Transistor
JF-Expert Member
- Aug 8, 2013
- 1,061
- 1,637
Habari,
Tatizo la bili kubwa ya umeme kwa wateja limekuwa likiwasumbua sana.
Zipo sababu za matatizo ya kiufundi, lakini pia kuna sababu ambazo si za matatizo ya kiufundi.
Tunapokagua nyumba na kuona haina tatizo la kiufundi, huwa tunatazama sababu nyingine ambazo pia huchangia tatizo hilo.
Zifuatazo ni baadhi ya sababu tulizogundua zinapelekea tatzo hili, nje ya sababu za kiufundi.
1. Matumizi ya vifaa vya kielectronics ambavyo vinatumia teknolojia ya zamani (Old technology).
Mfano T? hasa hasa PLASMA TV.
"Plasma TVs typically use 20 percent more energy than similarly sized LCD models."
Tv za zamani hasa flat tv, matumizi ya umeme ni mkubwa sana,unakuta mteja ana TV, ambayo ni ya kizamani flat ambayo ina watt 150, inch 28 tu.
Tv kama hii ikiwaka masaa 10 tu inakuwa imetumia zaidi ya unit 1.5, ambapo kwa mwezi ni zaidi ya unit 45.
2. Mafriji na mafriza yenye matatizo katika mfumo wa vipimajoto (thermostart).
Mafriji au mafriza yaliochakaa au yale ya mitumba asilimia kubwa yamekuwa na tatizo la vifaa vyake vinavyoratibu joto.
Kasoro hii husababisha friji au friza husika. kuendelea kuwaka hata pale ubaridi husika unapokuwa umefikiwa, sababu vitambuzi joto vinakuwa havifanyi kazi vizuri, hivyo kuongeza gharama isiyo ya lazima katika bill yako ya umeme.
Fahamu friji na friza ambayo mfumo wake wa kiratibu joto kipo sawa huwasha na kuzima mfumo wake wa kupooza "automatic" kulingana na kiasi cha ubaridi kilichosetiwa.
Kitendo cha kujizima husaidia kupunguza matumizi ya umeme
Pia umeme mdogo, uchakavu wa mipila ya milango, au kupungua sana kwa gesi, huchochea zaidi matumizi ya umeme kwa vifaa hivi.
3. Matumizi ya energy saver aina ya CFL, baada ya mabadiliko ya aina za taa kutoka katika filament bulb, watu wengi walifunga energy saver hizi za CFL (maarufu kama za utumbo).
Energy saver hizi tayari zimeshapata mshindani ambae ni LED(licha ya kuwa na madhara katika macho), ambapo kwa taa moja ya watt 40 ya CFL, unapata taa 4 zenye mwanga sawa na CFL, hiyo moja kwa maana nyingine kama chumba kimoja ulikua unafunga CFL 1 ya watt 40,sasa kwa hiyohiyo watt 40, utaweza kuhudumia mwanga vyumba vinne kwa LED zenye mwanga uleule lakini zenye wat 10, kila moja.
Hivyo watu wabadilike kutoka katika CFL, waje katika LED lamps (taa zetu wabana matumizi).
4. Kuacha vitu "standby", siku hizi watu hawazimi vifaa vya umeme, asilimia kubwa ya vifaa vinaachwa standby sababu vingi vinatumia remote control.
5. Wanafamilia wanao shinda nyumbani.
Wewe na mtu mwingine mnaweza kuwa na vifaa sawa, ila mmoja ana familia inayoshinda nyumbani mwingine hana, yule mwenye familia inakaa nyumbani lazima matumizi yake yatakuwa makubwa sababu lazima Tv na radio zitatumika zaidi, hii ndiyo maana kipindi cha likizo watoto wakirudi moja ya vitu vinavyoongezeka huwa ni bili ya umeme.
Eng.Transistor.