Jembe halimtupi mkulima , huu msemo umetamalaki sana hapa kwetu tz, lakini Mara kadhaa huwa unakuwaga na ukweli ndani yake.
Msimu wa 2018/19 nilijaribu kulima mpunga bahi hekari 5, japo nilikodi hekari 12 na kuzitifua zote kwa trekta, ila nikakumbana na ukame wakat napandikiza. Nilifanikiwa kuoandikiza mashamba matano tu, maji yakawa yameisha, hivyo nikawa Sina jinsi.
Si haba katika heka hizo tano nimeweza kurudisha mbegu, nimepata magunia 54, yenye ujazo wa debe saba Saba 7,7. Kiukweli nashukuru San mungu Kwan mwaka huu ulikuwa na changamoto sana. Wngine hawakuweza KUVUNA kabisa hata Lita moja.
Nimezidi kunifunza mengi katika kilimo ndugu zangu, wakati mm nimepata vigunia 54, Kuna mtu kapata migunia 400, na mwingine migunia 600, hivyo ukiwa kupanda uhakika wa kupiga pesa kupitia kilimo INAWEZEKANA.
Nimeona si haba niwaletee mrejesho wananzengo kwani Kuna baadhi ya wanajf walitaka mrejesho Mara baada ya kutoka shambani.
Picha hizi hapa.
View attachment 1148431View attachment 1148432View attachment 1148433View attachment 1148434View attachment 1148435View attachment 1148436View attachment 1148437View attachment 1148438View attachment 1148440View attachment 1148444