Washing machine zipo katika makundi mawili. Automatic (fully) na semi automatic (manual).
1. Semi automatic washing machine ni mashine ya kufulia inayofanya kazi kwa wewe kuisaidia. Yani kila hatua katika ufuaji inahitaji ushiriki wako.
Mara nyingi zina vyumba viwili. Cha kufulia na kukaushia.
Huwa zina kuja na mpira wa maji (water inlet pipe) na tundu la kuchomeka.
View attachment 1662225
Ushiriki wako ni kama ifuatavyo.
-Unaanza kwa kuweka maji. Unaweza kuweka kwa ndoo au ukachomeka mpira wake direct bombani. Hapa kiasi cha maji unakadiria mwenyewe.
- Then unaweka sabuni. Yaweza kuwa ya unga au ya maji. Then washa kidogo kukoroga halafu weka nguo. Bonyeza ifue. Muda unaset mwenyewe (unakadiria kulingana na uchafu na ugumu wa nguo).
-ikimaliza kufua, unabonyeza inamwaga maji then unaweka mengine inasuuza.
-Baada ya kusuuza unaweza amua kuhamishia nguo chumba cha pili cha mashine ikamue (hata hadi kukausha ukipenda).
Faida za Semi-automatic
a. Ni bei nafuu kuliko full-automatic.
b. Unaokoa maji maana unajipimia mwenyewe unavyoona.
c. Inasevu umeme kwa kuwa hatua zote za ufuaji unajipangia mwenyewe.
d. Si lazima kuwa na maji ya bomba direct. Unaweza weka mwenyewe.
e. Hufua kwa muda mfupi.
f. Haina vifaa vingi hivyo si rahisi kuharibika haribika.
Hasara zake
a. Haiwezi fanya kazi yenyewe. Lazima uisadie.
b. Zoezi la kuweka maji, kumwaga maji, kutoa nguo ili kukamua laweza sababisha maji kumwagika mwagika. Usipokuwa makini unaweza leta shot (kama ni mzembe kupitiliza).
c. Inatakatisha nguo ila haifikii automatic.
2. Automatic washing machine
Kama ilivyo jina lake. Inafanya kazi zote yenyewe. Huwa ina chumba kimoja tu. Zipo za kuweka nguo mbele na zipo za juu. (Front loading and top loading)
View attachment 1662226
View attachment 1662227
Unaunganisha mpira kwenye bomba. Unaweka nguo na sabuni. Unachagua ifanye yenyewe au uichagulie settings. Kama utaichagulia unaweza chagua kiwango cha maji, muda wa kufua, aina ya nguo n.k.
Ukisharuhusu ifue, itafanya yote yenyewe. Baada ya muda unaenda kutoa nguo zikiwa tayari.
Faida
a. Inafanya yote yenyewe. Unaweka nguo na kuondoka.
b. Inatakatisha zaidi
c. Teknolojia ya kisasa.
d. Inachukua nafasi ndogo ndani.
Hasara.
a. Ni ghali.
b. Maji mengi kwa kuwa inajipimia.
c. Umeme mwingi kwakuwa inafanya yote yenyewe kwa umeme.
d. Inafua kwa muda mrefu sana. inaweza fika hadi saa nzima.
e. Kinachokadiria maji, uzito wa nguo, kiasi cha sabuni n.k ni sensor. Wakati mwingine sensor hufa.
f. Inahitaji maji direct bombani ili ijichukulie. Huwezi chota na ndoo
NB: kwa familia ya kipato cha kati hizi mashine ni bidhaa muhimu na si anasa. Kufua ni kazi ngumu hata kama akina mama hawalalamiki. Kwa shilingi laki 3 au zaidi inaweza okoa nguvu na muda.