Mrejesho: Haya ni matatizo mbalimbali tuliyoyagundua katika baadhi ya nyumba zenye tatizo la bili kubwa ya umeme

Mrejesho: Haya ni matatizo mbalimbali tuliyoyagundua katika baadhi ya nyumba zenye tatizo la bili kubwa ya umeme

Transistor

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2013
Posts
1,061
Reaction score
1,637
Habari,

Tatizo la bili kubwa ya umeme kwa wateja limekuwa likiwasumbua sana.

Zipo sababu za matatizo ya kiufundi, lakini pia kuna sababu ambazo si za matatizo ya kiufundi.

Tunapokagua nyumba na kuona haina tatizo la kiufundi, huwa tunatazama sababu nyingine ambazo pia huchangia tatizo hilo.

Zifuatazo ni baadhi ya sababu tulizogundua zinapelekea tatzo hili, nje ya sababu za kiufundi.

1. Matumizi ya vifaa vya kielectronics ambavyo vinatumia teknolojia ya zamani (Old technology).

Mfano T? hasa hasa PLASMA TV.

"Plasma TVs typically use 20 percent more energy than similarly sized LCD models."

Tv za zamani hasa flat tv, matumizi ya umeme ni mkubwa sana,unakuta mteja ana TV, ambayo ni ya kizamani flat ambayo ina watt 150, inch 28 tu.

Tv kama hii ikiwaka masaa 10 tu inakuwa imetumia zaidi ya unit 1.5, ambapo kwa mwezi ni zaidi ya unit 45.

2. Mafriji na mafriza yenye matatizo katika mfumo wa vipimajoto (thermostart).

Mafriji au mafriza yaliochakaa au yale ya mitumba asilimia kubwa yamekuwa na tatizo la vifaa vyake vinavyoratibu joto.

Kasoro hii husababisha friji au friza husika. kuendelea kuwaka hata pale ubaridi husika unapokuwa umefikiwa, sababu vitambuzi joto vinakuwa havifanyi kazi vizuri, hivyo kuongeza gharama isiyo ya lazima katika bill yako ya umeme.

Fahamu friji na friza ambayo mfumo wake wa kiratibu joto kipo sawa huwasha na kuzima mfumo wake wa kupooza "automatic" kulingana na kiasi cha ubaridi kilichosetiwa.

Kitendo cha kujizima husaidia kupunguza matumizi ya umeme

Pia umeme mdogo, uchakavu wa mipila ya milango, au kupungua sana kwa gesi, huchochea zaidi matumizi ya umeme kwa vifaa hivi.

3. Matumizi ya energy saver aina ya CFL, baada ya mabadiliko ya aina za taa kutoka katika filament bulb, watu wengi walifunga energy saver hizi za CFL (maarufu kama za utumbo).

Energy saver hizi tayari zimeshapata mshindani ambae ni LED(licha ya kuwa na madhara katika macho), ambapo kwa taa moja ya watt 40 ya CFL, unapata taa 4 zenye mwanga sawa na CFL, hiyo moja kwa maana nyingine kama chumba kimoja ulikua unafunga CFL 1 ya watt 40,sasa kwa hiyohiyo watt 40, utaweza kuhudumia mwanga vyumba vinne kwa LED zenye mwanga uleule lakini zenye wat 10, kila moja.

Hivyo watu wabadilike kutoka katika CFL, waje katika LED lamps (taa zetu wabana matumizi).

4. Kuacha vitu "standby", siku hizi watu hawazimi vifaa vya umeme, asilimia kubwa ya vifaa vinaachwa standby sababu vingi vinatumia remote control.

5. Wanafamilia wanao shinda nyumbani.

Wewe na mtu mwingine mnaweza kuwa na vifaa sawa, ila mmoja ana familia inayoshinda nyumbani mwingine hana, yule mwenye familia inakaa nyumbani lazima matumizi yake yatakuwa makubwa sababu lazima Tv na radio zitatumika zaidi, hii ndiyo maana kipindi cha likizo watoto wakirudi moja ya vitu vinavyoongezeka huwa ni bili ya umeme.

Eng.Transistor.
 
Habari,

Tatizo la bili kubwa ya umeme kwa wateja limekua likiwasumbua sana.

Zipo sababu za matatizo ya kiufundi,lakini pia kuna sababu ambazo si za matatizo ya kiufundi.

