Mrejesho: Kuagiza rice combine harvester toka China

Mrejesho: Kuagiza rice combine harvester toka China

Watanzania tulivyo wehu, wengi wetu tunatumia kiasi kama hicho kuagiza Mark II na shughuli zako ni ajira ya take home less than 2 Million!
Ni priorities tu mkuu, wote tuna macho ila kila mtu anaona vitu tofauti.
 
Ok. Ahsante sn. Ubarikiwe ndg. Kila la kheri.

Baada ya hapo nunua mashamba huko ulime mwenyewe na ununue trekta. Muda si mrefu utakuwa Bhakressa.
 
Vipi umenunua na kusafirisa toka katika kampuni gani? na jina halisi la hizo za mkanda(zisizotumia matairi) zinaitwaje kwa kizungu.
 
12000$×2100 tsh=25,200,000tsh.
Unapoandika 3.5 nafikiri unamaanisha 3,500,000.Hivyo mpaka sasa umetuchanganya na wanaofikiri wamekuelewa bado hawajakufuatilia vizuri,plz bwana IPYAX sahihisha hapo tujue
 
Mnamo mwezi wa kwanza mwaka huu nilianzisha mada hapa jukwaani nikiomba ushauri wa kuagiza mashine toka China. Ishu ilikua niende China au niagize kwa mtandao kupitia Alibaba.

Nilipata ushauri wa kutosha tu huku wengine wakiniasa kwamba Alibaba nita tapeliwa hela bora tu niende China. Bahati mbaya budget yangu ilikua ndogo kwahiyo nisingeweza weza kwenda China basi nikaamua kuagiza kupitia Alibaba.

Namshukuru mungu mashine yangu ilifika salama kama wiki 2 zilizo pita na sasa nipo shamba napiga kazi. Napenda kutoa ushauri tu kwamba Alibaba wapo vizuri sana katika buyer's protection kwa hiyo risk ya kutapeliwa ni ndogo sana na kama una maswali usisite kuuliza.

View attachment 346004

View attachment 346005

View attachment 346006
12000$×2100 tsh=25,200,000tsh.
Unapoandika 3.5 nafikiri unamaanisha 3,500,000.Hivyo mpaka sasa umetuchanganya na wanaofikiri wamekuelewa bado hawajakufuatilia vizuri,plz bwana IPYAX sahihisha hapo tujue
 
5 m utalima heka 5 kule kwenye mashamba ya shirika ila lazima uwahi kuomba vibali vya kukodi. Heka 5 itakupa returned gunia 30 kwa kila heka ambazo jumla zitakua gunia 150. Ukiuza kuanzia mwezi wa 8 gunia 1 ni sh laki 1 ukifika December gunia 1 ni 150. Faida ipo kubwa tu.

Hata mimi ndio najifunza hivi sasa kama una maswali ambayo sina majibu basi ntauliza wadau hapa kwa info zaidi. Karibu sana
Mkuu samahani,hizi gunia 30 kwa heka ni za mpunga ama mchele namaanisha baada yakukoboa?
 
Nadhani kwa wakulima wadogo hii ni nzuri pia......

hqdefault.jpg
 
Asante mkuu ila pia maamuzi magumu ili yafanyike ni lazima utoke katika comfort zone. Mjini kuna fursa nyingi na bata pia ila shamba kuna fursa kubwa zaidi na uamuzi wa kuhamisha kambi kwenda bush sio rahisi hata kidogo.
Waambie mkuu wazee wa Pool Table
 
Back
Top Bottom