Mrejesho: Haya ni matatizo mbalimbali tuliyoyagundua katika baadhi ya nyumba zenye tatizo la bili kubwa ya umeme

Habari,

Tatizo la bili kubwa ya umeme kwa wateja limekuwa likiwasumbua sana.

Zipo sababu za matatizo ya kiufundi, lakini pia kuna sababu ambazo si za matatizo ya kiufundi.

Tunapokagua nyumba na kuona haina tatizo la kiufundi, huwa tunatazama sababu nyingine ambazo pia huchangia tatizo hilo.

Zifuatazo ni baadhi ya sababu tulizogundua zinapelekea tatzo hili, nje ya sababu za kiufundi.

1. Matumizi ya vifaa vya kielectronics ambavyo vinatumia teknolojia ya zamani (Old technology).

Mfano T? hasa hasa PLASMA TV.

"Plasma TVs typically use 20 percent more energy than similarly sized LCD models."

Tv za zamani hasa flat tv, matumizi ya umeme ni mkubwa sana,unakuta mteja ana TV, ambayo ni ya kizamani flat ambayo ina watt 150, inch 28 tu.

Tv kama hii ikiwaka masaa 10 tu inakuwa imetumia zaidi ya unit 1.5, ambapo kwa mwezi ni zaidi ya unit 45.

2. Mafriji na mafriza yenye matatizo katika mfumo wa vipimajoto (thermostart).

Mafriji au mafriza yaliochakaa au yale ya mitumba asilimia kubwa yamekuwa na tatizo la vifaa vyake vinavyoratibu joto.

Kasoro hii husababisha friji au friza husika. kuendelea kuwaka hata pale ubaridi husika unapokuwa umefikiwa, sababu vitambuzi joto vinakuwa havifanyi kazi vizuri, hivyo kuongeza gharama isiyo ya lazima katika bill yako ya umeme.

Fahamu friji na friza ambayo mfumo wake wa kiratibu joto kipo sawa huwasha na kuzima mfumo wake wa kupooza "automatic" kulingana na kiasi cha ubaridi kilichosetiwa.

Kitendo cha kujizima husaidia kupunguza matumizi ya umeme

Pia umeme mdogo, uchakavu wa mipila ya milango, au kupungua sana kwa gesi, huchochea zaidi matumizi ya umeme kwa vifaa hivi.

3. Matumizi ya energy saver aina ya CFL, baada ya mabadiliko ya aina za taa kutoka katika filament bulb, watu wengi walifunga energy saver hizi za CFL (maarufu kama za utumbo).

Energy saver hizi tayari zimeshapata mshindani ambae ni LED(licha ya kuwa na madhara katika macho), ambapo kwa taa moja ya watt 40 ya CFL, unapata taa 4 zenye mwanga sawa na CFL, hiyo moja kwa maana nyingine kama chumba kimoja ulikua unafunga CFL 1 ya watt 40,sasa kwa hiyohiyo watt 40, utaweza kuhudumia mwanga vyumba vinne kwa LED zenye mwanga uleule lakini zenye wat 10, kila moja.

Hivyo watu wabadilike kutoka katika CFL, waje katika LED lamps (taa zetu wabana matumizi).

4. Kuacha vitu "standby", siku hizi watu hawazimi vifaa vya umeme, asilimia kubwa ya vifaa vinaachwa standby sababu vingi vinatumia remote control.

5. Wanafamilia wanao shinda nyumbani.

Wewe na mtu mwingine mnaweza kuwa na vifaa sawa, ila mmoja ana familia inayoshinda nyumbani mwingine hana, yule mwenye familia inakaa nyumbani lazima matumizi yake yatakuwa makubwa sababu lazima Tv na radio zitatumika zaidi, hii ndiyo maana kipindi cha likizo watoto wakirudi moja ya vitu vinavyoongezeka huwa ni bili ya umeme.

Eng.Transistor.
Mweshimiwa ulinisaidia na unazidi kunisaidia asante gad saiv mm ni fundi electronics bila kusoma nitaelezea kwenye uzi maalum

Qn
 
Na kuna wateja ngangari hawashauriki
[emoji23][emoji23][emoji23]dawa yao nilisuka step down transiformer nika nunua betri N200 nikafunga charger control nika imodify ikijaza betry ina zima na transiformer pia yan umeme ukiisha mm natumia kila kitu geto kwangu kana kawa na umeme wajanikatia nikaiba tena hapo ndio walijuta.

Qn
 
Washing machine ni baba lao.

dodge
Ok mi nataka kununua hiyo mashine vipi mambo ya kufua mashuka na mataulo na ma jeans na ma boxer kibao je inakula sana moto nipe uzoefu. Mi naona bora kuipangia bajeti.
 
Habari,

Tatizo la bili kubwa ya umeme kwa wateja limekuwa likiwasumbua sana.

Zipo sababu za matatizo ya kiufundi, lakini pia kuna sababu ambazo si za matatizo ya kiufundi.

Tunapokagua nyumba na kuona haina tatizo la kiufundi, huwa tunatazama sababu nyingine ambazo pia huchangia tatizo hilo.

Zifuatazo ni baadhi ya sababu tulizogundua zinapelekea tatzo hili, nje ya sababu za kiufundi.

