtaji kuanzia 100m, chini ya hapo utatakiwa kukata leseni ya brocker.
Wengi wanauza kupitia leseni ya mtu mwingine ..ah habari za madini kila mtu anavyoona...wengine tutafia huku...
 
Nilishaifanya hii biashara kiukweli mpaka uje kuimaster inaitaj moyo mana tofaut yake na forex ni ndogo sana.mpaka nilikuja kujifunza namna ya kuipandisha asilimia kutoka karat 18 mpaka 22.mana kipimo hakijawah kusoma 100 mwisho ni 99 ndo pure.sio biashara ya kukurupukia inahtaj subira na risk
 
Kumbe maneno ya kuambiwa halafu unataka kubishana na ... hiyo bei ya 98,000-105,000 kwa mbichi ndo inayotembea hata hapa nilipo sasa hivi nashangaa huyo jamaa yako kwanini aende mbali huko msumbiji wakati angeenda hapo handeni angepata kwa bei hiyo hiyo.
Ukipeleka dhahabu jikoni au sokoni ni lazima ipigwe moto na hapa lazima uzito utapungua ndio maana kota ananunua 100,000 anapewa jikoni 108,000-110,000 baada ya kutoa tozo zote kutegemea na %ge purity, hapa ametengeneza faida ya elfu 2 au 3 kama sio hasara. Ukiwa na gram 50 zinaweza kupungua gram 3-7 kutegemea na aina ya dhahabu. Jana bei ilikuwa 130,000 jikoni so ukitoa mrabaha, vat unachobaki nacho ni hicho wewe hujazingatia haya.. na huyo jamaa yako hiyo ni pure smuggling watch out
Aisee za kusikia nimekwambia namba yange ipo na kama upo dar anakuja kuja apo muulize
 
Je unaweza kutumia leseni ya broker yenye jina la mtu mwengine kufanyia biashara?
Mkuu migodini kuna mambo mengi sana mradi muaminiane tu... watu wanatembea usk mzima ziwani wanaenda kuuzia +254
 
Umeni insipire sana, nilisha sikia habari za hii biashara kupitia kipindi cha E-fm (ubaoni-ripoti ya leo) kuna mdada alikuwa ana simulia jinsi mume wake alivyo kuwa akipambana na hii biashara mpaka kufanikiwa na alianza na 2M's pekee naona na wewe una nizidishia ukali wakusaka capital ili niingie humo kupambana kazi ninayo ifanya kwa sasa balipwa 250k so ina hitaji uvumilivu ili kufikisha mtaji hata wa 3M's maana hiyo hiyo 250k nina takiwa nihakikishe na weka akiba pia nakula na vaa kwa hyo hiyo 250k ila naamini nita fika tu kikubwa ni juhudi na kumuomba sana mungu atufungulie milango iliyo fungwa.
 
Hongera boss.

Ila sisi vijana huwez kutuona kwenye thread kama hizi, ila za mateso mtu anayopitia ndipo utakukuta huko, au tuliyempekua tukakuta sintofahamu( utapeli) ndio utatukuta huko, pengine hapa tumekupekua thread zote na comment zako zote humu tukakuta hauna chembe ya utapeli, kwahio huwez kutuona wengi ndio mana unaona ndani ya masaa 17 kuna comment 5 tu....
Hongera sana mkuu, Mungu akutangulie katika safari yako ya mafanikio.
 
Back
Top Bottom