Mrejesho: Faida nilizopata baada ya kuwatoa watoto wangu shule ya English Medium na kuwarejesha kayumba

Siku warudishe wafanye test na wenzake wa shule waliyotoka kama hujatoa machozi
Huyo jamaa anajipa matumaini hewa. Mimi nilisoma shule mojawapo katika zinazoitwa za vipaji nakumbuka nimetoka darasa la 7 wilayani kwetu nilikuwa wa moto sikosekani top 3.. kufika form one nikadhani hali itaendelea kawaida nikashangazwa kwenye stream yetu nikawa wa 22 katika watoto 30. Hapo nilikuwa nina average ya 61%. Ningekuwa St Kayumba huenda ningeongoza au kuwa top 3. Form four tukawa na Div One 50 huku 2 zikiwa 19. Imagine One ya 7 hadi 10 kuna wakali wamejazana hadi mimi kufikiwa ni mbali sana. Wazazi wanakosea kudhani kuwa wa kwanza ndo tija. Anaweza kuwa wa kwanza ila kaongoza vilaza wenzake.
 
Algore shule za private walimu huwa wanapika matokeo ili kuwa brain wash wazazi.

.uongo
Kwa nini shule za private za nsingi na sekondari za private huwa ndio nyingi zinaongoza kitaifa Unakuta katika shule mia bora kitaifa shule za Serikali zinakuwa 10.je wao pia huwa wana brain wash baraza la mitihani ya taifa?

Usijifariji kwa vitu hewa
 
Uzi ufungwe, majibu yote yapo hapa
 
Uzi ufungwe, majibu yote yapo hapa
Hapana. Huyo nae anataka kuhalalisha hoja isiyo na mashiko. Kwamba tukifika chuo kiingereza kinabadilika? Huo ni uongo. Misamiati inaongezeka lakini sio lugha kubadilika. Na kama mtu kiingereza cha kawaida tu kinamshinda hicho cha chuo si ndo balaa? Na kusema tukae tusubiri serikali irekebishe shule zake zote ni sawa na kukubali kuendelea kuwa wajinga na maskini na kukubali tabaka la watu wachache waendelee kufaidi fursa zinazoletwa na kuwa na elimu bora
 
NJE YA KUKIMBIA GHARAMA ZA ADA NA MATUNZO YA MTOTO FAIDA UPATAZO NI [emoji116]
Kuokoa watoto wako ktk janga la ushoga na usagaj, hizo shule za kizungu wanamitindo mingi ya hovyo ambayo iko kinyume na tamaduni za mtu aliyekamilika mahala popote dunian.

Pia kumfunza uhalisia wa maisha, kwa kizazi chetu mambo ya shule tungeachana nayo tunapoteza muda, somesha mpaka darasa la7 akishajua kusoma na kuandika inatoka huyo peleka , ufundi ama kuwa supervisor wake ajifunze shughuli zako za kiuchumi,

Achen kupoteza muda kusomesha watoto ktk hii mifumo mibovu ya elimu, wakisoma wachache nchn inatosha wengne tubaki kupambania mambo ya msingi.
 
Kutwa/wiki watoto wanacheza tu, eti kisa mwl kaenda kwenye mwenge, mara kuna shughuli za vyeti vya kuzaliwa, mara kuna chanjo, mtoto mpaka anamaliza miezi 6 daftari halijafika hata nusu.Jamaa eti hizo ndio shule.
 
Duh! Wewe umekata tamaa sana aisee....
 
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kutwa/wiki watoto wanacheza tu, eti kisa mwl kaenda kwenye mwenge, mara kuna shughuli za vyeti vya kuzaliwa, mara kuna chanjo, mtoto mpaka anamaliza miezi 6 daftari halijafika hata nusu.Jamaa eti hizo ndio shule.
Tuition zipo
 
Usikilizwe
 
Binafsi English Medium ninayo ikubali ni Feza sababu hawana Tuition wala kukaririsha watoto, likizo watoto wanaenda kama kawaida.
Shule za catholics hupiga marufuku kabisa mtoto kusoma tuition popote

Wanajiamini kuwa walichofundisha kinatosha
 
Tuache kujifariji shule ya kidumu na ufagio ni ngumu. Eti ukisoma shule za private unakua mayai😏
Haelewi huyo .Pita eneo la shule ya kayumba wanafunzi utakuta wanapiga makelele utafikiri uko soko la kariakoo mwalimu kama hajaingia nenda shule.ya private utakuta kuko kimya utafikiri hamna eatu eatoto wako serious kusoma mwalimu hata asipokuwepo
 
Kiwanja Mvuti???😁 Tatizo Pesa na wengi kama huyu mtoa Mada anajalibu kujustfy Umasikini wake kuwa alichofanya ni sawa.
Zipo faida za mtoto kusoma shule Za Private, Mtoto alieasoma Makurumla Secondary School uwezi mfananisha na yule aliesoma St. Joseph au Feza...Ikumbukwe hawa wote wanasoma syllabus moja na wanafanya mtihani wa Darasa la saba huo huo.
Isitoshe Mtoto anaesoma Feza , Watoto wenzanke anaosoma nao wanakuwa toka familia za watu wenye pesa, vyeo n.k anakuwa na Future Connection za huakika.Uwezi ukawa unasomesha mtoto wako kwa Mtogole Secondary School Yenye uhaba wa Walimu, Ukosefu wa Vifaa vya mahabara na Vitabu ukatagemea huyo mtoto akafaulu vizuri.Tafuta Hela acha fikira za Umasikini.Usintanie wewe
 

Attachments

  • 60B1C8E0-EBD2-43B1-B7E1-F78B877F09D8.jpeg
    7.7 KB · Views: 4
  • 18FBCCEC-F9EF-4406-992F-AF3F22D8CDEC.jpeg
    8.1 KB · Views: 3
  • 916CC458-65EC-49E0-AAC1-C41E662C6AEB.jpeg
    6.1 KB · Views: 4
  • 6F04A9D0-F67F-4A03-9E27-BF76E0908309.png
    29 KB · Views: 4
  • BBBBF5AD-5D09-4CA7-A1FB-B4CC82DB2E2C.jpeg
    8.1 KB · Views: 4
  • 10F106AD-90DD-4186-A724-1DB09DEA915D.jpeg
    7.1 KB · Views: 4
  • 814BEA04-572A-4850-92AC-3FA208A3590C.jpeg
    7.9 KB · Views: 4
  • 8682D699-0678-4E60-8A1C-035017E59526.jpeg
    10.7 KB · Views: 3
  • A77DE35D-FB5C-47EA-BF5D-3500C93D5E20.jpeg
    7.9 KB · Views: 4
  • C5465728-2077-4ED3-B2F2-C338CF8E1F23.jpeg
    9.1 KB · Views: 4
  • 3E68CAC5-6443-4335-8877-BECBE02F49CA.jpeg
    8.1 KB · Views: 4
  • 5E1A1DD5-5664-424F-97B0-79CCFF5E92D6.png
    23.9 KB · Views: 5
  • F42B6404-6DB3-47A0-990A-F51AB7D864D5.jpeg
    8.4 KB · Views: 6
  • 780C8AF1-947B-456E-8466-CDA9B90FCA5B.png
    32.6 KB · Views: 5
Hivi inawezekana mtoto kumtoa shule za private na kwenda government?, ninavyojua ni mtoto kumtoa government kwenda private inawezekana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…