Mrejesho: Maneno ya kejeli ya mume wangu

Mrejesho: Maneno ya kejeli ya mume wangu

Ni siku nyingi zimepita ,nimeona ni vyema nitoe mrejesho. Kesi ilimalizika mwaka 2017, na nilipata talaka yangu, hilo ndilo jambo la msingi kwangu.

Alifanikiwa kuchukua gari polisi maana polisi walisema ni kesi ya madai na sio ya jinai. Baada ya kuchukua gari alienda kuiuza na kununua gari jingine. Nalo likapata ajali akaliuza kwa bei ya hasara , sasa hivi yupo tu mtaani. Nyumba alibaki nayo na mimi nikabaki na kiwanja.

Mwaka jana aliwaambia wazazi wake anataka kuja kuomba msamaha sababu anaona maisha yake yamekuwa na mikosi na hajaweza kufanikiwa toka tumeachana. Wazazi wakamuambia anitafute mwenyewe, ila hakufanya hivyo sababu anaona aibu. Mimi nilishamsamehe, ingawa hakuwahi kuja kuomba msamaha.

Ni yeye kutubu kwa Mungu wake. Nishamove on, na niliweza kufanya mendeleo mengine mengi. Mungu amenipa vibgi zaidi. Nashukuru sana kwa michango yenu

Soma zaidi
Soma tena: Mrejesho: Maneno ya kejeli ya mume wangu
Mbona kama unafurahia anachopitia mwamba ,au ndio ulimuendea kwa sangoma nini ,shida kupokezana tuliza mshono
 
Atajijua mwenyewe. Sijaenda hata kwa Sangoma, yote hayo ya nini.
Bado una makasiriko na hii ni nature ya wanawake wengi ,samahani sikuandami ila all in all potezea tu na hapakua na haja ya kuja kuyaanika hapa hili game linabadilika tu kama paredi kwa kitendo kimoja tu cha nyuma geuka. Shida hua zinamjenga mtu na kumpa ukomavu wa maisha na ndio mda anaoupitia x wako .
Je paredi ikigeuka utakua tayari kuja kutusimulia hapa unayopitia au ndio madawati ya ujinsia na ustawi wa jamii patahusika ukitadai usaidizi wa malezi? ( kama mlizaa pamoja).
 
Paredi ligeuke kwa sababu gani. Kwani nimemfanyia thulma yoyote. Mtu akuibie kwa maksudi itawezaje kisahau. Ndio nature ya binadamu.
 
Kwa hiyo hukuridhika kuachwa ukaamua umroge ili aanguke?
 
Kwa hiyo hukuridhika kuachwa ukaamua umroge ili aanguke?
Hahahah sasa umroge mtu kwa lipi sasa. Sina muda huo. Toka tulipooana na nikaondoka pale wale sikuwahi kwenda kwa mganga. Kaanguka kwa sababu zingine na Mungu ndio anajua kwa nini.
 
Back
Top Bottom