Tunapokagua nyumba na kuona haina tatizo la kiufundi,hua tunatazama sababu nyingine ambazo pia huchangia tatizo hilo.

Zifuatazo ni moja ya sababu tulizo gundua zinapelekea tatzo hili,nje ya sababu za kiufundi.

1.Matumizi ya vifaa vya kielectronics ambavyo vinatumia tekinolojia ya zamani(Old technology).

Mfano TV hasa hasa PLASMA TV.

"Plasma TVs typically use 20 percent more energy
than similarly sized LCD
models."

Tv za zamani hasa flat tv,matumizi ya umeme ni mkubwa sana,unakuta mteja ana TV,ambayo ni ya kizamani flat ambayo ina watt 150,nch 28 tu.

Tv kama hii ikiwaka masaa 10 tu inakua imetumia zaidi ya unit 1.5,ambapo kwa mwezi ni zaidi ya unit 45.

2.Mafriji na mafriza yenye matatizo katika mfumo wa vipimajoto(thermostart).

Mafriji au mafriza yaliochakaa au yale ya mitumba asilimia kubwa yamekuwa na tatizo la vifaa vyake vinavyo ratibu joto.

Kasoro hii husababisha friji au friza husika. kuendelea kuwaka hata pale ubaridi husika unapokuwa umefikiwa,sababu vitambuzi joto vinakua havifanyi kazi vizuri,hivyo kuongeza gharama isiyo ya lazima katika bill yako ya umeme.

Fahamu friji na friza ambayo mfumo wake wa kiratibu joto kipo sawa huwasha na kuzima mfumo wake wa kupooza "automatic"kulingana na kiasi cha ubaridi kilicho setiwa.

Kitendo cha kujizima husaidia kupunguza matumiz ya umeme

Pia umeme mdogo,uchakavu wa mipila ya milango,au kupungua sana kwa gesi,huchochea zaidi matumizi ya umeme kwa vifaa hivi.

3.Matumizi ya energy saver aina ya CFL,baada ya mabadiliko ya aina za taa kutoka katika filament bulb,watu wengi walifunga energy saver hizi za CFL (maarufu kama za utumbo).

Energy saver hizi tayari zimeshapata mshindani ambae ni LED(licha ya kuwa na madhara katika macho),ambapo kwa taa moja ya watt 40 ya CFL,unapata taa 4 zenye mwanga sawa na CFL,hiyo moja kwa maana nyingine kama chumba kimoja ulikua unafunga CFL 1 ya watt 40,sasa kwa hiyohiyo watt 40,utaweza kuhudumia mwanga vyumba vinne kwa LED zenye mwanga uleule lakini zenye wat 10,kila moja

Hivyo watu wabadilike kutoka katika CFL,waje katika LED lamps(taa zetu wabana matumz).

4.Kuacha vitu "standby",siku hizi watu hawazimi vifaa vya umeme,asilimia kubwa ya vifaa vinaachwa standby sababu vingi vinatumia remote control.

5.Wanafamilia wanao shinda nyumbani.

Wewe na mtu mwingne mnaweza kuwa na vifaa sawa,ila mmoja anafamilia inayoshinda nyumbani mwingine hana,yule mwenye familia inakaa nyumbani lazma matumiz yake yatakuwa makubwa sababu lazima tv na radio zitatumika zaidi,hii ndiyo maana kipindi cha likizo watoto wakirudi moja ya vitu vinavyoongezeka hua ni bili ya umeme.

Eng.Transistor.
Sababu kubwa hujaisema, vifaa vyote tunavyotumia ni vya kizamani na Energe Eficency yake ni kuanzia Klass D na kuendelea. Vyombo vingi vipya na vya Kisasa Energy Efficency yake ni Klass A+++
Tofauti ya matumizi ya umeme Kutoka Klass D hadi A+++ ni Zaidi ya mara 3
 
Kuna wanaoacha mafeni wazi,huu mtindo upon nyumba nyingi.Anaweza mtu mzima au mtoto akawasha feni chumbani,akatoka bila kuzima,akaenda varanda akawasha feni ,akaondoka,akaenda chumba kingine hivyo hivyo.Unaweza ukakuta vyumba vitatu na varanda mafeni yanafanyakazi,bila kuweko mtu chumbani au vyaranda.
 
Back
Top Bottom