1. Matumizi ya vifaa vya kielectronics ambavyo vinatumia teknolojia ya zamani (Old technology).

Mfano T? hasa hasa PLASMA TV.

"Plasma TVs typically use 20 percent more energy than similarly sized LCD models."

Tv za zamani hasa flat tv, matumizi ya umeme ni mkubwa sana,unakuta mteja ana TV, ambayo ni ya kizamani flat ambayo ina watt 150, inch 28 tu.

Tv kama hii ikiwaka masaa 10 tu inakuwa imetumia zaidi ya unit 1.5, ambapo kwa mwezi ni zaidi ya unit 45.

2. Mafriji na mafriza yenye matatizo katika mfumo wa vipimajoto (thermostart).

Mafriji au mafriza yaliochakaa au yale ya mitumba asilimia kubwa yamekuwa na tatizo la vifaa vyake vinavyoratibu joto.

Kasoro hii husababisha friji au friza husika. kuendelea kuwaka hata pale ubaridi husika unapokuwa umefikiwa, sababu vitambuzi joto vinakuwa havifanyi kazi vizuri, hivyo kuongeza gharama isiyo ya lazima katika bill yako ya umeme.

Fahamu friji na friza ambayo mfumo wake wa kiratibu joto kipo sawa huwasha na kuzima mfumo wake wa kupooza "automatic" kulingana na kiasi cha ubaridi kilichosetiwa.

Kitendo cha kujizima husaidia kupunguza matumizi ya umeme

Pia umeme mdogo, uchakavu wa mipila ya milango, au kupungua sana kwa gesi, huchochea zaidi matumizi ya umeme kwa vifaa hivi.

3. Matumizi ya energy saver aina ya CFL, baada ya mabadiliko ya aina za taa kutoka katika filament bulb, watu wengi walifunga energy saver hizi za CFL (maarufu kama za utumbo).

Energy saver hizi tayari zimeshapata mshindani ambae ni LED(licha ya kuwa na madhara katika macho), ambapo kwa taa moja ya watt 40 ya CFL, unapata taa 4 zenye mwanga sawa na CFL, hiyo moja kwa maana nyingine kama chumba kimoja ulikua unafunga CFL 1 ya watt 40,sasa kwa hiyohiyo watt 40, utaweza kuhudumia mwanga vyumba vinne kwa LED zenye mwanga uleule lakini zenye wat 10, kila moja.

Hivyo watu wabadilike kutoka katika CFL, waje katika LED lamps (taa zetu wabana matumizi).

4. Kuacha vitu "standby", siku hizi watu hawazimi vifaa vya umeme, asilimia kubwa ya vifaa vinaachwa standby sababu vingi vinatumia remote control.

5. Wanafamilia wanao shinda nyumbani.

Wewe na mtu mwingine mnaweza kuwa na vifaa sawa, ila mmoja ana familia inayoshinda nyumbani mwingine hana, yule mwenye familia inakaa nyumbani lazima matumizi yake yatakuwa makubwa sababu lazima Tv na radio zitatumika zaidi, hii ndiyo maana kipindi cha likizo watoto wakirudi moja ya vitu vinavyoongezeka huwa ni bili ya umeme.

Eng.Transistor.
duka lako la vifaa vya kieleltroniki lipo wapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna wanaoacha mafeni wazi,huu mtindo upon nyumba nyingi.Anaweza mtu mzima au mtoto akawasha feni chumbani,akatoka bila kuzima,akaenda varanda akawasha feni ,akaondoka,akaenda chumba kingine hivyo hivyo.Unaweza ukakuta vyumba vitatu na varanda mafeni yanafanyakazi,bila kuweko mtu chumbani au vyaranda.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kweli kabisa
 
Nilikuwa na mpango wa kutafuta washing machine ya 9kg kumbe naongeza matumizi makubwa.
Inategemea na aina ya mashine, ya dada yangu round moja ya kufua hata haizungushi unit moja ya umeme. Vifaa vingi vipya vya umeme vimetengenezwa kutokula umeme mwingi so just buy a new one achana na electronics za mtumba.
 
[emoji23][emoji23][emoji23]dawa yao nilisuka step down transiformer nika nunua betri N200 nikafunga charger control nika imodify ikijaza betry ina zima na transiformer pia yan umeme ukiisha mm natumia kila kitu geto kwangu kana kawa na umeme wajanikatia nikaiba tena hapo ndio walijuta.

Qn
Kumbe wizi nao ni jambo la kujisifia.
Sawa Mr Kilimanjaro naona tendo limesadifu jina lako
 
Wiring ni tatizo,kuna nyumba zimefanyiwa wiring za kizamani mfano mahali pa kutumia electrical cable ya 2 panatumika 1.5.

Huwa wataalamu wa umeme wanashauri 1.5 waya utumike kwenye taa na vitu ambavyo avitumii umeme mwingi.

Madhara yake ni kupunguza efficiency ya kifaa husika nakupelekea umeme kwenda mwingi mfano freezer badala ya kuchukua Massa 5 kugandisha linaweza chukua mpaka 5days kufreeze kiasi fulani cha mzigo kilichobeba .

Ila kwa nyumba za kupanga unaweza ongea na landloard ukatumia sub meter bei yake ni simple tu 35,000/= hii inasoma kiasi cha umeme ulichotumia.
 
Back
Top Bottom